Yaliyojiri Dodoma: Maadhimisho ya Sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 2017

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Sherehe za maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinafanyika leo April 26, 2017 mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.

Tanganyika na Zanzibar ziliungana April 26, 1964 chini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalim Julius Nyerere na hayati Sheikh Abeid Karume.


1. Ni siku ambayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana.

2. Ni siku ambayo Tanzania ilizaliwa.

3. Siku ambayo maadhimisho haya yanafanyikia makao makuu ya nchi Dodoma kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.

Mgeni rasmi ni rais wa Tanzania na amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Tanzania.

Fuatilia uzi huu kwa live updates.

Rais MAgufuli anaingia Uwanjani

Wananchi wote wanaimba wimbo wa taifa wakiongozwa na rais Magufuli. Huu ni uzalendo mkubwa sana kwa nchi yetu upendo na mshikamano daima.Amiri jeshi mkuu anakagua gwaride.

Gwaride linaendelea kufanya vitu vyake sasa. Linalita kwa mwendo wa haraka mbele ya rais na mbele ya wananchi wote.

Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni;
Miaka 53 ya Muungano; Tuulinde na Kuuimarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,”

======

Rais Magufuli: Siku ya leo ni siku ya pekee, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutufikisha hapa”

Rais Magufuli: “Siku ya leo ndiyo birthday ya Tanzania”

Rais Magufuli: ”Baadhi ya mambo yaliyowezesha kuanzishwa umoja wetu ni undugu hata kabla ya kuja wakoloni walikuwa wakishirikiana ikiwepo biashara”

Rais Magufuli: ”Ushirikiano mzuri uliokuwepo kwa vyama vetu vya ukombozi, viongozi na wanachama wa vyama hivi viwili walikuwa wakishirikiana”

Rais Magufuli: “Muungano wetu umewezesha kuwepo na uhuru, amani na umoja wetu”

Rais Magufuli: “Tumejenga miradi mbalimbali ya huduma za jamii, Tanzania ya sasa sio ile ya 1964”

Rais Magufuli: “Wahenga walisema usione vyaelea vimeundwa, wapo watu wamewezesha mafanikio haya kupatikana”

Rais Magufuli: “Swala la kulinda Muungano sio jambo rahisi hivyo hatuna budi kuwapongeza waliowezesha kuwepo kwa Muungano wetu”

Rais Magufuli: “Bahati nzuri leo hapa tunae Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, tunawashukuru sana”

Rais Magufuli: "Napenda kuwaahidi mimi na Dk. Shein tutafata nyayo zenu za kudumisha Muungano"

Rais Magufuli: "Tukiwa tunaadhimisha miaka 53 ya Muungano tutafakari tulipotoka, tulipo sasa na tunapoenda, wengi wetu wamezaliwa baada ya mwaka 1964"

Rais Magufuli: "Kwa pamoja tunaweza, tukishikamana kwa pamoja tunaweza, na ninahakika kwa nguvu za Mwenyezi Mungu tutaendelea kusherehekea Muungano"

Rais Magufuli: "Pamoja na mafanikio lakini pia kuna changamoto, kuna kamati ya kushughulikia mambo ya Muungano ikiongozwa na Makamu wa Rais"

Rais Magufuli: "Kila Mtanzania anatakiwa kulinda Muungano wetu na njia bora ni kuchapa kazi"

Rais Magufuli: "Kwa mara ya kwanza tumefanyia Dodoma na hii ni nia ya dhati ya serikali ya kuwa makao makuu yawe Dodoma na niwahakikishie sasa tupo Dodoma"

Rais Magufuli: "Serikali imetenga Bilioni 200 ya kujenga ofisi na majengo, tuna miradi mingi ya maendeleo kwa ajili ya Dodoma"

Rais Magufuli: "Kwa kumaliza natoa shukrani kwa kamati ya maandalizi watu ni wengi ndani na nje wamejaa hii kweli inaonyesha Ddm ni makao makuu ya nchi"

Rais Magufuli: "Napenda kupongeza ngoma, na hasa hawa watani zangu wanavyozungusha shingo, wanazungusha kweli shingo"

Rais Magufuli: "Tunaadhimisha miaka 53 tukitambua watangulizi kweli waliulinda Muungano wetu"

Rais Magufuli: "Kikwete siku hizi anaonekana kijana kuliko mimi, anapendeza"

Rais Magufuli: "Muungano ndiyo jembe letu, na kamwe asijitokeze mtu atakaye jaribu kuvunja Muungano wetu akija akitokea atavunjika yeye"

Rais Magufuli: "Niwatakie sikukuu njema, Mungu ibariki Tanzania, asanteni sana"

======

1bbbc.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kitaifa katika uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma April 26,2017


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.

''Muungano ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda Muungano kwa nguvu zote. Yeyote atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.

Aidha Dkt. Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.

Rais Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda taifa moja lenye nguvu.

Aidha amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Mhe. Rais ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli na nchi kavu.

Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.

Kwa mara ya kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.

''Niwahahakikishie wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.

Sherehe za miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dodoma

26 Aprili, 2017
 
Nderemo na vifijo kwa wananchi hapa uwanjani wakisherehekea na kuburudika kwa ngoma mbalimbali na vikundi vya utamaduni vya asili na mziki wa kizazi kipya.
 
Viongozi mbalimbali wameshahudhuria wakiwamo wabunge mawaziri na viongozi wengine wa kitaifa, mabalozi, diplomats,wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya nk
 
Kikubwa cha kujiuliza ni umri wa hawa wazee wakat wanatekeleza hili (Tunaungana) na kipi sisi Tutakuwa tume au tumeisha accomplish kwa ajili Ya kizaz kijacho at that age.....Whether they were wrong or right utaona they hard a purpose of which today as a country we dont
 
Back
Top Bottom