Swali: Serikali ina mpango gani wa kuwapatia mawasiliano ya barabara halmashauri za mkoa wa Simiyu?
Majibu: Serikali inapanga kujenga barabara yenye urefu wa km 42km kwa kiwango cha Changarawe na katika bajeti ya mwaka 2016/17, serikali imetenga shilingi milioni 246 kutekeleza mpango huo.
Swali : Kwa nini serikali isifanye shule ya sekondari ya Mchinga kuwa na kidato cha tano na sita iliyopo katika mkoa wa Lindi?
Majibu : Serikali imetenga shule hiyo ya Mchinga kuwa ya kidato cha tano na sita, na wizara ya elimu itatuma wataalamu kukagua shule hiyo na ikijiridhisha itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Swali : Ni lini serikali itajenga zahanati kila kijiji na kituo cha afya kila kata?
Majibu : Serikali kwa kushirikana na wananchi imeanza ujenzi wa hospitali kila wilaya na pia hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la vituo vya afya kwa asilimia 31.9.
Serikali imetenga shilingi bilioni 181.5 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya afya nchini.
Swali : Serikali ina mpango gani wa kudhibiti mafuriko na majanga katika mkoa wa Mara?
Majibu : Serikali imechukua hatua kama ifuatavyo:
1.Kuelimisha wananchi wanaojenga maeneo ya mabondeni waache kufanya hivyo,
2.Kubaini na kuwataka wakazi wote wanoishi mabondeni kuhama ili kudhibiti uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji,
3. Kuhimiza upandaji miti,
4.Kudhibiti uharibifu wa misitu.
Aidha serikali inahimiza wananchi na wadau wote wa mazingira kupanda miti kila mwaka.
Swali : Ni marekebisho gani ya sheria ya tumbaku ya mwaka 2013, yaliyowanufaisha wakulima moja kwa moja?
Majibu : 1.Viongozi wabadirifu wamechukuliwa hatua za kisheria hasa katika mikoa ya Tabora na Ruvuma
2.Sheria imesaidia vyama kutoingia katika madeni
3.Tozo zote zinatozwa na vyama vya ushirika vinawanufaisha wakulima.
Serikali inafanya mpango wa kupitia tozo zote zinatozwa kwa wakulima na itawasilisha bungeni punde utakapokamilika.
Swali : Kuna kodi 26 katika kilimo cha kahawa, kwa nini serikali isifute kodi hizo kandamizi kwa wakulima?
Majibu: Ni kweli kuna kodi nyingi zinazotozwa kwenya zao la kahawa na mazao mengine. Serikali inapitia kodi na tozo zote katika mazao ya biashara ikiwemo zao la kahawa, kodi au tozo zitakazoonekana kandamizi kwa mkulima zitaondolewa.
Swali : Viwanda vya ushashi gineries na ubara gineries havifanyi kazi, serikali inatoa kauli gani?
Majibu : Serikali inatambua hilo, serikali imeanza mchakato wa kufufua viwanda hivyo. Aidha mkoa wa Mara una gineries tatu za pamba na wananchi wanashauri kuzitumia hizo.
Wakulima wengi wanauza pamba ikiwa ghafi hivyo kutonufaika ipasavyo, serikali ina mpango wa kuwawezesha wananchi kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuongeza thamani ya zao la pamba.
Serikali itapunguza bei ya pembejeo ili kupunguza gharama ya uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima.
Swali : Serikali ina mpango gani wa kujenga viwanda vya kusindika mazao katika mkoa wa Geita?
Majibu : Serikali inahamasisha wananchi na wadau kuwekeza katika viwanda ili kuweza kukuza viwanda nchini.
Inawataka halmashauri za miji na majiji kutenga maeneo kwa ajili ya kuwekeza katika viwanda.
Serikali inafuatilia mwekezaji maarufu wa juisi duniani kuja kujenga kiwanda cha juisi mkoani Geita.
Aidha serikali imetenga kiasi cha shilingi bilion 15 katika bajeti yake kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa vijana kuhusu kujiajiri na kutumia rasilimali zilizopo.
Swali : Ni lini serikali itajenga barabara ya Ulyankulu kwa kiwango cha lami?
Majibu : Kipaumbele cha serikali kwa sasa ni kuunganisha mikoa kwa barabara za lami, mpango huo ukikikamilika serikali itaanza kujenga nyingine.
Hata hivyo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ukikamilimilika serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe wakati inatafuta fedhaza kujenga kwa kiwango cha lami.
Swali la Nyongeza : Serikali ina mpango gani wa kupanua daraja la mto Wami?
Jibu : Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga fedha kwa ajili ya kupanua daraja la mto Wami
Swali : Serikali ina mpango gani wa kudhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia bandadari bubu?
Majibu : Serikali inatambua uwepo wa bandari bubu, Serikali imeanzisha utaratibu wa kufanya vikao na wakuu wa mikoa ya ukanda wa Pwani kwa kushirikiana na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na vyombo vya ulinzi na usalama.
Kwa kutambua umuhimu wa bandari hizo, serikali imeanza utaratibu wa kurasimisha bandari hizo.
Baadhi ya bandari zilizotambuliwa ni Mbweni, Mlingotini, Mkilambo na Kilwa kivinje
Aidha mpaka sasa bandari 9 zimetambuliwa na kurasimishwa.
Kwa Mwaka jana 2015 jumla ya wafanyabiasha 81 walikamatwa na jumla ya wafanyabiashara 17 wamekamwatwa kwa mwaka huu 2016