Yaliyojiri Bungeni leo: Februari 2010

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,180
Wanabodi,

Kama kawaida wananchi kama mimi, tupatapo nafasi huwa tunajituma mpaka mjengoni ili kuisikia live kwa naked eyes baadhi ya mijadala muhimu. Ndivyo ilivyokuwa kwa jioni ya leo, nimejihimu ili nisikie mjadala wa taarifa mbili za serikali ikirindima.

Saa 11:00 akaingia Naibu Spika, Mheshimiwa Sana, Mama Anna Makinda.

Aliposimama na kunza kuongea, kwanza nilinote, anaongea akiwa na pressure, huku anajitahidi sana kubana pumzi, kama vile anataka kutangaza taarifa muhimu, ningekuwa siko mjengoni, ningeweza kudhani labda kuna taarifa ya msiba!.

Kumbe, alikuwa anatangaza Kikao cha Bunge Cha Jioni Hii, kilichokuwa kijadili utendaji usioridhisha wa TICTS na RITES, kimeahirishwa ghafla kufuatia taarifa hizo zote mbili kutokuwa tayari!.

Hivi jamani, hii ni serikali inalichezea bunge na kulifanyia mzaha, au ni Bunge lenyewe haliko serious enough hivyo serikali kulifanya bunge ni shamba la bibi!?.
 
sasa na wewe huna kazi zingine za kufanya???????????? ulitegemea bunge la tanzania liwe naman gani leo???? ulifikiri wakiikuona pale watakuogopa waanza kuwa serious????????

kuwa serious pleas!!!!!!!!!!!!
 
Waheshimiwa wabunge wa wachangiaji wa humu JF kuweni na busara na hekima kujadili mambo.

Pasco alipoanza kusimulia yuko sahihi kwakuwa kiutaratibu wabunge pale hawana la kusema zaidi ya kutii maamuzi ya naibu spika. Matatizo yapo pande mbili, kwanza kwa serikali ambayo bila hofu wanaamua kutowasilisha ripoti hizo wakijua bunge halitawafanya chochote.

Pili ni wabunge wenyewe kufanywa shamba la bibi kila waziri anaamua kufanya lolote kama alivyofanya Kawamba kutowasilisha akiwa na uhakika na anachofanya kwakuwa bunge toto tu.

Hapo ndo mjenge mjadala wenu, kwamba what was the reason, who caused it, sheria na taratibu zinasemaje and whata next.
 
Usikatishe tamaa wapambanaji/ wafuatiliaji wa mambo...kama umeona habari hiyo haifai kwako ipotezee kuliko kutoa comments za kukata tamaa!

alikuwa anapambana na nini sasa, hakuna mpambanaji hapo...................... vinginevyo saa hizi angekuwa kishafungwa pingu anaisaidia polisi!!!!!!!!!
 
Naanza kuamini Bunge ni chombo cha serekali ni muhimili usiojiamini na kusahau wajibu wa kuwakilisha wananchi. Masuala yanayohusu maslahi ya watu na maendeleo yao si muhimu kama maslahi ya chama hawako tayari kuiweka serekali yao kikaangoni. Tusubiri tuone lakini kwetu matatizo ni sehemu ya maisha yetu wao wanangoja asilimia maana wanajua hatuna ubavu wa kuwawajibisha tumelewa mvinyo unaoitwa amani na utulivu. Usipige kelele
 
Naanza kuamini Bunge ni chombo cha serekali ni muhimili usiojiamini na kusahau wajibu wa kuwakilisha wananchi. Masuala yanayohusu maslahi ya watu na maendeleo yao si muhimu kama maslahi ya chama hawako tayari kuiweka serekali yao kikaangoni. Tusubiri tuone lakini kwetu matatizo ni sehemu ya maisha yetu wao wanangoja asilimia maana wanajua hatuna ubavu wa kuwawajibisha tumelewa mvinyo unaoitwa amani na utulivu. Usipige kelele

hadi leo ulikuwa hujaaamini??? sasa ulikuwa unafanya nini humu jamvini??????///
 
Mihimili yetu mitatu, Mahakama, Bunge na Katiba huwa vinaniacha hoi sana! Kila kitu sisi bora liende.
 
sasa na wewe huna kazi zingine za kufanya???????????? ulitegemea bunge la tanzania liwe naman gani leo???? ulifikiri wakiikuona pale watakuogopa waanza kuwa serious????????

kuwa serious pleas!!!!!!!!!!!!

Mzee, badala ya kumpongeza kwa kazi nzuri ndiyo unakuja na hii??? Kazi kweli kweli!!!!!!!
 
Mihimiri yetu mitatu, Mahakama, Bunge na Katiba huwa vinaniacha hoi sana! Kila kitu sisi bora liende.
Mkuu, hawa wanacheza na watanzania ambao 70% hawajui walipo wala hawajui nn tofauti kati ya maamuzi magumu na maamuzi ya kawaida (popular decisions and unpopular decision)

Obama alisimamia mswada wa afya akijua kabisa kuwa wapinzani na wamerekani wengi walikuwa hawauamini sana. alifanya unpopular decision...maamuzi magumu..........sisi tunataka Kaka yetu wa msata atuambie Kagoda ni nani.....kitu ambacho kila mtu anataka kusikia, eti tunasema ni maamuzi magumu kwake kuyafanya just because he doesnt want to respond......sisi hao tutawapa kura hawa jamaa.......of all the places, Dar ndo kwenye "supposedly" waelewa wengi na wanaopata habari kirahisi zaidi, lakini tutawapa hawa hawa!!

aaaagrrrrrrrrrrrr
 
Mihimiri yetu mitatu, Mahakama, Bunge na Katiba huwa vinaniacha hoi sana! Kila kitu sisi bora liende.

Mkuu nchi hii kuna mhimili mmoja tu nao ni RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa chama tawala.

Hii mingine unayoita mihimili ni vitendea kazi tu vya mhimili mkuu. Kimsingi ili kuokoa kodi za wananchi tungeweza kufuta hili bunge kwani bunge lenyewe linafanya kazi kwa kutegemea maelekezo toka kwenye mhimili mkuu.
 
I pointed out before that our parliament is not even a rubber stamp anymore, it is more like an empty shell.
 
Hivi Spika 6 alipodai kuwa Bunge linaweza "kwenda mbali zaidi" dhidi ya Serikali kuhusu Richmond alisahau kwamba simba alikuwa amelala tu na walikuwa wanamchezea sharubu wakati wote! Sasa hivi simba yuko macho masaa 24 hasa wakati makazi yake yanapotaka kuporwa mwezi Oktoba mwaka huu!
 
20% ya Wabunge ni mawaziri.

Assuming kwamba wale 'werevu' zaidi ndio huteuliwa kuwa Mawaziri, kwa hiyo 'top 20%' ya wabunge hugeuka kuwa ni sehemu ya serikali.

UfuNG'OMBE bin ufuMBUZI ni kuwa Waziri asiwe Mbunge. Hii itafanya top 20% ya wabunge wabakie kuwa wabunge. Kwa mujibu wa Pareto Principal, 20% hufanya 80% of contribution everywhere. Kwa hiyo tukiwatoa hao top 20% ya Wabunge, tutegemee perfomance ya bunge kuwa 20% ya ile ambayo ingejumuisha wale wabunge 'werevu'.

Hata hao wabunge waliobaki, top 20% yao inayotegemewa kutoa kutoa 80% of output (per Pareto principal), nayo 'inaishi kwa matumaini' kwamba siku moja mkuu wa kaya anaweza kuwakumbuka na kuwaweka kwenye 'ulaji' wa uwaziri. Kwa hiyo michango yao ni ya 'kujikomba' kwa sirikali na chama 'twawala'...

This leaves us with 20% of 20% of anticipated Bunge output. Kwa maneno mengine, tutegemee 1% ya kazi za bunge ambalo Wabunge si mawaziri.

No wonder bunge hilohilo limepitisha na kuridhia EAC, wakati EAC takes away power from wao...

Anyone expecting hiyo 1% output iwe na manufaa kwa taifa, anahitaji apewe ushauri na pia saa (asije akaendelea kupoteza muda).
 
nawasilisha hoja binafsi,kwa kuwa bunge hili ni mwanasesere,kwa nini tusiamue tusiwe na wabunge kwa miaka mitano halafu tuwe na rais dicteta mstaarabu atakae simamia raslmali zetu?na ustawi wetu kama kagame hivi.halafu tuone kuliko usanii huu wa kupoteza pesa nyingi za posho za hawa waishiwa?
 
1. CCM ushindi ni lazima...
2. Mtaji tuliyo rithi toka enzi za mfumo wa chama kimoja unatuwezesha kutawala milele!...
3. Vyombo vyote vya Usalama tunavimiliki c c m...abishae analo! Pingu tu...
4. Wananchi hawahitaji; maji safi na salama, barabara za lami, elimu ya kiwango, huduma bora za afya kwani tabibu za kijadi zinatosha, ..... wananchi wanahitaji; muda mwingi wa kulala na kupumzika na wandani wao, mlo mmoja kwa siku, watoto wasiwasumbue wazazi wakiwa wamepumzika!!!! ...

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.... Ushindi ni LAZIMA!!!!!!!


 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom