Yaliyojiri Club na Erickb52

Erickb52

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
18,539
11,442
Kweli club kuna maajabu sana na vituko vingi!
Jana nilikuwa zangu counter na DJ alikuwa vizuri sana yan bandika bandua bila kuchange beat wala kuharibu step za wateja wake! Nilistaajabu mdada mmoja alipokuja counter na mkaka kuchukua kinywaji,kope zake zilikuwa ndefu kama nusu nchi hivi nkamwangalia kwa makini nikaona zimeongezewa urefu yan zimemfanya amekuwa katuni hasaaa ila yeye alijiona katokelezea mbaya na mashauzi kibaoooo!
Then kuna binti mmoja aliletwa kupata toti mbili za godons alipokosa glass akazitwanga kavukavu hapohapo counter....nilifeel maumivu yake kooni lol wadada mko juu siku hizi.
Baadae kidogo nilimuona mkaka kajibebea juice kubwa ya Azam kwapani na mkononi kabeba Castle Lager na yuko anazunguka kila kona na anazinywa zote...sikujua flavor alokuwa anapata.
Baadae wakaingia Mmama na kasharobaro kamoja wakiwa wanaonyeshana mahaba kweli kweli lol Walikuwa wakibusiana na kukumbatiana mara kwa mara bila aibu na kuvuta hisia za watu!Kwa umri walipishana zaidi ya miaka 20 (Watu noma)
Wanaume nao hawakuwa mbali kuleta raha ya macho lol kuna mkaka alikuwa anacheza kwa style ya binua kiuno kama mdada yan alikuwa anajiachia utadhani sio ridhiki ila nilihisi ni pombe zilimkolea tu(Pombe zisizidi jamani)
Kimavazi kuna waliokuja wamevaa magauni marefu(Hawa nilihisi walokole wanaouacha ulokole taratibu au mahausigel) na wapo walokuwa wamepiga vimin haswaa na kifua nje lol mitego tupu wengine kawaida!
Kuna wanaocheza kwa step hadi raha lol huchoki kuwaangalia hata kidogo!

Kilichokuja kuniudhi nikaondoka ni mdada alipokuja na kuanza kujisogeza sogeza nilipokaa na kunigusagusa nikimuangalia anasema samahani kaka mh kila mara lol nikaona hapa hapafai tena nikaamua kuepusha msongamano nikaenda zangu kulala!

Je ni haya ndio yanayotokeaga club ?? Mbona yanastaajabisha?
Anyway mi sio mzee Mtambuzi mzee wa story

I remain
Erickb52
 
Hapo kwenye nyusi nahisi utakuwa umechanganya na kope bana...maana hadi nimecheka. Nyusi nusu inch,si atakuwa na msitu balaa...kama vampire yaan!!
 
Hapo kwenye nyusi nahisi utakuwa umechanganya na kope bana...maana hadi nimecheka. Nyusi nusu inch,si atakuwa na msitu balaa...kama vampire yaan!!
Ni kweli HEARTnilimaanisha kope lol huwa nazichanganya sana lol
 
Last edited by a moderator:
tena unabahati ungejichanganya ungewajua vizuri wadada wamjini..
Heheheheee ndetichia yan nilikuwa sichezi mbali na walett yangu mana ilikuwa mfuko wa nyuma dah
Halafu hawana aibu eti mara acheze akinigongeshea wowowoo dah
 
Last edited by a moderator:
Umeanza kwa ukweli ukamalizia kwa uongo.

Anyway tudanganye japo kiduchu, ulitumia condom?
Hahahahaaa Asprin sikuondoka na mtu coz wale walikuwa balaa
Wametokelezea kinegative halafu wanagonga toti mbili kavu siuwataiua aisee
 
Last edited by a moderator:
Heheheheee ndetichia yan nilikuwa sichezi mbali na walett yangu mana ilikuwa mfuko wa nyuma dah
Halafu hawana aibu eti mara acheze akinigongeshea wowowoo dah

wako radhi wakunyonye hata unyayo ilimradi tu ulegee..
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom