Yaliyojiri Clubhouse session ya JamiiForums Mei 26, 2022: Elimu kuhusu Saratani ya Jicho kwa Watoto

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,800
11,961
photo1653576370.jpeg

Nini chanzo cha Saratani ya Jicho kwa Watoto? Dalili zake ni zipi? Hali ya Ugonjwa huu ikoje hapa Tanzania?

Kufahamu haya na mengine zaidi, shiriki katika Mjadala na Wataalamu kuhusu Saratani ya Jicho kwa Watoto utakaofanyika Mei 26, 2022 kupitia Clubhouse, kuanzia Saa 12:00 Jioni

Kushiriki tembelea hapa: Fahamu kuhusu Saratani ya Macho kwa Watoto - JamiiForums

Mjadala umeanza

DKT. HEAVENLIGHT MASUKI, DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA MACHO

Saratani ya Jicho kwa Watoto hutokea kwenye pazia la Jicho ambalo husaidia kukusanya taarifa na kupeleka kwenye ubongo

Ili Saratani itokee, lazima kuwe na Mpangilio mbaya wa Seli. Unakuta zinazotakiwa kufa hazifi

Saratani hii mara nyingi inawaathiri watoto kutokana na ukuaji wa pazia la jicho. Mtoto anapozaliwa viungo mbalimbali vinakua

Pazia la mtoto anapozaliwa bado halijakomaa na huchukua hadi miaka minne. Katika wakati huu ndipo Saratani ya Jicho ndio huweza kutokea

Saratani ya Jicho kwa Watoto isipotibika mapema huwa ina tabia ya kusambaa

Saratani hii inaweza kwenda kwenye ubongo na sehemu nyingine za mwili isipotibiwa

- Dalili za Saratani ya Jicho kwa Watoto

Dalili ya kwanza kwa asilimia kubwa ni jicho la Mtoto linakua linawaka kama la paka. Mzazi akimuangalia usiku akaona kama jicho linawaka taa japo sio muda wote (hutokea sana usiku)

Ikipita miezi sita, jicho hili linaonekana kama la paka muda wote

Siyo kila kengeza kwa mtoto ni dalili ya Saratani ya Jicho, lakini mtoto chini ya miaka mitano akiwa na hali hiyo ni vema akachunguzwa.

Mzazi ambaye aliwahi kuwa na mtoto mwenye Saratani ya Jicho, akizaa mtoto mwingine huwa tunamshauri ampeleke mtoto hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo, tunasisitiza kufanya vipimo mapema kwa wazazi na watoto wenye historia ya saratani.

DKT. EVARISTA MGAYA, DAKTARI BINGWA MAGONJWA YA MACHO

Kitu ambacho huwa tunakitarajia kwenye matibabu ni kuokoa jicho liweze kuona, tukishindwa kuokoa jicho lione tunaliokoa jicho libaki, ikishindikana mwisho kabisa ni kuokoa maisha ya mtoto

Ukipima jicho la mtoto na kuona Saratani ya Jicho imesambaa zaidi kichwani, mfano ikifika karibu na ubongo, hiyo matibabu yake yanakuwa ni magumu sana, hapo tunampa dawa ili kusogeza maisha yake.

DKT. BERNADETHA SHILIO, MENEJA - MPANGO WA TAIFA WA HUDUMA ZA MACHO, WIZARA YA AFYA

Takwimu za Saratani ya Jicho kwa Tanzania kuna wagonjwa 20-100 kwa mwaka. Hii ni ngazi ya chini, kuna senta za juu tunapokea wagonjwa 90 kwa mwaka, hao ni wale ambao wamefika kwenye vituo vya tiba.

Wizara ya Afya imeona Saratani ya Jicho ni changamoto, wenzetu Nchi zilizoendelea wagonjwa wanafikishwa mapema hospitali na wanapata huduma, wachache sana wanafikia hatua ya kupoteza maisha

Tunashirikiana kwa ukaribu na Uingereza, wenzetu mtoto akishagundulika ana Saratani ya Jicho gharama zake zinakuwa zinasimamiwa na Nchi na wadhamini mbalimbali, hiyo inachangia ufuatiliaji tofauti na huku kwetu ambapo mzazi anakuwa anafuatilia mwenyewe

Dkt. Evarista: Kwa kadiri ya taratibu za Huduma za Afya, sio Hospitali zote zina Vitengo vya Macho, hivyo ukipata dalili hizo nenda kwenye Hospitali ya Macho iliyopo karibu nawe

Unaweza kwenda Hospitali ya Wilaya ambapo unaweza pewa rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kwa urahisi

Huduma ya kwanza ya Mzazi kwa Mtoto mwenye dalili za Saratani ya Kicho ni kutafuta nauli au msaada wa kuwahi hospitali mapema kwa ajili ya matibabu ya mapema na sio kununua dawa kwenye Maduka ya Dawa au vinginevyo

Dkt. Bernadetha: Mgonjwa hakatazwi kwenda kupata Tiba Mbadala lakini anaelezwa kuhusu umuhimu wa tiba ambayo atatakiwa kuipata hospitali

Zamani Wagonjwa wa Saratani ya Macho walikuwa wanakwenda katika Tiba Mbadala lakini hali ikishakuwa mbaya ndio wanarudi hospitalini

Mgonjwa hakatazwi kwenda kupata Tiba Mbadala lakini anaelezwa kuhusu umuhimu wa tiba ambayo atatakiwa kuipata hospitali

Zamani Wagonjwa wa Saratani ya Macho walikuwa wanakwenda katika Tiba Mbadala lakini hali ikishakuwa mbaya ndio wanarudi hospitalini

Katika Muongozo tulioutoa kuhusu Saratani hii, tumetoa maelekezo nini kifanyike kwenye Ngazi ya Jamii na Ngazi ya Zahanati

Kwa sasa tumeanza kutoa Huduma ya Elimu ya Afya ya Msingi ya Jicho kwa Mikoa ya Kilimanjaro, Singida na Morogoro

Saratani ya Jicho ni huduma ambayo inapatikana katika Bima za Afya

Changamoto ni kuwa kuna mahitaji mengine ambayo Mzazi anaweza kuhitajika kuingia mfukoni ili kufanya huduma katika vipimo vingine vya mgonjwa

Kanda ya Ziwa inaongoza kwa Wagonjwa wa Saratani ya Jicho, hii ni takwimu za awali

Takwimu za juu zinaonesha Mwanza na Dar es Salaam. Hii inaweza kuwa inatokana na wingi wa idadi ya watu

Dkt. Evarista: Wanaofanya katika kliniki za watoto Mwanza kuna mafunzo ya kuweza kutambua dalili mapema Wengine wanaweza kuchanganya Saratani na Mtoto wa Jicho, ndio maana unatakiwa kufika hospitali kufanyiwa vipimo mapema

Kwa Kanda ya Ziwa Watoto wengi wanapatiwa huduma Bugando. Idara ya Macho Hospitalini hapo ilipata ufadhili kutoka Marekani pamoja na KCMC

2016 kurudi nyuma Watoto wengi walikuwa wanachelewa kupatiwa matibabu kwa kuwa hawakujua ni wapi wangepata huduma

Mwanangu alikuwa anajicho moja kubwa lingine dogo ukimuangalia kwa umakini lile kubwa lilikuwa kama kengeza , na alifariki ghafla alipofika umri wa mwaka na miezi 9.
 
Mwanangu alikuwa anajicho moja kubwa lingine dogo ukimuangalia kwa umakini lile kubwa lilikuwa kama kengeza , na alifariki ghafla alipofika umri wa mwaka na miezi 9.
Pole sana ndugu, tatizo la jicho ndo lilikuwa chanzo cha kifo chake? Mlichukua hatua zozote za kimatibabu kabla hajafikwa na umauti?
 
Pole sana ndugu, tatizo la jicho ndo lilikuwa chanzo cha kifo chake? Mlichukua hatua zozote za kimatibabu kabla hajafikwa na umauti?
Hatukugundua chanzo cha kifo chake ata tulipoenda hospital na kupima vipimo vyote , kama malaria hakuwanayo ila alikuwa akianguka ghafla kama degedege na , anapumua kwa shida (kukoroma) iliwahi tokea mara mbili, mara ya kwanza alipona ila mara ya pili ndo akafariki , Na hali hyo ilikuwa ikimkuta asubuh, aliamka vizuri ila ghafla ilimkuta hyo hali.
 
Pole sana
 
Mwanangu alikuwa anajicho moja kubwa lingine dogo ukimuangalia kwa umakini lile kubwa lilikuwa kama kengeza , na alifariki ghafla alipofika umri wa mwaka na miezi 9.
Hatukugundua chanzo cha kifo chake ata tulipoenda hospital na kupima vipimo vyote , kama malaria hakuwanayo ila alikuwa akianguka ghafla kama degedege na , anapumua kwa shida (kukoroma) iliwahi tokea mara mbili, mara ya kwanza alipona ila mara ya pili ndo akafariki , Na hali hyo ilikuwa ikimkuta asubuh, aliamka vizuri ila ghafla ilimkuta hyo hali.

Poleni sana wewe na mzazi mwenzio...
 
Back
Top Bottom