Yaliyojiri Bungeni leo: Serikali yafafanua kuhusu watoto wengi wanaopimwa DNA konekana walizaliwa nje ya ndoa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Leo kikao cha tatu cha Bunge

Maswali na majibu yanaanza
bungeni.jpg

Inaanza Wiazara ya Tamisemi, Ofisi ya Rais

Swali: Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini anauliza kuhusu mvua zinazoendelea kuharibu barabara nyingi vijijini, serikali ina mpango gani wa kusisaidia TARURA?

Jibu: Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi anajibu, anaakiri mvu kuharibu maeneo mengi anasema serikali ina mpango wa kufanya utahamini kuhusu maeneo yaliyoathiriwa ili wachukue hatua

Swali: Mbunge wa Viti maalum, Agnes Marwa anauliza kuhusu ukosefu wa dawa katika hospitali ya Manyamanyama wilaya ya Bunda, ni lini serikali iytaongeza wauguzi na vifaa na kuipandisha hadhi?

Jibu:Naibu Waziri Tamisemi anasema kituo hicho hakijakidhi kuwa Hospitali baada ya kukaguliwa na wataalamu kutoka Wizara ya Afya kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya kutosha ikiwemo nyumba ya watumishi.

Swali: Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku, anuliza kuhusu kuwepo kwa mkanganyiko kati ya Wizara ya Afya na Wizara ya Tamisemi kuhusu kuipandisha hadhi kituo cha Afya Nzela kuwa Hospitali ya Wilaya lakini Tamisemi imekuwa bado haijaridhia, ni lini Waziri atakitembelea kituo hicho?

Jibu: Waziri wa Tamisemi, Suleiman Jaffo anajibu kuwa mara baada ya Bunge la Bajeti watakuwa na ziara maalumu kuzindua Hospitali za Wilaya hivyo mbunge asiwe na hofu

Inafuatia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


Swali: Swali la Zitto kabwe kuhoji Serikali imefikia hatua gani kwenye kuifanya bandari ya Kigoma kuwa bandari ya mwisho kwenye bidhaa za Burundi na Mashariki ya DRC, Serikali imefikia hatua gani kwa za kiforodha kwa bandari hiyo?

Naibu wazri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano, Atshasta Nditiye anajibu.

Jibu:Naibu Waziri anakiri kweli Serikali iliahidi kuifanya Bandari hii kuwa bandari ya mwisho Januari 2018

Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwezesha bandari za Ujiji na Kibirizi na zabuni kutangazwa, ila hakuna mzabuni hata mmoja aliyejitokeza kuomba

TPA imetangaza tena zabuni hizo mwezi Machi kimataifa na zimefunguliwa tarehe 3 Aprili na jumla ya wazabuni 21 wamejitokeza kufanya kazi hiyo na utathimini wa kumtafuta mjenzi unaendelea na itanyanyua utendaji kazi wa bandari ya Kigoma

Swali: Mbunge Mussa Mbaruku anauliza, anauliza bandari ya Tanga ina miundombinu duni sana na inafanya kazi chini ya kiwango serikali itatekeleza lini ahadi yake ya kuipanua na kuiimarisha?

Jibu: Naibu waziri wa Ujenzi anajibu, sasa hivi serikali imeshaanza matayarisho ya marekebisho ya bandari ya Tanga, serikali inaifanya bandari hiyo kuwa kubwa ili iweze kushusha vifaa kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta la Hoima

Inafuata Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto

Swali: Swali linauliza Rukia Kassim Ahmed mbunge wa viti Maalum anauliza serikali imejipangaje kutokomeza vitendo vya udhalilishaji kwa watoto?

Jibu: Naibu Waziri, Faustin Andungulile anajibu swali hilo

Serikali inahamasisha jamii kutoa taarifa na kulemisha kutoa taarifa za udhalilishaji wa watoto na inatoa adhabu kali kwa wanaokutwa na hati ya kosa hilo

Pia serikali imeanzisha kamati za ulinzi za wanawake na watoto kuanzisa ngazi za kijiji hadi taifa, lango ni kudhibiti matukio ya udhalilishaji katika maeneo husika

Pia kuna namba iliyotolewa ya kutoa taarifa juu ya udhalilishaji namba hio ni 116 na mtu anaweza kupiga namba hiyo kuripoti tukio lolote la udhalilishaji wa mtoto

Katika kipindi cha Januari hadi Disemaba matukio 1,072 yaliripotiwa kupitia namba hiyo

Sasa hivi adhabu kwa udhalilishaji wa mtoto ni milioni 5 au kifungo cha miezi 6 au zote kwa pamoja, ila serikali inatafakari kama kuna haja ya kuipandisha adhabu hiyo

Swali: Pauline Ghekul anauliza serikali ni kwa nini haijatekeleza mapaka sasa kujenga vyumba vya kujisitiri vya watoto wa kike kama ilivyoahidi na kusababisha watoto hao kudhalilika?

Jibu: Naibu Waziri anajibu, watoto wa kike wanahitaji sehemu ya kujisitiri wakiwa katika siku zao, na sasa wanaanza kulifanyia kazi kupitia Tamisemi na wizara ya elimu ya kujenga vyoo na vyumba maalum wa kujenga vyumba vya watoto kujisitiri

Swali: Silinde anauliza Swali, watoto kuolewa katika umri mdigo ni udhalilishaji, na serikali imeenda mahakamani kupinga watoto kuolewa zaidi ya umri wa miaka 18, je hii sio kuunga mkono udhalilishaji wa watoto?

Jibu: Naibu Spika anasema hilo swali halihusu wizara ya afya kwa kuwa sio iliyoenda mahakamani, yafaa aliulize kama swali kuu ili lijibiwe na wizara husika

Swali: Esther Matiko anauliza serikali imesema kuna madawati ya jinsia 117, hii inaonyesha hakuna madawati haya kwenye wilaya nyingine, anauliza pia ni kwa nini serikali isije na njia mbadala ya kuwapaelimu hao wanaofanya vitendo hivyo ili kukinnga matukio hayo kutokea?

Jibu: Waiziri Mwigulu Nchemba amesema serikali inafanya njia mbadala nyingi na na madawati ni zaidi ya 417 na kwenye vituo vya polisi mwameweka madawati ya jinsia pia

Pia serikali inaongeza juhudiza kutoa elimu na pia wanawahimiza viongozi wa kiroho kwenye nyumba za ibada maana mara nyingine matukio haya huambatana na imani za kishirikiana

Swali: Mbunge Chegeni aanauliza takwimu zinaonyesha kuwa kila watoto 6 wanaozaliwa, watoto wanne sio wa baba halali, serikali inatoa kauli gani juu ya udhalilishaji wa akina baba kwa kubambikiziwa watoto wasio wa kwao?

Jibu: Naibu waziri anajibu, si kweli kuwa kati ya watoto 6 wanaozaliwa, wannne sio wa baba halali, takwimu hizo zilikuwa zinatokana waliopeleka vipimo vyao kwa ajili ya vinasaba kutambua uhalali wa mzazi ambapo tayari kulikuwa na wasiwasi

 
Umerundika vitu viingi ambavyo haviendani na title. Bora ungesema, 'Yaliyojiri leo Bungeni', INGETOSHA na ungeeleweka zaidi.
 
Wabunge wawili wa chama cha wananchi CUF mmoja akiwa ni wa CUF maalim na mwingine CUF Lipumba wamezua gumzo ndani ya ukumbi wa bunge kwa kusutana huku kila mmoja akijiona ni mwamba.

Hali hiyo ilijitokeza wakati wa mchango wa mh RUKIA ambapo alimuomba msajili wa vyama vya siasa kuingilia kati mgogoro uliopo ndani ya CUF huku akikiri ukweli kuwa mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho umeathiri hata ushirikiano miongoni mwa wabunge wa CUF wenyewe kwa wenyewe.

My take: Poleni CUF. Nendeni chumbani mkayamalize.
 
Wabunge wawili wa chama cha wananchi CUF mmoja akiwa ni wa CUF maalim na mwingine CUF Lipumba wamezua gumzo ndani ya ukumbi wa bunge kwa kusutana huku kila mmoja akijiona ni mwamba.

Hali hiyo ilijitokeza wakati wa mchango wa mh RUKIA ambapo alimuomba msajili wa vyama vya siasa kuingilia kati mgogoro uliopo ndani ya CUF huku akikiri ukweli kuwa mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho umeathiri hata ushirikiano miongoni mwa wabunge wa CUF wenyewe kwa wenyewe.

My take: Poleni CUF. Nendeni chumbani mkayamalize.
Content ya habari bado haijaakisi kichwa cha habari. Hujaonesha pande hizo namna "zilivyoraruana" ziadi umeripoti kuwa mh RUKIA ameomba msajili aingilie kati mgogoro

Tujitahidi habari zetu kuzipa uzito sawa na kichwa cha habari zaidi itakuwa ni sawa na kusoma hbr za magezeti ya shigongo.
 
Magufuli katumia askari kumuingiza na kumlinda lipumba aliyejiudhuru mwenyewe kukalia kwa nguvu makao ya buguruni kila MTU anajua lipumba so Mwenyekiti halali
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba amepasua JIPU bungeni baada ya kueleza kuwa, Uzoefu unaonyesha pindi CHADEMA kikishiriki Uchaguzi, ndipo matukio ya uvunjifu wa Amani yanapojitokeza kwenye Chaguzi hizo.

Dk. Mwigulu alitoa mfano wa moja ya Chaguzi ambao Chadema iligomea kushiriki, ulifanyika kwa Amani na Utulivu.
Mjadala ambao uliwaibua wabunge wa CCM na kuwashambulia CHADEMA kwa mapungufu hayo.

Magazetini
IMG_3857.JPG
 
Sikufanikiwa kusoma lakini ukinipa PhD naikataa.

Kama kuna awamu itaaibisha tasnia ya taaluma ni hii. Imesheheni wasomi, wenye PhD kila idara, kuanzia juu kabisa. Ni kipimo kuona elimu yetu inavyoweza kutusaidia, lakini kwa hizi kauli, acha nisiongee sana.

Lakini wanashindwa hata kutuambia deni la taifa ni kiasi gani.
 
Huwa CDM wanashiriki peke yao kwenye huo uchaguzi?

Ni sawa na kusema mbwa yule ya pili husababisha chakula kumwagika kama atataka kula wakati mbwa wa kwanza anakula bila kufikiri kuwa ulafi na ubinafsi wa mbwa wa kwanza ndio chanzo
 
Uzeefu wa Mwingulu unaonyesha chadema wakishiriki uchaguzi uvunjifu wa taratibu na kanuni za uchaguzi unakuwa mkubwa

Unawatoaje mawakala wa chama nje wakati uchaguzi unaendelea?

Uzoefu unaonyesha chadema wakishiriki wnakuwa wanapmbana na tume ya uchaguzi, polisi wote hao wakiisaidia ccm

Mwigulu katafute watoto wa kuwadanganya
 
Sikufanikiwa kusoma lakini ukinipa PhD naikataa.

Kama kuna awamu itaaibisha tasnia ya taaluma ni hii. Imesheheni wasomi, wenye PhD kila idara, kuanzia juu kabisa. Ni kipimo kuona elimu yetu inavyoweza kutusaidia, lakini kwa hizi kauli, acha nisiongee sana.

Lakini wanashindwa hata kutuambia deni la taifa ni kiasi gani.
Kuna uzi mmoja nili comment hivi, "kwasasa sioni sababu yoyote ya watendaji wa serikali kua na elimu kubwa, ni matumizi mabaya ya rasilimali watu"
Mkuu, nakubaliana na wewe kabisa, sasa hivi msomi na asie soma huoni tofauti yoyote ya namna yao ya kufikiri.
 
Ulevi siyo lazima unywe pombe au uvute bangi. Kukihusisha chadema na vurugu ni aina mpya ya ulevi.
 
Swali: Mbunge Chegeni aanauliza takwimu zinaonyesha kuwa kila watoto 6 wanaozaliwa, watoto wanne sio wa baba halali, serikali inatoa kauli gani juu ya udhalilishaji wa akina baba kwa kubambikiziwa watoto wasio wa kwao?

Jibu: Naibu waziri anajibu, si kweli kuwa kati ya watoto 6 wanaozaliwa, wannne sio wa baba halali, takwimu hizo zilikuwa zinatokana waliopeleka vipimo vyao kwa ajili ya vinasaba kutambua uhalali wa mzazi ambapo tayari kulikuwa na wasiwasi


Mi nadhani Kupima DNA kuwengekewa urahisi tu kama ilivyo kupima homa, sio mpaka kuwe na kesi mahakamani sijui na Ustawi wa jamii
 
Back
Top Bottom