Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo 21.04.2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Kipindi cha maswali na majibu

Swali:
Je ni utaratibu gani ambao serikali imeweka kuwarudisha watanzania waliofikishwa kwenye balozi zetu, na je mawakala wanaopeleka watu nje wanaifidia vipi serikali?

Majibu:
Serikali imeweka utaratibu maalum na watanzania wanapokwenda nje ya nchi wanatakiwa kufuata taratibu halali na mawakala watachukuliwa kwa kutokufuata sheria.

Swali: Katika kituo cha afya cha Nzela-Geita lini kitakuwa hospital ya wilaya na lini hospitali ya Geita itakuwa hospitali ya mkoa na kuongezewa watumishi

Majibu: Waziri atafanya ziara na kuongeza watumishi kabla ya kuwa hospitali ya mkoa.

Swali:
Je lini serikali itatenga bajeti ya kujenga hospitali za wilaya nchi nzima
Majibu: Katika bajeti inamikakati kwaajili ya kuendeleza sekta ya afya kwa wilaya zote.

Swali:
Je kwa kiasi gani mfumo wa kupima utendaji kazi kwa uwazi
Majibu: Mfumo wa kupima utendaji kazi kwa uwazi ulianza mwaka 2004, na serikali inatarajia kuanza utekelezaji wa mfumo huu kwa mwaka 2016/2017 katika taasisi zote za umma.

Swali: Kwakuwa taasisi nyingi azifuati huu mfumo, je ni hatua gani serikali imechukua kwa watumishi wasiofuata mfumo huu, na kwakuwa kutangaza hadharani taasisi zinazofanya vizuri na vibaya ni jambo zuri kwanini serikali isianze kutekeleza utaratibu huu.
Majibu: Kuanzia 2010 katibu mkuu utumishi alitoa agizo la kutumia mfumo huu na kuweka tozo kwa watumishi wasio tumia mfumo huu. Serikali inpokea mapendekezo kuhusu pendekezo la kutangaza hadharani.

Swali: Kwakuwa matatizo ya jimbo la Kigambo kuhusu mahakama ya mwanzo, lini serikali italeta mpango wa kuboresha mahakama za mwanzo Buguruni, Temeke.
Majibu: Wiki mbili zijazo wizara itawasilisha mpango wa ujenzi wa mahakama ya mwanzo nchini kote.

Swali: Kwanini serikali iliwekeza kwenye kiwinda cha General Tyre bila ya mpango wa kitaalam.
Majibu: Serikali haiwezi kuwekeza kwenye kiwanda bila ya ruzuku, serikali inataka kukitoa kiwanda kwenye mfumo wa ruzuku, sasa lazima wapatikane wahisani kwa mkopo nafuu na ruzuku iende kwa wananchi.

Swali: Kumekuwa malalamiko mengi ya wastaafu na ni lini watapewa fedha zao?
Majibu: Bodi zinaendelea na mchakato baada ya SSRA kumalizia utaratibu wa malipo
 
Tunashukuru kwa update , ila inahitaji moyo wa uvumilivu sana kufuatilia bunge la sasa hivi
 
Mimi nataka live ya Sauti ya muhusika, hapa bado unaweza kuedit hakuna tofauti na walichofanya ccm kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya tv na radio
 
Back
Top Bottom