Yaliyojiri Dodoma: Shughuli ya Kitaifa ya kumuaga Hayati John Magufuli

Mradi wa Magufuli wa Stiegler's Gorge utazalisha MGW 2115 za umeme wa kutosha Nchi nzimà na ziada kuwauzia Nchi jirani ndo maana katika kumuaga Shujaa wa dunia, ni viongozi wa nchi jirani tu ndo wamekuja. Msife mtoto mafanikio ya Marehemu ndo hayo!
Shujaa wa dunia,viongozi wa nchi jirani ndo waliokuja.Sijaelewa.Ina maana nchi za jirani ndiyo dunia au vipi.
 
H
Lazima marehemu azunguushwe ili kuwakomoa Chadema ambao walikuwa wanasema hapendwi.
Hivi kwanini unapenda sana kuwataja taja hawa jamaa huoni unawapandisha juu.Kwa akili yako ndogo unaona unawakomoa.Sijui unawakomoaje labda.Ni kwamba unawanyima wote chakula au inakuwaje labda sijaelewa.

Sikatai alikuwa anapendwa,au pia inawezekana ikawa kinyume chake.Wakajitokeza kuhakikisha kama ni kweli.Ndivyo inavyokwendaga kila mahali.
 
Kw
Kwenye msiba virungu vya nini bana??? Mbona Nyerere haikuwa hivyo???

Polisi, jWTZ, Jkt, Magereza walikuwa na vyupa vya chai za maziwa dada. Kila ukikauka mdomo!! Kikombe hichoooo!

Soda hizooo, bwerere, Msasani ndo usiseme gari za pepsi zinaingia na kutoka!! Kwaya za wasabato live Magomeni dada!! Rc kwaya live nk, weee!! Mbona utanyamaza kulia!!

Orange squash!! Kila kona!!

Maji baridi. Uhai kilimanjaro.wee! usiombe hiyo ni mpaka msasani. Gari za maji zinatusindikiza tu bongo land yetu.

Ambulance za kutosha mita kumi kumi! Hata hkn aliye kufa.

Helikopta za polisi!! juu kwa juu mama wee!!niseme nini! Mie!! Inaangalia nani kazimia nani kafa. Sasa huyu si kanunua saba ziko wapi??Nyie wana sirikali Mna lenu jambo Mwataka piga dili humo eee??

Kamvua kadooogo!! kananyesha na hii mvua tangu kufa. Dsm mpaka mwitongo!
Yaani kufika tuu Musoma air port sie wa Dsm ndo tulipewa pole nyingi na huruma na watu wa Musoma wakawa wanatuomba huku wanalia tupumzike!

Wakatulilia sisi sasa kwa upendo ule wa ajabu!

Hapo sasa Tukaanza tena moja wote kulia tukisema "mtuacheni jamani"heeee!!! Uchungu baba wa Taifa amekwenda!!
Saana!! huyu ananikumbusha Baba wa Taifa tuu alivonitoka tu!!!
Kwa hiyo sisi tukiomboleza nyinyi mlikuwa mnasherehekea na serikali ilikataza kusherehekea.Mkaachwa tu, nimeamini sasa kuna double standard.Hawa wakifanya sawa, hawa wengine nao wakifanya kitu hichohicho kamata.Haya bana
 
Mkuu sio kila anaeudhuria msibani anakuja kuomboleza. Wengine unakuta wameenda kuangalia wahudhuriaj, wengine unakuta wanakatiza tu kuelekea kwenye mishe zao, wengine ni waombolezaji kweli, wengine wanaenda kuhakikisha kweli, kila mtu ana lake. Wengine leo sio ajabu wameenda kwa ajili ya kuona maraisi wanaotoka nje ya nchi, wengine si ajabu wameend ili tu kumuona Samia

Wanaotaka mwili uzungushwe nchini kwanza wanaikosea sana Familia. Pili wanafanya Taifa lionekane la Kilimbukeni. Na mengine mengi. Kama mtu ni mnyonge sijui mlalahoi atajua yeye anapambana vip
Si hawa jamaa zangu,wenzangu wanasema azungushwe ili kuwakomoa wanasema CHADEMA.Ili tufurahi na kuwakomoa kisawasawa akitoka tu Zanzibar apelekwe Kaskazini Kilimanjaro,Arusha,Manyara, nadhani hizi alikuwa hajafanya ziara za kutosha.Halafu Tanga,Tuende tena hapo sijui panaitwa Msaga au Msata Bagamoyo.Tutakuwa tumewakomoa mpaka mwisho kama msiba huu ni wa kukomoana.Fikiria kabla hujaandika
 
Nimefurahi leo kuona mabalozi na viongozi wa nje wamekuja kuaga ila Raisi Samia hadi sasa niliowaona wakiaga uwanja Wa Taifa ni Mabohora lakini wahindi sikuwaona na waatabu haeakujitokeza kuna wachache waliojitokeza ni wa Taasisisi inaitwa ISQama kama sikodei spelling .Big up.kwa mabohora.Kwa wahindi kajitokeza kiongozi wao wa dini tu lakini wao hawakutokea DAR wala uwanja wa jamhuri Dodoma wamemtelekezea kiongozi wao wa dini ya kihindu!!! Mabohora shukrani mlijitokeza kwa wingi kuaga Dar

Pelekeni shukrani zetu watanzania kwa kiongizi wenu mkuu duniani
Mabalozi wa nje wametokea nchi gani na ni kina nani,mbona sikuona Mc Akiwakaribisha kuaga mwili.
 
Mzungumzaji: I am glad to be in Tanzania. Magufuli was my best friend and I am very sorry for his loss.

Mkalimani: Mwambie mama aniwekee ugali utumbo. Jumapili ijayo ni pasaka na dagaa wameisha jikoni.
 
Uwanjani pale nanuonea huruma mama Janet amejawa simanji Mungu amtie nguvu,

Ila nawaonea huruma zaidi wale waliofiwa na ndugu zao waliouliwa kikatili, mke wa Ben Sanane, mama wa Azwori Gwanda, ndugu wa wale waliookotwa ufukweni kwenye viroba. Hawa nawaonea huruma zaidi.

Hawa walionewa ila Magufuli kachukuliwa na mungu hajaonewa, mke wa Magufuli ataishi vizuri mahela yako hapo mahekalu aliojengewa Chato nk ila wafiwa wa akina Ben Sananene na wengine walidhulumiwa uhai wao na wajane wamebaki katika unasikini baada ya waliowatengemea kudhulumiwa uhai wao. Narudia hawa nawaonea huruma zaidi.
Mkuu imeniuma sana. Mimi ningekuwa kiongozi katika adhabu kubwa kwangu ni Vifungo vya maisha kwa wenye makosa kubwa ama kinyume changu. Nisingekubali vifo vya style hii.inaskitisha sana...
 
Nimeskia kauli "Iliyokuwa sehemu ya mkoa wa Mwanza" lakini sikufanikiwa kufahamu ni nani ameeleza.

Hayati Magufuli alizaliwa sehemu iliyokuwa mkoa wa Kagera sio Mwanza kama aliyezungumza. Huo ni upotoshaji, hata wakati wa kampeni za kisiasa na wakati wa kuapishwa clearly ilisemwa ni iliyokuwa sehemu ya Kagera.

I wanted to correct this! Jiografia na Uraia nayo yafanywe masomo ya lazima.

Out again
Kumbuka kagera ilikua mkoa wa ziwa magaribi na huu ulikua party ya mkoa wa Mwanza.kabla ya kugawanywa.before 70z
 
Kw

Kwa hiyo sisi tukiomboleza nyinyi mlikuwa mnasherehekea na serikali ilikataza kusherehekea.Mkaachwa tu, nimeamini sasa kuna double standard.Hawa wakifanya sawa, hawa wengine nao wakifanya kitu hichohicho kamata.Haya bana
Hawa wame muuua wao!! Ndiyo maana katazakataza nyingi.
Kwani unadhani walimpenda basi???

Angeenda mtoto wake hosp. asingekubali waliyomfanyia mzee rais.ila waliwekwa pembeni.

Jiwe Alikuwa anacheza na hatari Kubwa bila kujua richa ya kumuonya mara kibao. Sikio la kufa.....
 
Kumbuka kagera ilikua mkoa wa ziwa magaribi na huu ulikua party ya mkoa wa Mwanza.kabla ya kugawanywa.before 70z
Nope! Bro, Ziwa Magharibi ulikuwa mkoa uliojitenga same Mwanza, Shinyanga, Mara na Kigoma.

Baada ya vita vya Tanzania na Uganda vilivyofanywa pakubwa katika eneo la mto Kagera ndani ya Mkoa wa Ziwa Magharibi (Western Lake Region) ndio Tanzania ilibadili jina la mkoa kutoka Ziwa Magharibi na kuwa Kagera likiwa inspired na mto Kagera it was like 78 au 79.
 
Kw

Kwa hiyo sisi tukiomboleza nyinyi mlikuwa mnasherehekea na serikali ilikataza kusherehekea.Mkaachwa tu, nimeamini sasa kuna double standard.Hawa wakifanya sawa, hawa wengine nao wakifanya kitu hichohicho kamata.Haya bana
sisi ndiyo sisi hkn mwingine funguka
Baba yetu jk nyerere alipo kufa watu wenyewe wali ji organise!
 
Tayari msafara umeshajipanga kuondoka Ikulu Chamwino kuelekea bungeni kuagwa kisha utapelekwa uwanja wa Jamhuri

=========

DODOMA: WABUNGE WATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA DKT. MAGUFULI

Spika wa Bunge Job Ndugai akiwaongoza Wabunge na Viongozi wengine mbalimbali kwenye shughuli za kuuaga mwili wa Hayati Magufuli

Wabunge wa Bunge la Tanzania wametoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano aliyefariki dunia Machi 17, 2021

Wabunge wameuaga mwili wa Dkt. Magufuli katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma na baada ya zoezi hilo kukamilika, mwili huo utapelekwa Uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya shughuli ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho ambao itahudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kimataifa

NAIBU SPIKA: WENGI WAMEONA MEMA YA DKT. MAGUFULI. WATU WENGINE KUTOONA WEMA NI KAWAIDA

Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania umewasili Viwanja vya Bunge Dodoma kisha atapelekwa Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli ya kumuaga Kitaifa

Akizungumza katika Viwanja vya Bunge, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson ameeleza walio wengi wameona mema aliyofanya Dkt. Magufuli, akisema watu wengine kutoona wema ni jambo la kawaida

RATIBA YA KUMUAGA DKT. MAGUFULI DODOMA YABADILISHWA

Kutokana na wingi wa watu waliojitokeza Uwanja wa Jamhuri kumuaga Hayati Dkt. John Magufuli, ratiba imebadilishwa ambapo imeelezwa mwili utaagwa na watu wachache uwanjani

Imeelezwa mabadiliko hayo yamefanyika ili kutoa nafasi kwa wananchi kuaga kwenye mitaa ili watu wote waweze kutoa heshima zao za mwisho

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Binilith Mahenge amesema baada ya watu wachache kuaga, mwili wa Dkt. Magufuli utatolewa Uwanjani na kupitishwa round about ya Jamhuri na kisha katika Barabara ya Iringa na kisha ya Polisi

Ametaja Barabara nyingine ambazo mwili utapita kuwa ni Jamatini, Bunge, Morena, Emaus kuzungushia Barabara ya Waziri Mkuu hadi African Dreams na kutokea Barabara ya Arusha hadi Uwanja wa Ndege.

WAZIRI MKUU: NAMNA NZURI YA KUMUENZI DKT. MAGUFULI NI KUUISHI UTUMISHI WAKE

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema namna nzuri ya kumuenzi Hayati Dkt. John Magufuli ni kwa Watu kuuishi utumishi wake uliojaa ujasiri, maono na mapenzi makubwa kwa Nchi

Akizungumza katika Uwanja wa Jamhuri amesema, "Wengi tulitamani aendelee kuwa nasi kimwili, hata hivyo kifo ni suala lisiloepukika"

Ameungana na kauli iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Watanzania kuendelea kushirikiana na kuzidisha umoja na mshikamano.

-

Umoja wa Afrika: Magufuli alikuwa mkombozi wa Afrika katika Utawala na Uchumi.​

Rais wa DR Congo ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa nchi za Afrika ameyasema haya alipokuwa akitoa salamu za rambirambi leo Dodoma.

Ameongeza pia Hayati Magufuli aliifanya Afrika iheshimike tena na pia ametimiza ndoto za waasisi wa nchi barani Afrika.

RAIS KENYATTA: DKT. MAGUFULI AMEONESHA WAAFRIKA TUNA UWEZO WA KUSIMAMIA UCHUMI WETU

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema katika miaka michache, Dkt. John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania ameonesha kuwa Waafrika wana uwezo wa kujitoa katika utegemezi wa watu na vitu vya nje

Amesema, "Kwa muda mfupi tumeona kazi ya barabara, ujenzi wa Uwanja wa Ndege na mambo mengine mengi ambayo yatakuwa na manufaa kwa Watanzania na wana Afrika Mashariki"

Rais Kenyatta amemuelezea Hayati Dkt. Magufuli kama Rafiki wa karibu ambaye walikuwa wanaongea mara kwa mara. Amesema kifo chake ni pigo kwasababu alikuwa mtu wa heshima

Ameongeza, "Nawahakikishia tutaendelea kufanya kazi pamoja, tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunaleta pamoja Jumuiya ya Afrika Mashariki"

RAIS RAMAPHOSA WA AFRIKA KUSINI AMSHUKURU DKT. MAGUFULI KWA MAMBO MATATU

Katika hotuba yake Uwanja wa Jamhuri Dodoma, Rais Cyril Ramaphosa amesema Hayati Dkt. Magufuli alisimama kama shujaa dhidi ya Rushwa na ubadhirifu, akimuelezea kama Kiongozi aliyepinga vitendo hivyo akiamini Viongozi wanapaswa kutumikia wananchi wao

Amemshukuru Dkt. Magufuli kwa kuelekeza nguvu katika maendeleo ya Kiuchumi wa Taifa la Tanzania, Ukanda na Bara la Afrika kwa ujumla

Vilevile, Rais Ramaphosa amemshukuru Hayati Dkt. Magufuli kwa kuwa Mwana wa Afrika aliyeona umuhimu wa tamaduni kukumbukwa na kufundishwa, akisema alikuwa Kiongozi aliyetaka watu kujivunia Lugha za Kiafrika

Amesema Tanzania ilipata bahati kuwa na Kiongozi kama Hayati Dkt. John Magufuli

RAIS SAMIA: MATOKEO NDIO JIBU PEKEE ALILOPENDA KUSIKIA DKT. MAGUFULI. SIO VISINGIZIO NA LAWAMA

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Hayati Rais Magufuli alipenda kusikia matokeo kutoka kwao na wala sio visingizio na lawama

Amesema, "Alitukumbusha kuwa amejitolea maisha yake kuwa sadaka kwa Watanzania hivyo hakuwa na budi kufanya kazi usiku na mchana kuwaletea Maendeleo. Sote tulihofia sana iwapo alipata muda wa kutosha wa kupumzika"

Amesema katika Uongozi wa Dkt. Magufuli, wamejifunza mengi akisisitiza "Tupo vizuri, tumeiva sawasawa"

MWILI WA DKT. MAGUFULI WAZUNGUSHWA MARA TANO UWANJA WA JAMHURI

Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli umezungushwa mara katika Uwanja wa Jamhuri ili kutoa fursa kwa wananchi kutoa heshima zao za mwisho

Hilo limefanyika baada ya Viongozi, Wakuu wa Nchi mbalimbali pamoja na Familia ya Dkt. John Magufuli kutoa heshima zao za mwisho katika Uwanja huo ambapo shughuli ya Kitaifa imefanyika

Baada ya kuzungushwa katika uwanja huo, mwili wa Dkt. Magufuli utazungushwa kupita maeneo kadhaa ili wakazi wa Dodoma waweze kumuaga Kiongozi huyo


Waulize wanyarwanda na waganda
 
Back
Top Bottom