Yaliyojiri Arusha katika mazishi ya waliouliwa na Polisi

Kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema
Ukatili, ukatili ni unyama
Ukatili, ukatili ni unyama

Mashujaa tutawakumbuka kwa wema
Mlokubali kujitoa muhanga

Kwa ajili ya kutetea haki zetu
Kwa ajili ya kutetea utu wetu
Afadhali ya kufa kuliko kuonewa
Afadhali ya kufa kuliko kunyanyaswa
Mashujaa tutawakumbuka daima ee MILELE.

…………….Kuzitoa roho za watu bila sababu
Hata watoto wadogo wamekosa nini ?
Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu
Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu

Hayo ni maneno ya Hayati Marijani Rajabu kwenye wimbo wake unaitwa UKATILI NI UNYAMA
 

Attachments

  • Ukatili_Ni_Unyama_MARIJAN_RAJABU_&_DAR_INTERNATIONAL_ORCHESTRA.mp3
    902.1 KB · Views: 88
Tuko hapa nje, tetese zimekuja kwamba kinachotuchelewesha Hapa ni mganga mkuu anasuasua kusaini!
 
Kamwe huwezi kuzuiya nguvu ya umma kwa kutumia risasi , mabomu na slaa nyingine
 
hapa mochwari namwona godbless lema.mbowe na wengine wengi sijui kuna mabishano gani huko ndani. ila bado tunasubiri tujue ni kitu gani kitaendelea.ila huku nje kila mtu anasema lake ila habari kamili 2tapata watakapotoka nje
 
Jamani nimeulizia kwanjia ya cm muda si mrefu naambiwa miili bado haijawasili. Wana JF twendelee kuhabarishana tusichoke. Tuko pamoja.
 
Kuna mwana JF nimeongea nae na simu kutoka Arusha ananiambia kuwa hospitalini walikuwa wamekataa kutoa miili bila kuifanyia postmortem wakati hiyo miiili imekaa mortuary almost 7 days sasa najiuliza hizo siku saba zote wakati miili iko hosiptali ni kitu gani kiliwashinda kuifanyia postmortem waje wafanye leo kama sio uzembe na upumbavu wasije wakawa na agenda zingine
 
hapa mochwari namwona godbless lema.mbowe na wengine wengi sijui kuna mabishano gani huko ndani. ila bado tunasubiri tujue ni kitu gani kitaendelea.ila huku nje kila mtu anasema lake ila habari kamili 2tapata watakapotoka nje

Thanks Kev yaani watu wanataka kuanza kuleta propaganda hadi kwenye miili ya watu waliokufa shame on them
 
Kila mtenda wema atakumbukwa kwa wema
Ukatili, ukatili ni unyama
Ukatili, ukatili ni unyama

Mashujaa tutawakumbuka kwa wema
Mlokubali kujitoa muhanga

Kwa ajili ya kutetea haki zetu
Kwa ajili ya kutetea utu wetu
Afadhali ya kufa kuliko kuonewa
Afadhali ya kufa kuliko kunyanyaswa
Mashujaa tutawakumbuka daima ee MILELE.

…………….Kuzitoa roho za watu bila sababu
Hata watoto wadogo wamekosa nini ?
Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu
Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu

Hayo ni maneno ya Hayati Marijani Rajabu kwenye wimbo wake unaitwa UKATILI NI UNYAMA

ukatili ni unyama , serikali ya CCM, imefanya unyama kamwe hatutawasahau
 
Regge za bob malley zimeanza, machalii wanasisimka, nadhani huko ndani mambo yanakaribia kuiva
 
Back
Top Bottom