#COVID19 Yaliyojiri JamiiForums Clubhouse kwenye Mjadala wa UVIKO-19, Umechanja au haujachanja? Nini mtazamo wako?

Waliochanja wana hoja nyepesi sana.Ngoja tusubiri siku yetu watajua hawajui🤣🤣🤣
 
Kwanini wataalaamu wamekimbilia kwenye chambo badala ya kutafuta tiba ya ugonjwa?
Utaambiwa virus havina dawa. Lakini huko vijijini mtu akiugua mafua (flue - virus) kisha akatafutafuta majani ya mkaratusi wenye majani membamba akajifukiza anapona kesho yake. Sasa unajiuliza ni virus kweli ndivyo haviponyeshwi na ugonjwa!?
 
Huu mjadala ungedumu kwa muda wa siku tatu, napendekeza. Kwa wakati huo huo uliopendekezwa, ili kuwapata wadau waliojiandaa wengi zaidi.

Maana inaweza kutokea baadhi ya maswali muhimu yakakosa majibu au majibu yasijitosheleze.

Au kuna taarifa ilitolewa humu JF kabla, kuwajulisha watu?
Mimi naona ni bora hospital mgonjwa Wa corona akifaa watangazwe hapo kila mtu angeogopa na tahadhari ingechukuliwa kwakuwa nimeshuhudia zile familia zilizotoa taarifa watu wamechukuwa taadhari na viongozi waache tabia ya kuwapa RAIA hofu mimi nilichanja sikuona madhara yoyote by
 
Siyo kwa bahati mbaya
====
Vipi hoja ya wataalamu wetu wakishirikiana na serikali kutengeneza chanjo yetu limegusiwa kwanye mjadala!?

Ni suala jema.

Ni suala ambalo linaelekezwa kwa watu wa afya zaidi, ikiwa ni moja kwa moja kimjadala na kiutendaji.

Hili ni suala ambalo linahitaji utashi na utayari: kimaarifa, kisiasa na kiuchumi.

1: Kimaarifa: kuwa na wataalamu wa kutosha na teknolojia ya kuweza kuchenjua molecules za dawa na wadudu husika.

Hapa unatakiwa kujua katika kiwango cha seli, kitu gani kina athari gani kwenye seli level. Iwe chanya au hasi. (Molecules discovery). Ujue pia utaendelea kuizalishaje. Utaendelea kuzalisha si aina moja ya molecules bali tofauti kwa malengo tofauti.

2: Utashi wa kisiasa na uchumi
Huu ni uwekezaji ambao faida yake si ya leo. Ni ya vizazi vijavyo. Je tuko tayari kwa uwekezaji huu? Kwa mataifa ya wenzetu, si serikali bali makampuni makubwa na yenye mitaji mikubwa ndo yanafanya kazi hizi. Pamoha na haya pia yanajihusisha katika ugunduzi wa dawa mpya na kuzifanyia tafiti. Je twaweza kuanzisha na kuwekeza pesa kwaajili ya maarifa, teknilojia na muda?

4: Kutimiza vigezo
Ili kuwa na mazingira ya aina hiyo hakuna janjajanja. Ni lazima kutimiza vigezo kwani vitu hivi viko under a very scrutiny process. Utakachozalisha chochote uwe tayari kuonyesha ufanisi wake kwa vitendo na si blabla. Kama si hivyo, watu wanapigia chini utafiti wako hata kabla haujavuka level ya kutoka maabara kwenda kwa wanyama.

5. Baadaye, ujue utaibeba vipi toka maabara mpaka kwa kiumbe/viambata na usiharibu ubora wa dawa husika au kuibadili.

Mfano: katika molecules 200 za ugunduzi kwa chanji ya corona ni saba tu zilipewa kibali, kutoka level moja ya utafiti kwenda nyingine.

Hii ni kuhakikisha kunachozalisha kuna ushahidi wa kutosha juu ya kutendakazi na usalama. Pata maarifa kwenye kitu kinaitwa drug discovery and development process.
 
Hao wataalamu wa afya niwafahamu vizuri tu karibu wote. Uwezo wao naufahamu na kazi zao nazijua.

Najua sio rahisi kuamini, lakini ukweli ni kuwa Hawajui lolote kuhusu kirusi cha Covid 19 na chanjo zake. Ebola tu yenyewe hawajui lolote wala maabara ya kuchunguza bacteria wake!

Wao wamekuwa tu wapiga debe kutafuta tu umaarufu waonekane wanjua na kuongeza wateja katika biasha zao za afya.

Hawana maabara, hawawezi hata kusoma na kuelewa machapisho kuhusu kirusi hicho katika journal kama Nature, Science, NEJM nk. Hata hawajawahi kushiriki wala kujadili na wanasayansi waliotengeneza hizo chanjo. Hawezi hata kuhudhuria mikutano yao ya kiasanyansi kwa sababu hawana cha kuchangia.

Wataalamu hao wanagoogle tu vijitaarifa na kujiita "mabingwa". Endeleeni kudanganywa. Uzuri tu wananchi walio wengi WAHADANGANYIKI! na vijitaarifa vya "mabingwa" uchwara wasio hata na maabara ya ebola sembuse kirusi cha corona.
 
Nini maana ya chanjo? Njanjo ya ini ambayo hadi sasa binaadam inatubidi tuchanje,je ukichanjwa chanjo ya ini ukikutana na vinavyosababisha homa ya maini utaugua?

Ndiyo.

Kuugua ni nini?
Ni yale mapokeo ya mwili wako kwa kitu kigeni mwilini/ugonjwa. Katika hali ya kawaida hata homa ya ini yenyewe dalili zake ni mild/ndogo sana, kama kupata mafua(flue like).

Ndio maana watu wengi hatujui tunapoambukizwa. Ila madhira yake ndo huwa makubwa/complications.

Hivyo, chanjo itakuzuia kwenda kwenye complications kama ini kuathirika na mengine. Lakini kujisikia hauko sawa kama dalili ndogo ndogo utapata (unwellness).
 
Hao wataalamu wa afya niwafahamu vizuri tu karibu wote. Uwezo wao naufahamu na kazi zao nazijua.

Najua sio rahisi kuamini, lakini ukweli ni kuwa Hawajui lolote kuhusu kirusi cha Covid 19 na chanjo zake. Ebola tu yenyewe hawajui lolote wala maabara ya kuchunguza bacteria wake!

Wao wamekuwa tu wapiga debe kutafuta tu umaarufu waonekane wanjua na kuongeza wateja katika biasha zao za afya.

Hawana maabara, hawawezi hata kusoma na kuelewa machapisho kuhusu kirusi hicho katika journal kama Nature, Science, NEJM nk. Hata hawajawahi kushiriki wala kujadili na wanasayansi waliotengeneza hizo chanjo. Hawezi hata kuhudhuria mikutano yao ya kiasanyansi kwa sababu hawana cha kuchangia.

Wataalamu hao wanagoogle tu vijitaarifa na kujiita "mabingwa". Endeleeni kudanganywa. Uzuri tu wananchi walio wengi WAHADANGANYIKI! na vijitaarifa vya "mabingwa" uchwara wasio hata na maabara ya ebola sembuse kirusi cha corona.

Nadhani ni vyema wewe kutumia ujuzi unaowazidi ili kuongeza uwezo katika hili kuliko kuonyesha tu kuwa uwezo wao ni mdogo.

Unatumia uwezo wako kuwafanya walio na kidogo wasifanye kwasababu wewe unajua zaidi?

Nadhani haya ni matumizi mabaya ya ulichonacho. Hadithi ya kaa ndani ya ndoo. Unamdondosha mwenzako wakati ameshapanda juu na anakaribia kutoka kwenye ndoo.

Tujifunze kuthamini michango ya wenzetu japo yawezakuwa ni kidogo na kuongeza thamani pale ambapo hawajafika.

Twajenga nyumba moja, twagombea fito za nini?
Leta ulichonacho tujenge nchi hapo maarifa yako yatakuwa na manufaa.
 
Ndiyo.

Kuugua ni nini?
Ni yale mapokeo ya mwili wako kwa kitu kigeni mwilini/ugonjwa. Katika hali ya kawaida hata homa ya ini yenyewe dalili zake ni mild/ndogo sana, kama kupata mafua(flue like).

Ndio maana watu wengi hatujui tunapoambukizwa. Ila madhira yake ndo huwa makubwa/complications.

Hivyo, chanjo itakuzuia kwenda kwenye complications kama ini kuathirika na mengine. Lakini kujisikia hauko sawa kama dalili ndogo ndogo utapata (unwellness).
Hakuna chanjo ambayo ukichanjwa haupati tena hiyo homa?
 
Kuna aliyesema waandishi wa habari kuwafata na kuwahoji wanaohubiri kupinga chanjo.Tatizo lipo kwa hao waandishi kwani hawana uelewa wa kutosha juu ya chanjo ama covid yenyewe. Mfano rahisi ni hoja za Gwajiboy ambazo zote zinajibika kirahisi na mtu hata asiye mtaalamu wa mambo ya afya, lakini sikuona andiko kwenye gazeti lolote linalotoa majibu ya zile hoja na kufanya watu waendelee kuamini habari zisizo za kweli kutoka kwa gwajiboy.
Kwahiyo nafikiri wataalamu wa afya wanaweza wakaanza na kuwaelimisha waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vyote vya habari kwani kwa kutumia hawa tutaweza kuifikisha ELIMU YA KWELI juu ya covid na chanjo yake kwa wananchi walio wengi.
ELIMU YA KWELI ITOLEWE ILI MWANANCHI AAMUE KWA USAHIHI.
kwa sasa kuna mkumbo tu kwa wengi wa kuchanja au kutochanja.
 
Hii ni kuhakikisha kunachozalisha kuna ushahidi wa kutosha juu ya kutendakazi na usalama. Pata maarifa kwenye kitu kinaitwa drug discovery and development process
Asante sana Mkuu kwa ufafanuzi mzuri sana.
Bandiko lako hili litanisaidia sana kupata maswali ya kutafuta ufahamu juu masuala haya kutoka kwa kada za kibiashara, kitabibu na kubwa kuliko zote kada ya kisiasa. Yaani naiona furusa kubwa sana kwenye kada ya kisiasa kwa sababu nitapata maswali mengi nitakayo yapenyeza kwa wajumbe kama karata ama kete zao wakati muafaka utakapofika kuzitumia.

Ha ha ha haaa! Kada ya wanasiasa naona inatoa macho.....!!!! Wanasiasa itendeeni haki kada yenu kwa kuonyesha uwezo wenu wa kusaidia kada nyingine zitatue changamoto ya magonjwa haya kwa kutumia rasilimali tulizonazo. Wale walasiyo wajomba wala washangazi wetu wadamu (Wwwwwww)!
 
Ni chanjo gani hapo nyuma walipewa wanadamu kwa ajili ya kujikinga na homa flani kisha wakachanjwa badae waliambukizwa nao wanaathirika? Kwa mfano chanjo ya polio, chanjo ya uti wa mgogo. Chanjo ya ini
Yellow fever
 
Mbali nakuangalia waliochanja na ambao hawajachanja ukizingatia Uviko-19 umeonekana ni gonjwa ambalo utakuwepo muda. Mpango gani uliopo wa wataalamu wetu wa Afya kuja na chanjo zetu kama Taifa ? Maana mataifa mengine tunaona wanakuja na chanjo zao. Tusisahau pia Taifa lipo katikati ilihali ni lazima ikitokea unataka kutoka nje ya nchi.
Nafikiri tatizo kwa nchi nyingi ni budget. Unafikiria kuwekeza fedha nyingi ambazo pengine utaweza zirudisha kwa kuuza hizo chanjo lakini sasa utamuuzia nani? Unapima gharama unaona za kuagiza ni cheap zaidi kuliko kutengeneza mwenyewe.

Ndiyo maana unaona hata mataifa tajiri kuliko Tanzania ( Japan, Brazil, Misri, Algeria, Korea ,Qatar nk) wanaendelea kuagiza.
 
Wote mna mlengo mmoja , mnajiuliza maswali wenyewe mnajijibu wenyewe.
Mmezungumzia kuhusu ku-expire kwa chanjo ila hamjasema zina-expire lini. Ni kwamba hamjui au basi tu
 
Back
Top Bottom