Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo Mei 05, 2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Bunge la JMT

Waziri wa katiba na sheria analeta hotuba ya bajeti ya wizara,

Taarifa ya kamati ya katiba na sheria kwa mwaka wafedha 2016-2017 na mapendekezo

Msemaji wa kambi ya upinzania anawasilisha mezani kauli ya kambi ya upinzani juu ya makadirio ya wizara ya katiba na sheria

==================================

MASWALI KWA WAZIRI MKUU


Swali: Serikali unamkakati gani kuondoa tozo kwa mkulima wakorosho
Majibu: Serkali imefanya maamuzi ya kupunguza tozo zote za hovyo haswa zile za asilimia 15 katika vifungashi na tozo imeondoka na kukabidhiwa kwa mfuko wa Wakfu ulioundwa na wadu na utasimamia ununuzi wa pembejeo na kugharamia tatizo hivyo itabakia asilimia 65.

Swali: Serikali iko tayari kuwalipa wakulima wanao dai fedha zao
Majibu: Uko uendeshaji wa hovyo kwenye vyama vya msingi na vyama vikuu serikali imeandaa usimamizi wa dhati ili wakulima wote wapate maslahi, mifumo inayotumika sio ya serikali ni ya wakuima wenyewe katika kuuza na kusimamia na ni wajibu wa wakulima kuwauliza viongozi wao wa vyama vya msingi na vyma vikuu na wasilipo ridhika wanaweza kwenda mahakamani ili kuwawajibisha watendaji wabovu na hii ni kwa wakulima wote.

Swali: Katika miaka ya karibuni kumekuwa na migogoro mingi ya wakulima, wafugaji na maliasili, serikali lini itateua kamati ya kitaifa kupitia mapendekezo ya jinsi ya kuondoa migogoro kwa amani
Majibu: Ipo migogoro mingi ya wafugaji na wakulima katika jamii na umefika wakati wa kuitafutia ufumbuzi na serikali imeanza kuondoa migogoro ya ardhi. ili kuondoa migogoro na pia kuna watendaji wa hovyo na wapo waekezaji wanaoingia kinyemela na kuleta migogoro na serikali imeandaa task force ya wizara za ardhi, kilimo na maliasili ili kubainisha mipaka na mwisho seriakali kuweka mipaka. Na wafugaji wote watatengewa maeneo kama Lanchi.

Swali: Ni lini waziri kuu atatembelea Tabora kujionea migogoro?
Majibu: Atafanya ziara mara baada ya bunge kuisha ili kuongea na watu walio na migogoro na wadau wa kilimo cha tumbaku ili kuleta tija

Swali: Kwasababu gani serikali haijapeleka ripoti ya haki za binadamu umoja wa mataifa
Majibu: Serikali imeridhia mikataba mingi ili kuridhia na kufungua milango ili kuwafanya wenzetu wenye uemavu kuwa sehemu ya maendeleo ya taifa. Serikali itafanya mapitio ya awamu iliyopita ili kuandaa makakati wenye tija.

Swali: Serikali imejipanga vipi kutekeleza ahadi za kujenga barabara
Majibu: Ahadi zote zitatekeleza na barabara zitajengwa kwa kiwango cha lamu, na serikali imeanza kwa kuunganisha mikoa kwa barabara na baadae kujenga barabara za kuunganisha wilaya na ahadi zote za rais zitatekelezwa.

***Swali la nyongeza limekatishwa kwasababu Mbunge aliyetakiwa kuuliza amedhihirika hakujiandaa

Swali: Serikali imejipangaje kuzifanya halmashauri kuwa wanahisa katika kila miradi katika halmashauri zao
Majibu: Halmashauri kupitia TIC watakuwa wasimamizi na watanufaika kupitia uwekezaji unaofanya katika eneo lao na watakuwa na benki ya ardhi ili kuwafanya nao kuwa wanahisa kwa utaratibu utakaowekwa. Serikali itawaunganisha wawekezaji na halmashauri na kwakuwa halmashauri watakuwa wemandaa makubaliano.

Swali: Tozo zinazotokana na ardhi ni kama katika uwekezaji, kwanini serikali isiwafanye halmashauri ya Temeke kuwa wanahisa katika miradi yao
Majibu: Serikali imegundua kuna usimamizi mbovu, na halmashauri ya Temeke imepata muwekezaji wa kichina na halmashauri sasa iko kwenye mjadala wa tozo na manufaa itakayopata. Serikali inandaa utaratibu ili halmashauri zinufaike. Halmashauri zote ziwe makini kusimamia tija ya wawekezaji katika halmashauri zetu.

Swali: Mvua zinaharabu mazao na kueta vihashiria vya njaa, je serikali imejipangaje na tishio la njaa katika taifa
Majibu: Serikali inatoa pole kwa wananchi wote waliokumbwa na mafuriko, baada ya kupata taarifa kutoka mamlaka ya ali ya hewa na inaonyesha mvua zitaendelea kwa kubwa na serikali imejipanga kupitia kitengo ch maafa na kufanya tathmini kupitia halmashauri na serikali itaendelea kupeleka misaada katika sehemu zilizopata maafa.

Swali: Wanafunzi hawatakiwi kufanya siasa vyuoni na menejimenti ziepewa maelekezo kuaadhibu wanafunzi walio kinyume na sera za CCM haswa chuo kikuu cha Dodoma.
Majibu: Sio kweli kwamba kuna maelekezo kwenye vyuo na hakuna unyanyasaji unaofanywa katika vyuo, na watanzania wote wanauhuru wa kujiunga na vyama wanavyotaka lakini hawaruhusiwi kufanya siasa wakati wa masomo wala kazi. Nawasihi viongozi kuwa sio msimamo wa serikali na watanzania wote Tanzania ni yetu sote na kila mtu anauhuru wa kupenda chama anachotaka lakini lazima matakwa ya sehemu husika yafuatwe.

MASWALI NA MAJIBU KWA WAZIRI MKUU YAMEKWISHA

====================================

MASWALI YA KAWAIDA


Swali: Je vikundi vingapi vimenufaika na mikopo katika halmashauri
Majibu: Katika mwaka wa fedha 2015-2016 vikundi vingi katika mkoa wa Iringa vitanufaika na mikopo.

Swali:
Je lini serikali itakamilisha kipande cha Dodoma-Mayamaya kwa kiwango cha lami
Majibu: Barabara hii inaendelea kujengwa kwa sehemu tatu moja kutoka Dodoma mpaka mayamaya Km 43 na Mayamaya kwenda Vela na Vela mpaka Bomba. Mkandarasi alisimama baada ya kuchelewa kwa malipo na sasa amelipwa na atamaliza kazi mwezi disemba mwaka 2016.

 
Wanatuonenya live wakiwa wanabembelezana,wakati wa hoja za wawakilishi wa wananchi ndio wanazima!Huu ni ujinga na upuuzi uliokithiri.
Kwani kipindi cha maswali na majibu wenye tv wanakuwa wameongezeka?watu wanakuwa hawako makazini?Gharama hazisomi wakati huo?
 
Back
Top Bottom