Yaliyojiri Ikulu Dar: Rais Magufuli amtaka CAG Kichere kutojifanya Muhimili mwingine, amwambia anaweza kuondolewa hata akiwa na mwaka mmoja

Maoni ya Profesa

1572854657792.png
 
Spika wa Bunge Mh Job Ndugai amempongeza CAG mpya Charles Kichere kwa uteuzi alioupata na kumuahidi ushirikiano uliotukuka.

Ndugai amesema watamtegemea sana Kichere katika kupata ukweli wa namna serikali inavyotumia kwa mujibu wa sheria fedha zilizopitishwa bungeni.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kila la heri Kicheree, Ila hawa kina Ndugai si wa kuwaamini sana, la msingi piga kazi kwa mujibu wa Katiba.
 
Spika wa bunge mh Job Ndugai amempongeza CAG mpya Charles Kichere kwa uteuzi alioupata na kumuahidi ushirikiano uliotukuka.

Ndugai amesema watamtegemea sana Kichere katika kupata ukweli wa namna serikali inavyotumia kwa mujibu wa sheria fedha zilizopitishwa bungeni.

Maendeleo hayana vyama!
Safi sana.
Nasubiri mhimili wa judiciary nao umpongeze dr.
 
Magufuli kamuapisha jaji mmoja, ambaye ni Mchagga na alikuwa fair competition. Anasema jamaa alivyo muadilifu hadi alipokuwa fair competition watu walikuwa wanajiuliza "Huyu ni Mchagga gani asiyependa rushwa?"

Alisema Makonda, kuwa Mengi alikuwa ni Mchagga wa pekee, Mchaga gani anaesaidia yatima, na leo baba naye amewakilisha mawazo ya wengi, walio kuwa kumbe watu wengi hushangaa wakiona Mchagga haibi, hapokei rushwa, na anasaidia watu.

Swali, Wachagga mlifikaje hapa, kwenye jamii kuwaona namna hii?
 
Anamuapisha CAG mteule, anasema maneno ya msingi sana.

1. Usiende kujifanya na wewe ni Muhimili, Mihilimi ni mitatu tu. (ASSAD alijiona muhimili eeh)

2. Una nidhamu sana, unatenguliwa hapa, na pale, lakini haulalamiki

3. Una elimu nzuri na uzoefu wa kazi.
 
Back
Top Bottom