Yaliyojiri BOT: Kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na India

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
Wanabodi,

Niko kwenye ukumbi wa BOT hapa jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika kongamano kubwa la kibiashara kati ya India na Tanzania ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.

clip_image002.gif

clip_image004.gif

clip_image006.gif
KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA

Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji linalofanyika leo Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi hapa katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la Kongamano hili ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha wafanyabiashara kutoka katika sekta zifuatazo: Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara. Makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi tano za juu kiuwekezaji hapa nchini (kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji). Kulingana na takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, Kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2.122. Miradi inayoongoza katika kusajiliwa na TIC katika kipindi hicho ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53% ni miradi ya kutoka sekta hii.

Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unashiriki ila idadi kubwa ni wafanyabiashara Watanzania wenzetu wenye asili ya India.

Kwa sasa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, ndio anahutubia.

Fuatana nami.

Paskali
 
Wanabodi,

Niko kwenye ukumbi wa BOT hapa jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika kongamano kubwa la kibiashara kati ya India na Tanzania ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu.

clip_image002.gif

clip_image004.gif

clip_image006.gif

INDIAN BUSINESS FORUM

TANZANIA

clip_image008.gif
clip_image010.gif
TAARIFA KWA UMMA

KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA INDIA

Kufuatia tukio la ugeni wa kitaifa wa Mheshimiwa Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India hapa nchini, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), pamoja na Jukwaa la Biashara la India (IBF) na Shirikisho la Biashara na Viwanda la India (FICCI) wanaandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Siku ya Jumapili tarehe 10 Julai 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.

Lengo kuu la Kongamano hili ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara wa nchi hizi mbili kukutana pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya biashara na uwekezaji.

Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka India utajumuisha wafanyabiashara kutoka katika sekta zifuatazo: Kilimo, Viwanda, Miundombinu, Elimu, Afya, Nishati na Maji.

Tanzania na India ni nchi zenye ushirikiano wa muda mrefu katika masuala ya kisiasa, kijamii na kibiashara. Makampuni kutoka India ni miongoni mwa mataifa yanayoshika nafasi tano za juu kiuwekezaji hapa nchini (kwa kuzingatia thamani katika uwekezaji). Kulingana na takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania kati ya mwaka 1990 na Juni 2016, Kituo kimeweza kusajili jumla ya miradi 442 ya uwekezaji kutoka India yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2.122. Miradi inayoongoza katika kusajiliwa na TIC katika kipindi hicho ni ile iliyopo katika sekta ya viwanda na usindikaji ambapo takribani asilimia 53% ni miradi ya kutoka sekta hii.

Umma wa wafanyabiashara kutoka Tanzania unashiriki ila idadi kubwa ni wafanyabiashara Watanzania wenzetu wenye asili ya India.

Kwa sasa Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa, ndio anahutubia.

Fuatana nami.

Paskali
Wahindi wataishia kuuza spare za pikipiki zao Kariakoo! kama wachina walivyokuja eti ni wawekezaji, sasa wanauza spare za pikipiki zao na karanga mitaani! Kupoteza muda tu na wahindi
 
Mkuu acha negativity, be positive!, kwa kukusaidia tuu kama hujui, uchumi wa nchi hii, umeshikwa na Wahindi!. Uko mikononi mwao!. Wahindi hawa, ni wale Wahindi masikini ambao waliletwa nchini kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati, ujira wa ukibarua wao, ndio wakautumia kujengea yale maghorofa yote mijini!. Watanzania where are we?!.

Kama Wachina na Wahindi wanaishia kuuza spea na karanga mitaani, wameona there is an opportunity, they seize it na kuitumia!, Sisi Watanzania tunachangamkia nini?!.

Hata ikitokea una mkeo, kazi yako ni kulala tuu, akatokea jirani kukusaidia kumtimizia, wewe unapaswa kumshukuru huyo jirani anayekusaidia pale uliposhindwa na sio kumlaumu!.

Kama soko linahitaji karanga, wewe mwenye hizo karanga umeshindwa kuzifikisha sokoni kwa walaji, kuna ubaya gani Mhindi kutoka India na Mchina kutoka China kuja nchini kwako, kuzikaanga karanga zako, na kuwauzia watu wako wanaopenda kula karanga?!.

Paskali
 
Mimi ni mfanyabiashara wa uuzaji wa madini semi precious stones,wadau wakubwa ambao nawauzia ni wahindi wanatokea jaipur,Walioko hapa dar ambao ni wanunuzi na india Kuna market kubwa ya madini haya kwani wana viwanda vya kutengeneza bids.
Wanunuzi waliyoko kwa sasa ni wachache kwa maana ya kwamba waliyopo wanalalia sana ktk
Bei za kununua.
Ningependelea wanunuzi waongezeke zaidi ili kuwepo na competition kwa buyers....
Je ktk msafara wa waziri Mkuu huyó Kuna wafanyabiashara haooo..
 
Mkuu acha negativity, be positive!, kwa kukusaidia tuu kama hujui, uchumi wa nchi hii, umeshikwa na Wahindi!. Uko mikononi mwao!. Wahindi hawa, ni wale Wahindi masikini ambao waliletwa nchini kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati, ujira wa ukibarua wao, ndio wakautumia kujengea yale maghorofa yote mijini!. Watanzania where are we?!.

Kama Wachina na Wahindi wanaishia kuuza spea na karanga mitaani, wameona there is an opportunity, they seize it na kuitumia!, Sisi Watanzania tunachangamkia nini?!.

Hata ikitokea una mkeo, kazi yako ni kulala tuu, akatokea jirani kukusaidia kumtimizia, wewe unapaswa kumshukuru huyo jirani anayekusaidia pale uliposhindwa na sio kumlaumu!.

Kama soko linahitaji karanga, wewe mwenye hizo karanga umeshindwa kuzifikisha sokoni kwa walaji, kuna ubaya gani Mhindi kutoka India na Mchina kutoka China kuja nchini kwako, kuzikaanga karanga zako, na kuwauzia watu wako wanaopenda kula karanga?!.

Paskali
We ni mtu mzima mwenye mke na watoto, mfano huo haukufai hata kidogo. Wakubwa hatuongei hivyo maana hujui kama watoto ulio nao ni wa kwako ! Kuna mifano mingi ambayo ungeliitumia kwa umri wako! Utatoa mfano kama huo mbele ya watoto wako? Nadhani hapo umekosa Busara Paskali!
Sasa ndio waitishe mikutano na mbwembwe zote kuja kuuza karanga Pasikali. Nilitegemea ungesema kuwa hapana tumejifunza ya wachina , hatutakubali Wahindi waje kihivyo! Tutawapa masharti ya uwekezaji siyo karanga etc. Pasikali unafahamika na wengi ukitoa mifano kama hiyo utawapa watu mashaka wanaokuamini kwa kujenga hoja za nguvu. Na si kweli kuwa vibarua wa kihindi kwenye ujenzi wa reli ndio walijenga maghorofa!
 
hapo kazungumzia fursa ya exportation ya nafaka kunde,dengu etc
hii pia inabidi uwepesi uwekwe na tuwe makini tusije jikuta ni wahindi tu ndio wanaexport hizo kitu india.
Serikali itoe elimu kwa wakulima wa dengu na choroko au mbaazi wa mfno singida,shinyanga, mwanz etc ikiwezekana hawa wakuu wa wilaya wafanye hiyo kazi, waunde vikundi ili hizo dengu wasafirishe wao wenyewe hadi india, Maana uzoefu unaonyesha wahindi ndio walanguzi wakubwa wa hizi kitu huko vijijini tena kwa bei isiyomnufaisha.
Hayo yaliyosemwa na rais yasiishie hapo ayadelevop into actionplans na zisambazwe nchi nzima na kusimamiwa kwa ufanisi.
Hao wanaotaka kujenga viwanda vya madawa nao wasije dsm tu wapewe maeneo mikoani(hapa ndio inakuja umuhimu wa reliable power supply na influstructure).
Pili hii nayo ya ciwanda kutoka india iangaliwe vizuri maana sera za huyu jamaa ni kuvutia wawekezaji wawekeze india ili wapromote export kwa nchi kama za kwetu labda kama atusaidie kwa maana ya msaada.
 
We ni mtu mzima mwenye mke na watoto, mfano huo haukufai hata kidogo. Wakubwa hatuongei hivyo maana hujui kama watoto ulio nao ni wa kwako ! Kuna mifano mingi ambayo ungeliitumia kwa umri wako! Utatoa mfano kama huo mbele ya watoto wako? Nadhani hapo umekosa Busara Paskali!
Sasa ndio waitishe mikutano na mbwembwe zote kuja kuuza karanga Pasikali. Nilitegemea ungesema kuwa hapana tumejifunza ya wachina , hatutakubali Wahindi waje kihivyo! Tutawapa masharti ya uwekezaji siyo karanga etc. Pasikali unafahamika na wengi ukitoa mifano kama hiyo utawapa watu mashaka wanaokuamini kwa kujenga hoja za nguvu. Na si kweli kuwa vibarua wa kihindi kwenye ujenzi wa reli ndio walijenga maghorofa!
Mkuu Chuakacha, pole kwa kuumizwa na jibu langu, ila kiukweli mimi natoka Kanda ya Ziwa, kabila langu ndilo kabila linaloongoza kwa kupenda wanawake na kupenda watoto, haijalishi ni watoto wako au ni wakusaidiwa, kwa sababu tuna wanawake wengi, na watoto wengi, na hatumaindi kusaidiwa, ila watoto wote ni wetu na tunawapenda!.

Mimi mwenyewe japo naishi Bongo, wife wangu anaishi US, mimi na wife wangu wote ni weusi, ila mmoja wa kabinti kangu kalichozaliwa US ni keupe kutokana na hali ya hewa ya kule!, kabinti haka ndio my favorite kid!, hivyo usimaind sana comments zangu, zingatia tuu hoja zangu za msingi!.

Watanzania tumejaaliwa fursa kibao nchini mwetu, ila sisi ni wavivu, kuanzia kufikiri hadi kutenda!, tunapenda sana kulala tuu bila kufanya kitu, wakitokea wageni kuchangamkia fursa badala ya kushukuru, wamekuja kufanya kile sisi tulichoshindwa, tunaishia kulalamika na kuwalalamikia!, na tukiachiwa kufanya, tunaishia kushindwa!.

Fanya kazi, get rich, or die trying!.

Paskali
 
Mkuu acha negativity, be positive!, kwa kukusaidia tuu kama hujui, uchumi wa nchi hii, umeshikwa na Wahindi!. Uko mikononi mwao!. Wahindi hawa, ni wale Wahindi masikini ambao waliletwa nchini kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati, ujira wa ukibarua wao, ndio wakautumia kujengea yale maghorofa yote mijini!. Watanzania where are we?!.

Kama Wachina na Wahindi wanaishia kuuza spea na karanga mitaani, wameona there is an opportunity, they seize it na kuitumia!, Sisi Watanzania tunachangamkia nini?!.

Hata ikitokea una mkeo, kazi yako ni kulala tuu, akatokea jirani kukusaidia kumtimizia, wewe unapaswa kumshukuru huyo jirani anayekusaidia pale uliposhindwa na sio kumlaumu!.

Kama soko linahitaji karanga, wewe mwenye hizo karanga umeshindwa kuzifikisha sokoni kwa walaji, kuna ubaya gani Mhindi kutoka India na Mchina kutoka China kuja nchini kwako, kuzikaanga karanga zako, na kuwauzia watu wako wanaopenda kula karanga?!.

Paskali

Paskali unafeli sana.

Wahindi unaosema waliletwa kama vibarua wa kujenga reli,hapo ndio unapokosea.

Infact waliletwa na Waingereza sana sana kuwasaidia kutawala kwa level yoyote ile...Katika any social setting alianza Mzungu,then Muhindi then Mwafrica mkiani,katika kazi yeyote ile..walifaidika kwa kuwekwa daraja la kati makusudically..

Plus tuna bad blood with them historically,mi binafsi sitaki urafiki nao haijalishi wanatawala dunia au wana mali kivipi...snitches
 
Mkuu Chuakacha, pole kwa kuumizwa na jibu langu, ila kiukweli mimi natoka Kanda ya Ziwa, kabila langu ndilo kabila linaloongoza kwa kupenda wanawake na kupenda watoto, haijalishi ni watoto wako au ni wakusaidiwa, kwa sababu tuna wanawake wengi, na watoto wengi, na hatumaindi kusaidiwa, ila watoto wote ni wetu na tunawapenda!.

Mimi mwenyewe japo naishi Bongo, wife wangu anaishi US, mimi na wife wangu wote ni weusi, ila mmoja wa kabinti kangu kalichozaliwa US ni keupe kutokana na hali ya hewa ya kule!, kabinti haka ndio my favorite kid!, hivyo usimaind sana comments zangu, zingatia tuu hoja zangu za msingi!.

Watanzania tumejaaliwa fursa kibao nchini mwetu, ila sisi ni wavivu, kuanzia kufikiri hadi kutenda!, tunapenda sana kulala tuu bila kufanya kitu, wakitokea wageni kuchangamkia fursa badala ya kushukuru, wamekuja kufanya kile sisi tulichoshindwa, tunaishia kulalamika na kuwalalamikia!, na tukiachiwa kufanya, tunaishia kushindwa!.

Fanya kazi, get rich, or die trying!.

Paskali
You might be telling the truth or not. Let me believe your words with regard to watoto! Paskali ukiwa mbali na mke wako kwa umbali huo, lazima ukubali yote na ujifariji. How, kwa kutojali whatever comes out! Labd Paskali nakuona vibaya, it might be uko kwenye miaka ya ujana! I am over sixty, siwezi toa mfano kama huo mbele ya watoto, na kwenye kadamnasi . Tuyaache.

Paskali fursa zipi za wazi? Sidhani kama kuna mtu bado amelala era hii! Nakumbuka Mzee Mkapa alikuwa anaimba kama ulivyo nanga hizo fursa na hapo kwenye red, aliishia kufanya biashara akiwa Ikulu (kinyume na maadili) na kujiuzia Kiwila.

Kama fursa zingelikuwa kama unavyozinadi, asingelijiingiza kwenye maovu hayo makubwa! Fursa zingelikuwa wazi hivyo, wizi wa serikalini usingelikuwa to that magnitude! Paskali, mikopo imekuja juzi. Ndio unaona barabara zimejaa magari , boda boda etc. Wakati naajiliwa 1983, shuleni kwetu hakukuwa hata mwalimu mwenye baiskeli! Baadaye ndiyo BCU wakatoa mikopo kwa walimu tukapata baiskeli. Nikahama, nikaja kwenye shirika la Umma. Kulikuwa na watu wana PhD, Masters, well educated, alikuwa ni mmoja aliyekuwa na gari baada ya kutoka UK kwenye PhD studies. Hapakuwa na mikopo, fursa hazikuwepo. Salaries were too low to make any progress unless you swindle public funds!

All in all, kwa fursa za mikopo kwa sasa, nawahimiza vijana wasiogope mikopo, watumie fursa ya hiyo mikopo.
Paskali wasukuma wanauana sana kwa wivu unaposema hatumaind, sikubali!
Kazi njema!
 
Paskali unafeli sana.

Wahindi unaosema waliletwa kama vibarua wa kujenga reli,hapo ndio unapokosea.

Infact waliletwa na Waingereza sana sana kuwasaidia kutawala kwa level yoyote ile...Katika any social setting alianza Mzungu,then Muhindi then Mwafrica mkiani,katika kazi yeyote ile..walifaidika kwa kuwekwa daraja la kati makusudically..

Plus tuna bad blood with them historically,mi binafsi sitaki urafiki nao haijalishi wanatawala dunia au wana mali kivipi...snitches
Nashukuru kwa maelezo yako. Waliletwa kuwasaidia wazungu kutawala. Utakumbuka hata sheria nyingi za sasa ni za kutokea India. Hivyo walikuwa wa msaada mkubwa kwa waingereza katika kutawala. Na ndio walipata mikopo wakati huona kuweza kuwa na viwanja katikati ya mji na kujenga majengo aliyoyasema Paskali. Pakali arudie historia kidogo ajikumbushe. Manamba wa reli wasingeliweza kujenga maghorofa for sure
 
Paskali unafeli sana.

Wahindi unaosema waliletwa kama vibarua wa kujenga reli,hapo ndio unapokosea.

Infact waliletwa na Waingereza sana sana kuwasaidia kutawala kwa level yoyote ile...Katika any social setting alianza Mzungu,then Muhindi then Mwafrica mkiani,katika kazi yeyote ile..walifaidika kwa kuwekwa daraja la kati makusudically..

Plus tuna bad blood with them historically,mi binafsi sitaki urafiki nao haijalishi wanatawala dunia au wana mali kivipi...snitches
Mkuu, hawa jamaa waliletwa Tanzania kama vibarua wakati wa ujenzi wa reli ya kati kati ya Tanzania kati ya mwaka 1905-1914 enzi hizo Tanzania ikiwa chini ya utawala wa Mjerumani!. Hii ilifuati vibarua wa kiafrrika, wakiisha lipwa tuu mshahara, hawaji tena kazini mpaka fedha zao ziishe!.

Naomba kunukuu toka Wiki, "The Indian population in Tanzania expanded under British rule. Cheap indentured labour was brought, mainly from Punjab, for the construction of the railway, and while the majority of the railway workers returned to India after its completion, some remained. Other Indians arrived, from Gujarat, Punjab and Goa, drawn by the opportunities created by the opening of the railway". mwisho wa kunukuu!.

Paskali.
 
Paskali muongo mkubwa...reli ya kwanza east africa ni ya mjerumani na ilianzia pale Tanga Usambara 1893 ikaenda 40km tu mpaka Korogwe.

Mwaka 1904 ikaanza Dar mpaka Kigoma 1914 ambapo ni mwanzo wa WWI waingereza wanawashinda Wajerumani....hizi reli bongo hii mpaka hapo wamejenga wazungu wajerumani na waafrica tuu hakuna muhindi...saa hiyo India ni koloni la Waingereza,Mjerumani anajeuri ya kuwachukua wahindi wa punjab kupitia wapi?

Wahindi walitia maguu kwenye reli ya ya waingereza ya Mombasa-Uganda /Lunatic Line ambayo ilianza 1896-1901 na wahindi walioletwa ni 32,000 na baada ya kazi walirudi kwao na waliobaki ni 6,000 tu.

Wahindi waliletwa tanzania na waingereza walipochukua koloni baada ya kushinda WWI ambapo ni mbele ya 1914 huko ili wawasaidie kutawala kwenye level ya ukarani.

Uongo uongo wako eti waliletwa tanzania kuanzia mwaka 1905-1914 ni uongo maana muda huo wajerumani walikua ndio watawala tanganyika na wajerumani walikua hawana access yeyote ya wahindi wa india maana walikua chini ya uingereza.
 
Back
Top Bottom