#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

serikali ya mabavu ya ccm walifanya big mistake kumtishia Gwaajima na kamati za bunge,wangekuwa weledi wangeunda kamati ya wataalam wa afya na kumuita Gwajima na kuzungumza tena live huku watanzania wote tukiona,sichanji wala sina mpango kabisa
 
Nasema hili , na huu na mtazamo binafsi.

Kuna watu wengi sana hawajaona umuhimu wa kupata chanjo.

Lakini bado, wataalamu wetu wa afya wameshindwa kuja na ushawishi wa kwanini ni muhimu kupata chanjo, kuna watu hawana elimu za Afya na wanabaki na swali ambalo hadi sasa halijajibiwa kwa usahihi kuwa Kwanini watu waliochanjwa wanaweza kupata maambukiz sawa na watu ambao hawajapata chanjo, kwanini waliochanjwa wanapaswa kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari sawa na watu ambao bado hawajachanjwa?
 
Pamoja na kuwa kuchanja ni hiari lakini muitikio wa watu ni mdogo sana. Wataalamu wa Public health wafanye hamasa ya kuelimisha jamii.

posters au mabngo, Instagram na redio na TV.
 
Jamii Forums inakukaribisha kwenye Mjadala wa Ugonjwa wa UVIKO-19 na Waliopata Chanjo

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Clubhouse leo Septemba 2, 2021 kuanzia Saa 11:30 jioni hadi saa 2:00 usiku

Link: UVIKO-19: Mjadala wa waliopata Chanjo - JamiiForums

=====

UPDATES:
=====

=> Dkt. Elisha Osati: Kila siku napokea watu ambao wanataka niwahakikishie wakachanjwe. Sio kwamba hawataki ila wanataka uhakika Tukiendelea kutoa elimu itakuwa jambo zuri. Bahati mbaya hatutoi takwimu lakini tuna wagonjwa wengi katika Wodi zetu #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Aikande Kwayu: Wananchi hawawezi kuona tupo serious wakati kuna mikusanyiko mikubwa Ile imani ya kwamba ugonjwa upo, tukachanje lazima tuoneshe hatari ya ugonjwa na tuoneshe tupo serious kupambana #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Aikande Kwayu: Ni muhimu 'ku-engage' Viongozi wa Dini kwa nguvu sana kuhakikisha chanjo inaongelewa Misikitini au Kanisani Issue ya wasiwasi wa chanjo sio Tanzania tu ni duniani #JamiiTalks #UVIKO3

=> Neema Lugangira: Tunahitaji Wataalamu wetu wa Afya kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi. Vituo vya Afya vipo ngazi zote #JamiiTalks #UVIKO3

=> Mbaraka Islam: Sisi kama Vyombo vya Habari tuna wajibu mkubwa kusaidia jamii. Hili suala linahusu maisha ya watu Tufike mahala tuchukulie hii kama vita kwasababu watu wanakufa. Bahati mbaya tumeweka mzaha #JamiiTalks #UVIKO3

=> Mbaraka Islam: Wanahabari tuziache Habari zinazopotosha. Tuwatumie Wataalamu na wao wajitokeze mara kwa mara kwa kuandika makala, redio nk Sio lazima Serikali au Wabunge wafanye kazi, Watu wote wajitolee #JamiiForums #UVIKO3

=> Jeff Msangi: Tanzania ingeweza kujaribu kuondoa misinformation kwa kuondoa vitu mbalimbali Kitu ambacho naona kinasumbua kusaidia watu wengi wapate chanjo ni mixed messages. Takwimu zingeweza kusaidia watu kwenda kuchanja. Bila kupeleka taarifa kwa Umma ni sawa na kazi bure

=> Dkt. Francis Furia: Kumekuwa na mabadiliko kwa sasa hivi. Wizara ina timu ya wataalamu ambao wamekuwa wakiendesha vipindi vya TV na Redio Kuna jitihada imefanyika, changamoto ni kwamba ili tuweze kufanikiwa ni lazima iwe effort ya timu yote sio Wataalamu wa Afya pekee #UVIKO3

=> Semkae: Suala la trust kwenye chanjo ni muhimu. Mama akimwambia Binti bado hujazaa chanjo itakuletea madhara, binti hana budi kumuamini Familia na mtu anaposhinda ni jambo la kuzingatia, kama unashinda na watu wasioamini chanjo, hata daktari akisema ni salama hatomuamini

=> Neema Lugangira: Lipo kundi kubwa ambalo halijaamua kama linataka kuchanja au la, tunapaswa ku-focus kwenye kundi hilo Political will ipo kubwa sana, lakini lazima tuunganishe effort zote (Wanasiasa, Viongozi wa Dini, Wasanii nk) tuweze kuongea lugha moja #UVIKO3 #JamiiTalks

=> @DrMabula: Ni kwa muda mrefu takwimu za Maambukizi hazijatolewa na hata ukiuliza Wizarani ni kama kila Mtu anamtupia mwingine mpira Kuna Watu wanataka kupata Chanjo lakini kutokana na ratiba zao za majukumu muda wanaopata nafasi wanakuta hakuna Kituo ambacho kipo wazi #UVIKO3

=> Onesmo Ole Ngurumwa: Haifai kulazimisha watu kuchanja kwa sababu suala la afya ni suala binafsi > Lakini suala la COVID-19 ni tofauti kwa kuwa ni suala la kitaifa sio binafsi tena

=> Dkt. Namala: Watu wanaotoa taarifa za uongo wafuatwe na wahojiwe na wanahabari, wanaowapa taarifa pia wafuatwe na kuulizwa > Kisha wanahabari wajibu zile hoja za wote wanaotoa taarifa za uongo. Lakini tukiacha waongee tu, tutawagawa watu

=> Neema Lugangira: Tusiwe na hofu kuhusu chanjo zilizopo kuexpire. Hata Afrika Kusini batch kubwa ya kwanza ya chanjo iliexpire Tupo katika sensitive period ambayo chanjo imetambulika. Kuna kundi kubwa lipo katikati halijafanya maamuzi #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Elisha Osati: Hizi dozi za kwanza zinaweza zisifike malengo zikaexpire. Tuliochanja tukijitokeza zaidi na kuwa Mabalozi watu watachanja Ukimbadilisha mtu mmoja kwenye familia, wengine wanabadilika #JamiiTalks #UVIKO3

=> Onesmo Olengurumwa: Huenda tusifikie lengo la uchanjaji. Mentality ya kwamba Tanzania ni kisiwa na hatuwezi kuathiriwa ni kubwa sana Tulikosea kuamini kama Rais amechanja Watanzania wengine nao watachanja. Hatuna coordinated campaign ya watanzania kuchanjwa #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Francis: Tulikosea kukosa mpango wa namna ya kutoa chanjo kwa kudhani kwamba Rais akichanja basi watanzania watachanjo Lazima tuwe na kampeni ya kitaifa ya kuchanja kama tulivyokufa na kampeni ya kitaifa ya COVID-19

=> Neema Lugangira: Kwenye upotoshaji wa masuala ya #COVID19, kundi ambalo limeonekana moja kwa moja ni kundi ambalo hata mimi nimo Wataalamu wa Afya mnayo kazi kuhakikisha hakuna jumbe tofauti kati yenu nyuma wa pazia. Lipo kundi ambao halikubali chanjo #JamiiTalks #UVIKO3

View attachment 1921196View attachment 1921197View attachment 1921198View attachment 1921199View attachment 1921200View attachment 1921201View attachment 1921202View attachment 1921203View attachment 1921204View attachment 1921205
+
sijachanja sintashiriki
 
Hiyo mijadala mnapoteza muda tu, kwa dunia ya leo kunamtz ambaye hajui kuwa chanjo ya uvico tayari ipo nchini na kuchanjwa ni hiari?

1. Sichanji, kwasababu siyo lazima. Cd4 buku jero zinanitosha.
2. Covid nilishaugua, ni ugonjwa unaotibika wenyewe tu, yaan kama mafua tu. (USINIIGE)
3. Virusi vya covid naona kila siku wanaibuka generation mpya, nasubiri pia nipate hao akina delta, MU n.k ili nijipime kama naweza kuwashinda (Nitaweza tu if God wishez)

Nb, Personally sipendi kabisa kutumia dawa ovyoovyo hasa hizo za viwandani, ni baada ya wizara husika kuruhusu dawa za Quinine miaka hiyo kwaajili ya kutibu malaria na zikanipelekea uziwi permanently hadi leo. Never and never trust anybody.

OVER.
 
Mbali nakuangalia waliochanja na ambao hawajachanja ukizingatia Uviko-19 umeonekana ni gonjwa ambalo utakuwepo muda. Mpango gani uliopo wa wataalamu wetu wa Afya kuja na chanjo zetu kama Taifa ? Maana mataifa mengine tunaona wanakuja na chanjo zao. Tusisahau pia Taifa lipo katikati ilihali ni lazima ikitokea unataka kutoka nje ya nchi.
 
Jamii Forums inakukaribisha kwenye Mjadala wa Ugonjwa wa UVIKO-19 na Waliopata Chanjo

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika Clubhouse leo Septemba 2, 2021 kuanzia Saa 11:30 jioni hadi saa 2:00 usiku

Link: UVIKO-19: Mjadala wa waliopata Chanjo - JamiiForums

=====

UPDATES:

=====

=> Dkt. Elisha Osati: Kila siku napokea watu ambao wanataka niwahakikishie wakachanjwe. Sio kwamba hawataki ila wanataka uhakika Tukiendelea kutoa elimu itakuwa jambo zuri. Bahati mbaya hatutoi takwimu lakini tuna wagonjwa wengi katika Wodi zetu #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Aikande Kwayu: Wananchi hawawezi kuona tupo serious wakati kuna mikusanyiko mikubwa Ile imani ya kwamba ugonjwa upo, tukachanje lazima tuoneshe hatari ya ugonjwa na tuoneshe tupo serious kupambana #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Aikande Kwayu: Ni muhimu 'ku-engage' Viongozi wa Dini kwa nguvu sana kuhakikisha chanjo inaongelewa Misikitini au Kanisani Issue ya wasiwasi wa chanjo sio Tanzania tu ni duniani #JamiiTalks #UVIKO3

=> Neema Lugangira: Tunahitaji Wataalamu wetu wa Afya kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa sahihi. Vituo vya Afya vipo ngazi zote #JamiiTalks #UVIKO3

=> Mbaraka Islam: Sisi kama Vyombo vya Habari tuna wajibu mkubwa kusaidia jamii. Hili suala linahusu maisha ya watu Tufike mahala tuchukulie hii kama vita kwasababu watu wanakufa. Bahati mbaya tumeweka mzaha #JamiiTalks #UVIKO3

=> Mbaraka Islam: Wanahabari tuziache Habari zinazopotosha. Tuwatumie Wataalamu na wao wajitokeze mara kwa mara kwa kuandika makala, redio nk Sio lazima Serikali au Wabunge wafanye kazi, Watu wote wajitolee #JamiiForums #UVIKO3

=> Jeff Msangi: Tanzania ingeweza kujaribu kuondoa misinformation kwa kuondoa vitu mbalimbali Kitu ambacho naona kinasumbua kusaidia watu wengi wapate chanjo ni mixed messages. Takwimu zingeweza kusaidia watu kwenda kuchanja. Bila kupeleka taarifa kwa Umma ni sawa na kazi bure

=> Dkt. Francis Furia: Kumekuwa na mabadiliko kwa sasa hivi. Wizara ina timu ya wataalamu ambao wamekuwa wakiendesha vipindi vya TV na Redio Kuna jitihada imefanyika, changamoto ni kwamba ili tuweze kufanikiwa ni lazima iwe effort ya timu yote sio Wataalamu wa Afya pekee #UVIKO3

=> Semkae: Suala la trust kwenye chanjo ni muhimu. Mama akimwambia Binti bado hujazaa chanjo itakuletea madhara, binti hana budi kumuamini Familia na mtu anaposhinda ni jambo la kuzingatia, kama unashinda na watu wasioamini chanjo, hata daktari akisema ni salama hatomuamini

=> Neema Lugangira: Lipo kundi kubwa ambalo halijaamua kama linataka kuchanja au la, tunapaswa ku-focus kwenye kundi hilo Political will ipo kubwa sana, lakini lazima tuunganishe effort zote (Wanasiasa, Viongozi wa Dini, Wasanii nk) tuweze kuongea lugha moja #UVIKO3 #JamiiTalks

=> @DrMabula: Ni kwa muda mrefu takwimu za Maambukizi hazijatolewa na hata ukiuliza Wizarani ni kama kila Mtu anamtupia mwingine mpira Kuna Watu wanataka kupata Chanjo lakini kutokana na ratiba zao za majukumu muda wanaopata nafasi wanakuta hakuna Kituo ambacho kipo wazi #UVIKO3

=> Onesmo Ole Ngurumwa: Haifai kulazimisha watu kuchanja kwa sababu suala la afya ni suala binafsi > Lakini suala la COVID-19 ni tofauti kwa kuwa ni suala la kitaifa sio binafsi tena

=> Dkt. Namala: Watu wanaotoa taarifa za uongo wafuatwe na wahojiwe na wanahabari, wanaowapa taarifa pia wafuatwe na kuulizwa > Kisha wanahabari wajibu zile hoja za wote wanaotoa taarifa za uongo. Lakini tukiacha waongee tu, tutawagawa watu

=> Neema Lugangira: Tusiwe na hofu kuhusu chanjo zilizopo kuexpire. Hata Afrika Kusini batch kubwa ya kwanza ya chanjo iliexpire Tupo katika sensitive period ambayo chanjo imetambulika. Kuna kundi kubwa lipo katikati halijafanya maamuzi #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Elisha Osati: Hizi dozi za kwanza zinaweza zisifike malengo zikaexpire. Tuliochanja tukijitokeza zaidi na kuwa Mabalozi watu watachanja Ukimbadilisha mtu mmoja kwenye familia, wengine wanabadilika #JamiiTalks #UVIKO3

=> Onesmo Olengurumwa: Huenda tusifikie lengo la uchanjaji. Mentality ya kwamba Tanzania ni kisiwa na hatuwezi kuathiriwa ni kubwa sana Tulikosea kuamini kama Rais amechanja Watanzania wengine nao watachanja. Hatuna coordinated campaign ya watanzania kuchanjwa #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Francis: Tulikosea kukosa mpango wa namna ya kutoa chanjo kwa kudhani kwamba Rais akichanja basi watanzania watachanjo Lazima tuwe na kampeni ya kitaifa ya kuchanja kama tulivyokufa na kampeni ya kitaifa ya COVID-19

=> Neema Lugangira: Kwenye upotoshaji wa masuala ya #COVID19, kundi ambalo limeonekana moja kwa moja ni kundi ambalo hata mimi nimo Wataalamu wa Afya mnayo kazi kuhakikisha hakuna jumbe tofauti kati yenu nyuma wa pazia. Lipo kundi ambao halikubali chanjo #JamiiTalks #UVIKO3

=> Dkt. Francis: Kuwalazimisha watu kupata chanjo ni suala zuri, lakini kwa kuwa tunachanjo chache itakuwa haiwezekani kwa kuwa hazitoshi Ukiona juhudi zilizowahi kuwekwa kwenye vitambulisho vya wajasiriamali unaweza ukaona kuwa inawezekana kuwafikia watu wote

=> Dkt. Elisha Osati: Ni kweli mtu anaweza kuugua baada ya kupata chanjo. Malengo mapana ya chanjo sio tu usipate ugonjwa Lazima watu waelewe ukipata chanjo unaweza kuumwa, ila ugonjwa wako utakuwa very 'mild' #JamiiTalks #UVIKO3

View attachment 1921196View attachment 1921197View attachment 1921198View attachment 1921199View attachment 1921200View attachment 1921201View attachment 1921202View attachment 1921203View attachment 1921204View attachment 1921205
+
naona wapi mjadala?
 
Binafsi nimechanja Johnson kama miezi miwili iliyopita.nikiri kuwa niliipata nje ya nchi na kiukweli sijapata madhara yeyote na niseme tu unaedza pata mafua na kikohozi ama dalili za covid kwakuwa nimezungukwa na kundi kubwa la ambao hawana chanjo. Lakini bado naamini kuchanja ni bora zaidi kuliko ambaye hajapata chanjo. Watanzania wengi walijengewa hofu na rais marehemu Magufuli.
 
Back
Top Bottom