Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU
BUNGE LA 11-MKUTANO WA 3
OFISI YA WAZIRI MKUU
Swali: Swala la kuhamia Dodoma limechukua muda mrefu serikali ina msimamo gani?
Majibu: Serikali imeshaanza kutunga sheria ya makao makuu ya nchi. Na muswada utaletwa bunge ili iwe sheria rasmi.
OFISI YA WAZIRI MKUU TAISEMI
Swali: Je ni lini serikali itatoa kauli rasmi ili ofisi za wizara zianze kujengwa na kuendelezwa Dodoma.
Majibu: Baada ya sheria kupitishwa kila hatua ya kuhamisha makao makuu litafanyika kisheria
Swali: Kituo cha Afya Chamwino Ikulu kinahudumia watu wengi sana na haki a kifaa cha CT-Scan
Majibu: Kifaa cha CT Scan kina gharama ya Tsh Mil 72. Hivyo serikali imeandaa utaratibu wa kununua kupitia bajeti ya 2016-2017.
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Swali: Ni lini serikali italeta sheria bungeni ili miaka ya hifadhi isogezwe na watu wapate sehemu za kulima?
Majibu: Serikali imeandaa zoezi litakalo husisha wizara 6, ili kufanya mchakato wa kutafuta ardhi kwaajili ya kilimo.
Swali: Wananchi wa Songea mjini hawana umeme wa uhakika na waategemea umeme wa chama cha Masista je werikali inamkakakati gani?
Majibu: Serikali imeanza kupeleka umeme wa grid ya taifa na utagharimu jumla ya Dolla Kimarekani mil 34.68
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Majibu: Chini ya Katiba ya Tanzania 45 mamlaka ya rais yako ktk kumsamehe mtu aliyekatika tuhuma lakini hakutumia kifungu hiki.
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Majibu: Serikali inatambua umuhimu wa huduma hii na ndio maana imeweka vifaa maalumu kwaajili ya kubebea walemavu, wagonjwa na wenye matatizo. N aimeweka huduma hizi katika viwanja vya Mwanza , Mafia, Tanga, Songwe, Mtwara na lift katika kiwanja cha Bukoba.
Swali: Je ni ini serikali itaanza kujenga soko la Kagunga lililopo mpakani mwa Tanzania na Burundi
Majibu: Soko la Kisasa Hekta 1 mil 200 ujenzi juhudi zakumpata mzabuni zinaendelea.