Yaliyojili MBARALI: Mabango ya VODACOM yang'olewa, RC-Mbeya aamuru yarudishwe haraka. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyojili MBARALI: Mabango ya VODACOM yang'olewa, RC-Mbeya aamuru yarudishwe haraka.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by wwww, Apr 29, 2012.

 1. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  WanaJF jmosi jana ya tarehe 28.04.2012 nikiwa kwetu Ubaruku kwa ajili ya mapumziko mafupi nilisikia tetesi kuwa katika mji wa RUJEWA ambao ni makao makuu ya Wilaya yetu ya Mbarali kuna mshikemshike baada ya Mabango ya VODACOM yaliyotundikwa kwa ajili ya kutangaza biashara zao hasa MPESA kung'olewa kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kutolipiwa ushuru.

  Ndugu zangu ilibidi nisafiri kutoka Ubaruku kwenda Rujewa yapata km 4 na nauli ni Tshs. 1,000.00. Nilipofiki Rujewa nikamtafuta rafiki yangu wa siku nyingi anayeishi Rujewa na ni Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ili anipe mkanda kamili kwa kilichojiri.

  Yule bwana alinipasulia jibu, akiniambia ''hawa VODACOM wamezoea, wamefanya Wilaya hii kama shamba la bibi ambapo wanaweza kuweka matangazo yao bila kulipia kwavile tu wanakingiwa kifua na Wanasiasa na Watendaji Serikalini''. Akaniambia ukitaka habari kamili nenda kwa Wakala wa VODACOM pale stendi ya Rujewa akanitajia jina.

  Nikaondoka hadi pale kwa Wakala, ambaye hakutaka kunitajia jina lake kwavile yeye sio msemaji wa VODACOM. Huyu bwana alinieleza kuwa ni kweli kama unavyoona hakuna bango lolote la VODACOM hapa stendi, Mjini (akinimaanisha hatua chache kutoka pale stendi)pia eneo la Igawa (Mji mdogo ambao uko barabarani kutoka Mbeya kwenda Dar-es-Salaam).

  Aliendelea kunisimulia kuwa ''niliwaona vijana wakiondoa mabango hayo na nilipowauliza nani kawatuma kufanya hivyo kiongozi wao aliniambia ni Ndg. Afrika(Mhasibu wa Mamlaka ya Mji Mdogo Rujewa)''. Niliomba namba ya simu ya Bwana Afrika yule kiongozi wao akanipa lakini akaniambia simu yake kwa sasa haipatikani kwasababu ya kukosekana kwa umeme. Nilipompigia majira ya mchana siku ya Ijumaa tarehe 27.04.2012 akaniambia yeye sio msemaji wa Mamlaka, ameamuliwa na Afisa Mtendaji wa Mamlaka kuyaondoa kwavile hawajalipa ushuru wa mabango, kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa Mtendaji wa Mamlaka.

  Wakala yule akaniambia ''Mimi ni msimamizi tu wa haya mabango, hivyo ilibidi nitoe taarifa kwa VODACOM mkoani Mbeya, Meneja akaniomba namba ya Afisa Mtendaji aliyejulikana kwa jina moja tu la Mkemwa, sikuweza kuipata, hivyo nikampatia namba ya Afrika. Hivyo kilichoendelea sijui, lakini mabango yote yametolewa.

  RC - MBEYA (Abbass Kandoro) aingilia kati.
  Inaelezwa kuwa Meneja wa VODACOM alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Mbeya asaidia jahazi ili mabango yarudishiwe mahali pake. Naambiwa Mkuu wa Mkoa alimpigia simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Aswege Kaminyoge ahakikishe mabango yanarudiswa mahali pake kwa gharama ya Mamlaka ya Mji Mdogo Rujewa. Taarifa inaendelea kusema Mkurugenzi akaamuru mabango yarudishwe haraka kwani amepewa amri na mkubwa.

  Hata hivyo mpaka naondoka pale Rujewa mabango ya VODACOM hayakuwa yamerudishiwa. Inasemekana Watumishi wa Mamlaka wameungana kutoyarudisha mabango hayo mpaka VODACOM watakapolipa ushuru stahiki na wako tayari kwa lolote kutoka kwa Mkurugenzi na Mkuu wa Mkoa.

  Mtumishi mmoja ambaye hakutaka kunitajia jina lake alisema, '' Tabu ya nchi hii siasa ni kila kona hata kwenye masuala ya kisheria''. Anasema kabla ya huyu bwana (Afrika) kuhamishiwa hapa, kutokea Halmashauri ya Wilaya tulikuwa na hali mbaya sana, tulikuwa kama wafungwa, hatukuwa na hadhi ya utumishi kwa vile hatukuwa na fedha hata kidogo kwa vile vyanzo vingi vilivyokuwepo havikuweza kuibuliwa. Anasema alipofika alianza kwa kuibua vyanzo vya mapato na sasa ninavyokuambia Mamlaka ina pesa za kutosa kuendesha shughuli za kila siku, sasa tayari wakubwa wameanza kumkatisha tamaa kwa kumtisha.

  Mtumishi huyu anasema Kandoro kama ana hisa VODACOM atulipe yeye ushuru wetu wa mabango, la sivyo hatukubaliani naye hata kidogo. Ni yeye anayesababisha Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali isitusaidie kwa lolote kifedha Mamlaka ya Mji Mdogo Rujewa ili kuendesha shughuli zetu za kila siku, sasa anataka sisi tuishije? Tunafanya kazi katika mazingira magumu sana kwani Halmashauri haitoi hata senti kwetu, sasa huyu bwana amejitahidi kuvumbua vyanzo vya mapato wanasiasa wameshaanza kumziba mdomo.

  Mtumishi huyu anaendelea kwa kusema ''hatukatai kutii amri ya Mkuu wa Mkoa, lakini atuambia pesa zetu tutazipataje kutoka VODACOM ikiwa ni miezi miwili tangu tuwatake watulipe kupitia ajenti wao SYSCORP MEDIA LTD ya Dar-es-Salaam hatujalipwa?

  Wanajamvi haya ndiyo yanayofukuta huku Rujewa Mbeya, na inasemekana huyu ndg. Mkemwa na Afrika wapo hatarini either kupoteza kazi au kuhamishwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa.

  Serikali inasema haina pesa vijana wakiibua vyanzo wakubwa wanawakaba koo sijui kama tutafika au ndio kuendelea kuombaomba kwa wazungu.................................?

   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Wezi wakubwa
   
 3. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ni baadhi ya makampuni yanayofanya kazi kisirisiri kama waganga wa kienyeji na hata wabunge wameliona hilo. mkuu wa mkoa angewaambia halmashauri atalishughulikiaje hilo ili halmashauri ipate haki yake toka vodacom. Kama taifa inapata hiyo hela wangezieleza halmashauri mgao toka taifa hadi chini unakuwaje kuondoa fujo itakayoweza jitokeza kila halmashauri ambako hawa jamaa na wengine wana matangazo ya aina hiyo
   
 4. N

  Ndole JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 352
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama ni kweli basi Kandoro atakuwa na matatizo ya ubongo.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kama mkuu wa mkoa ana risiti za malipo ya hayo mabango toka Vodacom aziweke hadharani, vinginevyo alitakiwa amfikishe mahakamani kesho asubuhi meneja wa vodacom mkoa wa Mbeya kwa kuikosesha Halmashauri mapato.
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi Abbas Kandoro bado hajajifunza na lile saga la Mbeya Mjini. Aache kuingilia mambo kwa kuwa yeye ana mamlaka fulani. Atumie misingi ya sheria, utu na haki katika kuhakikisha mambo yamekwenda vizuri.
   
 7. E

  Ernest Da Vinci Senior Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapo sio kandoro wpo wengne nyuma yke,hyo bwana ni kama shield tu,ila no longer at easy!!!
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  kazi ni kwao.
   
 9. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ewe mleta mada ni "yaliyojiri" sio "yaliyojili". Jifunze Kiswahili ni lugha ya Taifa.
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Ficha upumbavu wako we kicheche!!
   
 11. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Kama wewe ni mahiri wa kiswahili, mbona hatujaona kamusi lako? Mtu hakatazwi kukosea!
   
 12. wwww

  wwww JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 350
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 60
  Nashukuru kwa hilo, lakini kiswahili ni kigumu sana. Hata hivyo nitaendelea kuwaletea kitakachojiri hapo kesho kwani inasemekana Meneja wa VODACOM Kanda ya Mbeya atakuwa Ofisi za Mamlaka ya Mji Mdogo Rujewa.
   
 13. b

  buswe Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Naomba wabunge wapeleke bungeni haraka mapendekezo ya kurekebisha sheria inayosimamia wakuu wa mikoa na wilaya. Baada ya kanzishwa mfumo wa vyama vingi ilitakiwa wakuu wa mikoa na wilaya wawe watumishi wa kawaida wa serikali kama walivyo katibu tawala wa mkoa na wilaya. Nashangaa tuaendelea kuwa na wakuu wa wilaya ambao ni makada wa chama mpaka sasa. wakuu wa mikoa na wilaya wanahudumia wananchi wa vyama vyote, hivyo hawatakiwi kuwa makada wa chama chochote. RAS na DAS wapewe majumu ya ma-RC na ma-DC.
   
 14. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  ulevi wa madaraka. Dawa yake ni wananchi kuamka.
   
 15. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Nasubiri TRA watakapo pambana nao !
   
 16. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kandoro ni muumini mkubwa wa ufisadi. Anastahili kunyongwa 2015.
   
 17. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  VODACOM inaongoza tanzania kwa kutolipa kodi!hata songas hawalipi kodi kule lindi eti wanalipa ilala mahali HQ yao ipo
   
 18. Eliza wa Tegeta

  Eliza wa Tegeta JF-Expert Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM wana share VodaCom
  Hapo unategemea nini
  Kandoro hakutoa amri kienyeji.

  Hao ndio CCM, mabango yaliyowekwa kinyume na taratibu wakati wa kampeni, yakimnadi kikwete yalibadilishwa na kuwa Voda siku ya mwisho ya kampeni.
  Wahuni hawa!! Wezi na mafedhuli
   
 19. M

  Mbuyi Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 13
  Naona anatajwa Mkuu wa mkoa wakati hapo kuna Mkuu wa Wilaya, Enhee tena mwanajeshi fulani amabye hana chama, yeye anawekwa wapi katika hili?
   
 20. N

  NnyaMbwate JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,398
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Rostam Aziz ni mmoja wa wanahisa wa VODACOM! Tafakari, Chukua Hatua!!
   
Loading...