Bunge la 11, mkutano wa 3, kikao cha 17
Maswali na majibu
Maswali na majibu
Swali: Ni lini serikali itapeleka gari jipya katika hospitali ya wilaya ya Tunduru?
Majibu: Halmashauri imetenga shilingi Milioni 141 kwa ajili ya kununua gari ya kubebea wagonjwa. Pia zimeombwa shilingi milioni 300 ambapo serikali inahakikisha fedha hizo zinapatikana.
Aidha serikali imepanga kufanya sensa maalum ili kuja na mpango mkakati wa ujenzi wa zahanati na hospitali kwa kuzingatia idadi ya watu katika eneo husika.
Swali: Ni kwa nini shule ya serikali ya wasichana ya Nyamkungu inaendelea kuwa ya kutwa na haipandishwi hadhi kuwa ya bweni?
Majibu: Halmashauri inatakiwa kutuma maombi wizara ya elimu kuomba shule kuwa ya bweni hadhi. Wizara itatuma wataalamu kuhahakiki kama inakidhi mahitaji na ikiridhika, itapandishwa hadhi.
Swali: Ni lini serikali itaweka mfumo wa uandaaji wa mafuta nchini na kupunguza gharama ya kuagiza kutoka nje?
Majibu: Serikali kupitia wizara ya viwanda inajipanga kuhakikisha nchi inajitegemea katika mafuta. Aidha serikali inahimiza kila kaya kulima angalau hekari moja ya alizeti katika mikoa inayostawisha mazo haya (Singida na Kigoma) ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta unakuwepo nchini.
Swali: Je serikali ina mpango gani wa kukarabati makazi ya askari hasa Zanzibar?
Majibu: Serikali ina mpango wa kufanya ukarabati katika makazi ya polisi na gharama halisi ni shilingi bilioni 1.5.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kuwaunga mkono wachimbaji wadogo wadogo wa Busiri
Majibu: Wizara imetenga eneo lenye ukumbwa wa hekta 11,000. Wizara tayari imegawa lesini 81. Pia serikali inawapatia ruzuku na elimu wachimbaji hawa. Pia serikali inawatembelea wachimbaji hawa.
Swali: Ni lini serikali itasimamia kukamilika zoezi la kuunganishwa umeme katika jimbo la Geita vijijini?
Majibu: REA na TANESCO wameongeza kasi kuhakikisha kazi ya kuunganisha umeme inakamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Suluhisho la kukatika kwa umeme ni kupitia mradi unaotoka Mbeya wenye kilovolti 400.
Aidha REA awamu ya tatu inatarajia kusambaza umeme kila kijiji nchini.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kuvizalisha viwanda ambavyo havifanyi kazi au vinasuasua?
Majibu: Viwanda vinavyosuasua ni vile vilivyobinafsishwa. Serikali inawasiliana na wawekezaji ili kuhakikisha viwanda hivyo vinafanyakazi. Pia serikali inavishauri kutumia teknolojia ya kisasa. Aidha serikali inawashauri kuwashirikisha wawekezaji wengine pale wanaposhindwa kuviendesha. Serikali itahakikisha kunapatikana umeme wa uhakika na kuondoa tozo zisizo na tija.
Serikali itavitaifisha viwanda vinavyokiuka mkakataba wa uwekezaji na kupewa mwekezaji mwingine.