Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Naamini sasa kwa kinachoedelea Bungeni kama mtu unajua kuchekecha mambo kamwe hautampuuza Roma Mkatoliki na kwamba ati "alijiteka".
Ulimboka katekwa kateswa katupwa Mabwepande mpaka leo hakuna uchunguzi wala majibu, Yeye mpaka leo hakusimulia nani kamfanyia hivyo.
Salma wa DW katekwa kateswa katupwa kati kati ya mji. Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.
George Mgoba katekwa kateswa katupwa Magwepande, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.
Kibanda katekwa kateswa katobolewa jicho, Yeye mpaka leo hakusimulia kinagaubaga nani kamfanyia hivyo. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.
Yalinikuta mimi, wengi mpaka leo wanasema nilijiteka...na maneno kibaaaao....
Ben Saanane maarufu Ben-Rabiu Wa Saanane katekwa mpaka leo mwezi wa 4 huu, Hakuna yeyote mpaka leo anayeweza kusimulia kinagaubaga au hata kulisemea tu nani kamfanyia hivyo kijana huyu hazina ya taifa. Wakasema amejiteka mpaka leo hakuna uchunguzi.
Roma na wenzake wametekwa wameteswa mnajipa moyo mnasubiri uchunguzi?
Ili wote tuamini kwamba Tanzania kuna utekaji na utesaji inabudi WOTE tuonje machungu haya ya kutekwa na kuteswa. Naamini wabunge hawa wasingeonjeshwe shubiri wasingefunguka hivi. Muda ukifika hatutaoishana hivi katika kuongea, WOTE tutaongea Lugha moja na hili limeanza huko Bungeni.
Nukuu za Wabunge leo ni jibu la haya mambo:
"Nipo tayari kuthibitisha kwamba waliovamia Clouds Tv ni Usalama wa Taifa kutoka kikosi cha Ulinzi wa Rais, Nipo tayari pia kuthibitisha aliyemtoloea bastola Nape ni Usalama wa Taifa"
Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo)
"Hivi Waziri wa Habari alikwenda kufanya nini katika Press ya Roma, mkiambiwa mlimteka mtakataa? Bora kusema ukweli kuliko kukaa kimya, najua mtasema kwa kuwa nilikosa uwaziri No!"
Juma Nkamia (CCM)
"Mimi nimekamatwa na kuteswa na Usalama wa Taifa. Nimenyanyaswa sana nchi hii. Ikibidi mnifukuze CCM (machozi)".
Hussein Bashe (CCM)
"Hakuna sababu ya Mwigulu kuendelea kukaa kimya wakati wananchi wanaishi kwa wasiwasi juu ya usalama wao. Kutoa kauli kunasaidia kutoa hofu"
Ridhiwani Kikwete (CCM)
"Mimi ni miongoni mwa wabunge niliotishwa na Mkuu wa mkoa wa Dar, na mpaka sasa mimi sikanyagi Dar licha ya kuimisi sana"
Hillary Aeshi (CCM)
Tafakari, Chukua hatua
Na Yericko Nyerere