Yaliyojili jioni hii mahakamani kati ya Mnyika vs Hawa Ngh'umbi

hizo pesa zinazotumika kuendeshea kesi km hii ambayo haiitaji uwe mtaalam wa mambo ya sheria kujua kuwa ni upuuzi ni BORA MARA MIA ZINGETUMIKA KUGHARAMIA MAFUNZO YA PANYA WATEGUAO MABOMU LABDA TAIFA LINGEPATA FAIDA.HIZI NI DALILI ZA KIFO!!!
 
Hii kesi haina kichwa, inatupotezea muda kuifatilia. Hongera Mhe. Mnyika kwa umakini ulionao.
 
Duuuuh hawa Ng'umbi aibu hii utaificha wapi ndugu yangu!!!!!!!


Ona sera za CCM!!!!!!!!!
Nipigeeeeeeee Nisipigeeeeeeee????????????????????
Pigaaaaaaaaaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota rangi ganiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?????????????
Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa Chama cha Mapinduzi.
CCM Oyeeeeeeeee.
Oyeeeeeeeeee.

us.enge tu
 
Magamba wana matatizo kweli?wanachimbua chimbua tu visivyochimbuka na kupoteza resources ambazo zingekuwa injected kwenye productive areas,sasa hapo kesi iko api?
 
Duuuuh hawa Ng'umbi aibu hii utaificha wapi ndugu yangu!!!!!!!


Ona sera za CCM!!!!!!!!!
Nipigeeeeeeee Nisipigeeeeeeee????????????????????
Pigaaaaaaaaaaaa
Bendera ya CCM ina rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mahindi yanaota rangi ganiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiii.
Ukipanda mpunga unaota rangi ganiiiiiiiiiiiiii???????????
Kijaniiiiiiiiiiiiiiii
Migomba yote ina rangi ganiiiiiiiiiii?????????????
Kijaniiiiiiiii.
Piga makofi na vigelegele kwa Chama cha Mapinduzi.
CCM Oyeeeeeeeee.
Oyeeeeeeeeee.

Haaa haaaaa haaaaa magamba wanatia aibu
 
Heshima kwako Lau,

Mkuu nimependa ulivyowasilisha mtiririko wa kesi,naomba wengine wanaoleta thread kuhusiana na kesi za uchaguzi waige mfano wa Lau.
 
Mbunge wa ubungo john mnyika amemuudhi Jaji upendo Msuya wa mahakama kuu kanda ya Dar es salaam kiasi cha kumtaka wakili wake amuonyeshe kile Jaji huyo alichosema ni sawa na kudharau mahakama. Jaji Msuya alieleza kuudhiwa na mbunge huyo jinsi alivyokuwa akijibu maswali mbalimbali ya wakili wa mlalamikaji, Issa Maige, wakati akijitetea katika kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi. kesi lilifunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge kupitia CCM Hawa ng'umbi. Jana Mnyika alipanda kizimbani kujitetea huku akikana madai yote na kudai kuwa, hata kasoro zinazolalamikiwa hazikuathiri matokeo, lakini alipobanwa kwa maswali na wakili Maige alifika mahali akamuudhi Jaji Msuya anayesikiliza kesi hiyo. Mambo yanayodaiwa kumuudhi jaji msuya ni jinsi mnyika alivyokuwa akijibu maswali hayo, wakati mwingine alikuwa akijibu kinyume na swali na wakati mwingine kutoa maelezo marefu ambayo yalikuwa hayahitajiki. kutokana na hali hiyo jaji msuya ilibidi aingilie kati mara kwa mara akimtaka mnyika ajibu swali kwa kadri alivyokuwa akiulizwa, badala ya kutoa maelezo ambayo hayakuwa yakihitajika hata hivyo Mnyika aliendelea kupiga chenga. Hali hiyo ilimuudhi Jaji msuya na wakili wake, Edson mbogolo alisimama na kumnong'oneza mnyika mambo kadhaa "Nafikiri wakili ni vyema pia umemwelewesha kuwa majibu mengine anayojibu si sawa, na hii inaweza kutafsiriwa kuwa ni dharau kwa mahakama maana nimeisha muonya na kumuonya lakini bado tu". Baada ya onyo hilo Mnyika alionekana kutulia na kujibu maswali kadhaa ya wakili Maige kwa utulivu na kwa kadri swali lilivyokuwa likiulizwa. katika hatua nyingine, Mnyika alipingana na aliyekuwa msimamizi Msaidizi wa uchaguzi , Gaudence kadiarara , kuhusu madai ya matumizi ya komputa zake (Mnyika) kuhesabia kura Majibu ya swali hilo ni miöngöni mwa majibu yaliyoonesha kumuudhi jaji Msuya kwa jinsi Mnyika alivyokuwa akijibu. Wakili Maige: kwa hiyo DW1 ni muongo? Mnyika: nimesema maelezo yake siyo ya kweli, Wakili Maige: sawa siyo sahihi kwa hiyo ni Muongo, kweli au sikweli? Mnyika: nimesema maelezo yake siyo ya kweli. katika kujibu maswali ya wakili Maige, Mnyika alikiri kuwapo na dosari katika matokeo yaliyorekodiwa katika fomu ya matokeo ya jumla na kwamba, kwa jinsi yalivyorekodiwa siyo sahihi wala halali. Pia, alikubali kuwa kama angeyabaini mapema asingesaini mpaka yangerekebishwa huku akikiri pia kuwa katika hali hiyo mwenye mamlaka ya kurekebisha dosari hizo kwa sasa ni Mahakama. Mnyika pia alikiri alikiri tofauti ya kura zaidi ya 14000 inayoonekana katika fomu hiyo yeye binafsi hawezi kuielezea. Lakini katika awali katika ushahidi wake wakati akiongozwa na wakili wake, Mbogolo, Mnyika alidai kuwa dosari hizo haziathiri matokeo hayo na kwamba, hata kama ikithibitika kuwa tofauti ya kura hizo ni za ng'umbi , bado hawezi kushinda. nukuu Mwanainchi 31.3.2012
 

Wakili J: Imeelezwa kulikuwa na mabadiliko na matumizi ya laptop

Mnyika: Kiukweli kulikua na mabadiliko. Tulipoanza 01/11/2010 Fomu zilikuwa zinaingizwa katika kifaa maalumu scanner kasha kisha yanaingizwa katika system maalum "results management system" Zoezi lilipoanza saa tano asu mpaka saa 2usiku fomu chache ziliingizwa.

Wakili J: Unaweza kukumbuka idadi?

Mnyika: Sikumbuki exactly lakini kati ya 200 na 400. Hazijadizi 400 wala kupungua 200. Tukawaambia Tume, kwani katika kifugnu cha maadili wagombea wanaweza kutoa ushirikiano wakiona mambo hayaendi sawa. Pia kuna kifungu tume inatakiwa itangaze matokeo mapema. Alikuwepo mgombea wa AFP, NCCR. Ushauri tuliotoa, nakumbuka mimi binafsi nilitoa. Msimamizi hakuwepo, nikasema naomba wamuite Msimamizi mwenyewe aje aone na kutoa ushauri. Wasimamizi wasaidizi wakaniahidi kuwasiliana nae ili kujua cha kufanya. Huku zoezi la kuongeza yaani kujumlisha likiwa linaendelea.

Jaji: Hivyo taarifa walipelekewa

Mnyika: Sijui kwa njia gani ila natambua baadae bwana Gaudance alitoka na kuja na laptops

Mheshimiwa Jaji.Jaji: Alitoa ushahidi namba 2?

Mnyika: Ndiyo, shahidi wa kwanza upande wa walalamikiwa alikuja na laptops.

Jaji: Ngapi?

Mnyika: Laptop 4, akapanga pembeni mwa laptop iliyokuwapo zikiwa tano.Wakatuambia waliwasiliana na Msimamizi na anakuja pamoka na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Bwana Kiravu. Na tuendelee na zoezi tulilokuwa tunaendelea nalo mpaka wao watakapo fika. Msimamizi alifika na Mkurugenzi, Bwana Kiravu sikumbuki muda ilikuwa around saa tano. Walifika wakazungumza kisha wakatufata kujua hapa kuna tatizo gani. Tukawaambia zoezi la kuingizwa kura taratibu wakasema wameshauriana watumie mfumo wa kawaida wa spreadsheet na watumie laptops zilizoletwa. Wakala wangu Bwana Eric Ongara akauliza tutaziamini vipi? Zimeletwa baadae. Bwana Kiravu akasema yeye anatimu ya wataalamu wa IT, watahakiki ili zitumike wakamtaja Dr.Sixtus . Kulikuwa na movement nyingi za wataalamu wa Tume. Sisi pamoja na hatukuakiki, tulikubali zitumike kwa sababu mbili; 1. Mfumo utakao tumika wa kawaida wa spread sheet 2. Namba za matokeo ni zile zile toka vituoni.Tukakubali, lakini sisi nasi tutakwa tunalinganisha kura kwa kuingiza nasi matokeo toka vituoni kama kuna tofauti tutazisema. Wakarejea, wakaanza nasi tukiwa na laptop zetu, mawakala wengine na laptop zao.

Wakili J: Vyama 16; ndani kulikuwa na mawakala wangapi?

Mnyika: Lini? Tarehe 31 au 01 usiku?

Wakili J: Mchakato mzimaMnyika: Wakala wa CHAUSTA, AFP, wakala wa CHADEMA, NCCR Mageuzi Bwana Kazi moto, na wakala wa CUF.

Wakili J: Henry Kishato aliyetoa ushahidi wake sijasikia ukimtaja.

Mnyika: Sijamtaja kwa sababu simfahamu. Katika hizi taratibu zote hakuwepo. Ilipofika nmida ya saa 3 usiku alikuja mtu katika sehemu tuliyokaaJaji: Lini? Tarehe ngapi?

Mnyika: 01/11/2010 saa 3 usiku Mheshimiwa Jaji wakati tunajumlisha kwa system nyingine. Akaja mahala tulipokuwa tumekaa. Anannuka pombe. Ile hali aliyokuwa nayo, watu wakamuuliza ni nani? Akaenda kwa msimamizi kujitambulisha tukasema tutakuwa na uhakika gani? Ana nakala ya kiapo au barua? Uende Msimamizi akikubali aje kutambulisha kwetu. Baada ya hapo akaondoka. Sijamwona tena, na sikumbuki kumuona tena.

Jaji: alipoondoka je alishiriki katika majumuisho au hakushiriki?

Mnyika: Hakushiriki

Wakili J: Huyu anayesema alikuja na wafuasi zaidi ya nane?

Mnyika: Nilifika mara mbili. Mara ya kwanza siku ya 31/10/2010 baadae siku ya tarehe 01/11/2010. Na baada ya hapo sikuondoka. Aliyetoa ushahidi mimi amenikuta. Angewezaje kuniona. Sijaeleza. Na maelezo yangu yapo katika kumbulumbu za mahakama yako tukufu Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: unaweza kuzungumzia juu ya kutajwa wafuasi hao?

Mnyika: alitaja kwa majina; Boniface ambaye ni Diwani kata ya Ubungo, Pamba ambaye ni diwani kata ya sinza, ,Mallya na Nassoro alionyesha kwa kunyoosha kidole. Alipohojiwa ataje wengine zaidi alishindwa na alitaja tu Bwana Eric ambaye anakiri alistahili kuwepo. Wengine alishindwa.

Wakili J: Kulikuwa na ushahidi gani juu ya kuruhusiwa kuingia au kutoingia?

Mnyika: Nilipata bahati ya kuingia na kutoka. Kisha kuingia tena. Nilichokiona Loyola. Polisi wengi wenye uniform na silaha. Kulikuwa na polisi wengi nje, na wenye diffender na silaha. Kulikuwa na polisi wengine nje ya chumba cha kujumlishia. Kila safu ilikuwa na silaha. Ndani ya ukumbi wenyewe kwa uzoefu wangu katika kushiriki chaguzi, Loyola ilikuwa exceptional. Kwani ndani ya ukumbi kulikuwa na askari wenye uniform wasiopungua watano. Kati ya saa moja na tatu; ilikuja group nyingine ikiongozwa na RPC Kalinga hawa walilinda usalama ndani.

Jaji: RPC wapi?

Mnyika: Kanda maalumu DSM, lakini mkoa wa Kinondoni. Nami nilimlalamikia kwanini kuna askari wengi sana barabarani, nje ya mlango na ndani. Iingie katika kumbukumbu zako Mheshimiwa Jaji kwani mwaka 2005 katika kituo cha majumuisho, kulikuwa na askari wanalinda ndani na nje. Tuliambiwa na Msimamizi tukapumzike. Tuliporudi, tulikuta magari ya askari yaliongezeka mengi sana na magari ya maji ya kuwasha kisha wakatangaza matokeo. Nilipoona nikamuuliza nini wanataka kufanya sasa usiku; akaniambia usiwe na wasiwasi, tumekuja kuimarisha ulinzi. Niliikubali kauli ile kwa shingo upande.

Wakili J: Juu ya kuzongwa zongwa kwa Msimamizi wa Uchaguzi?

Mnyika: Madai si kweli. Ingekuwa ajabu polisi hadi RPC kuwepo na kuona Mkurugenzi anazongwa zongwa bila wao kuchukua hatua yoyote. Naomba niihakikishie mahakama yako tukufu Mheshimiwa Jaji kulikuwa na ulinzi wa kutosha.

Wakili J: Unaweza kuzielezea hizo nyakati au awamu na yaliyojiri?

Mnyika: Awamu tatu. Mosi, saa 12 jioni mpaka saa mbili usiku zoezi lilikuwa taratibu sana. Tulikuwa kama mawakala tunamwita kuuliza zoezi litaisha lini au sisi tuna tutuma mwakilishi wetu anaenda kuuliza kisha anashuka chini. Awamu ya pili; Mkurugenzi na Kirabu tulishauriana na kutueleza wameamua kutumia excel spread sheet. Na baada ya zoezi hilo la kutumia hiyo excel, zoezi lilienda haraka. Labda maswali ya kawaida fomu gani mmesoma namba tofauti na sisi tuliyokuwa nayo, kwa ujumla kusahihishana.

Wakili J: Hapo hali utasemaje?

Mnyika: Mambo yalikuwa shwari bila wanajibizana.

Wakili J: Fomu angalia unaweza ukaelezeaje?

Mnyika: Fomu za matokeo

Wakili J: Unaweza taja vituo vilivyopo?

Mnyika: 1. Tumaini Nursery namba 3 2. Malaika Nursery 3. St. Peter A5 (P-2) 4. Urafiki B 2 5. St. Peter A 1

Wakili J: Unafahamu lalamiko?

Mnyika: Analalamika idadi halisi ya waliopiga kura na idadi halali ya kura. Kwa maelezo mengine, idadi ya kura zenye mgogoro hazijajazwa.

Wakili J:Unaiambia nini mahakama?Mnyika: Baada ya kusikia lalamiko, nimetazama fomu. Nikiangalia nakala.

Jaji: Ni copy au?

Mnyika: photocopy na si duplicate

Mnyika: Kwa kila kituo nikiangalia St.Peters A1 kuna kura 3 za malalamiko exhibiti P-2,idadi halisi ya waliopiga kura ni 153, idadi ya kura halali 150. Tofauti ni kura 3. Exhibit P-3; maelezo waliyotoa kituo hiki kina kura 166 na si 160 katika idadi halisi ya waliopiga kura. Tukichukua walichosema mahakamani idadi ya kura 160; kuna tofauti ya kura 6.Exhibit P.4; idadi halisi ya waliopiga kura 133; idadi ya kura halali 131. Tofauti kura 2Exhibit P.5; idadi halisi ya waliopiga kura 147, idadi ya kura halali 144. Kuna tofauti ya kura 3. Kituo kinbgine;Exhibit P.6; idadi halisi ya waliopiga kura 148, kura halali 147. Tofauti kura 1.Ukijumlisha tofauti P.2 hadi P.6; kura zenye mgogoro zipo 15. Iingie katika kumbukumbu zako Mheshimiwa Jaji tofauti kati yangu na mlalamikaji ilitangazwa kushinda zaidi ya kura elfu 16. Hata kama ingethibitika bila shaka, hizi kura ni zake angepata kura 15 nyongeza. Jambo ambalo lingefanya tofauti bado kwa kura elfu 16. Kutokana na vielelezo walivyoleta nikaenda mbele zaidi, nikafikiria yasiyo fikirika in worst case scenario. Hii idadi halisi ya kura wote wangempigia yeye katika kituo hiki; nikajumlisha exhibit P.6 (Kura 148)+ P.5 (kura 147) + P.4 (kura 133)+ P.3 (156)+P.2(153)= Kama utaniruhusu kurejea kwangu hakuzidi kwa kura 100. Hata kama nikipata sifuri (0). Hivyo haikuzidi kura elfu16. Hiyvo madai yake na hivi vielelezo haviwezi kukidhi haja ya kufuta matokeo. Hayana athari kwa matokeo.

Jaji: Unachotaka kusema ni nini?

Mnyika: Hata kama kura zote za vituo hivyo ziwe zake bado asingekuwa mshindi Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Alisema wyalifanyika wapi marekebisho?Mnyika: Katika chumba cha majumuisho Mheshimiwa Jaji

Wakili J: Unaiambia nini mahakama?

Mnyika: Nilikuwapo katika majumuisho. Hakukuwa na marekebisho. Naelewa utaratibu masuala ya vituo yana malizikia vituoni.

Wakili J: Hoja yao nakala walikuwa nayo wao ni 166 na sio 160Mnyika: Nakala waliyotuletea ni photocopy na si copy (duplicate). Siwezi kuthibitisha jambo lolote katika photocopy. Nimezunguma hayo kutonana na nakala ile halisi na si copy of the copy. Siwezi kuthibitisha chochote juu ya copy of the copy.

Wakili J: Exhibit P.1 angalia

Mnyika: Exhibit P.1 fomu 24 (b); "Matokeo ya uchaguzi wa bunge katika jimbo"

Wakili J: Umetambua kuwa ni matokeo ya jimbo gani?

Mnyika: Natambua kwani imeandikwa hivyo. Natambua katika jina langu, Mnyika John John, (ME) imeandikwa kura zangu 66,742 na imewekwa alama ya vema chini ya sehemu imewekwa mgombea aliyeshinda imetiwa saini na wakala wangu Eric Ongara. Nakiri ni fomu nakala aliyosema ni fomu halisi.

Wakili J: Upande wa mlalamikaji fomu inasomekaje?Mnyika: Mgombea namba 3; 50,544 kura alizopata Hawa Mgonja Nghumbi. Jina la wakala wake halijajazwa, sahihi ya wakala au mgombea haijajazwa kitu.

Wakili: Mlalamikaji analalamikia nini?

Mnyika: Kwa mujibu wa hati; ana lalamikia matokeo si sahihi na ibabidi yabatilishwe kwa ushahidi hapa mahakamanai ameonyesha utofauti wa kura na wapiga kura. Amesema; 117,639 kura halali inatofautiana na idadi ya kura halali ukijumlisha kila mhombea inakuwa kura elfu 13 na ushee kuna utofauti wa takribani kura elfu 12.

Wakili J: unataka kurejea kumbukumbu?

Mnyika: Naomba nirejee katika kumbukumbu Mheshimiwa JajiJaji: wakili Maige una tatizo lolote akirejea kumbukumbu?

Wakili H: Kama anarejea katika P.1 sina tatizoJaji: Jumlisha copy ya P.1

Mnyika: 132,396 jumla za kura ambazo wagombea wamepata. Naomba kwa ruhusa yako nitoe kura halali (117,639). Katika fomu P.1 tofauti; 14,757.Naomba kura zangu nitoe na alizopata mlalamikaji; 66,742-50,544 = 16,198 kuraNaomba nitoe tofauti ya kura; 16,198-14,757= 1441 kuraNaomba wakili aendelee.

Jaji: Kabla hizo hesabu sasa unataka kusemaje? Hitimisho lako?

Wakili: ulikuwa unataka kusemaje?

Mnyika: Hiyo tofauti inayoelezwa haina athari kwa matokeo ya ushindi wa kura. Kwanza; fomu sehemu yaJaji: Hayana athari. Hayo mengine si lazima

Wakili J: Hizi kura zilitoka wapi?

Mnyika: Hizi kura 66,742 ambazo mimi nimezipata zimetokana na kujumlisha kuea zilizotangazwa katika vituo kwa kuangalia na kupitia fomu zilizotoka kituoni za matokeo na kura za mlalamikaji 50,544 zimetokana pia na karatasi toka vituoni hizo hizo. Hivyo ni matokeo halisi

.Wakili J: Karatasi ina kolamu ngapi?

Mnyika: tatu; moja jimbo la uchaguzi.Ya pili nambaJaji: Eleza jibu swali la wakili

Wakili J: toa maelezo ya hizo rowsMnyika: Eneo la 1; Jimbo la Uchaguzi 2; Matokeo ya uchaguzi kwa kila mgombea; a. Jina la mgombea b. Jinsia c. Chama d. Mgombea yupi kashinda e. Jina la wakala f. Sahihi 3; Taarifa za kupiga kura; a. idadi ya wapigaji kura iliyoandikwaJaji: Tunazungumzia kuhusu rows au kolamu?

Mnyika: Nilisema row mheshimiwa Jaji na si kolamu

Jaji: Ndicho hicho? Kolamu au row?

Wakili J: Row!Jaji: Kuna rows ngapi?

Mnyika: tatu. 1[SUP]st[/SUP] row: Jimbo la Uchaguzi; - Ubungo
- Halmashauri manispaa: Kinondoni- Namba ya Jimbo: 0070103- Mkoa: DAR ES SALAAM2[SUP]nd[/SUP] row: Jina la mgombea, jinsia, jina la chama, kura alizopata, mgombea aliyeshinda, maelezo weka alama ya vema. Alama hiyo imewekwa katika jina langu; jina la wakala/mjumbe na sahihi3[SUP]rd[/SUP] row: Idadi ya wapiga kura walioandikishwa, idadi halisi ya waliopiga kura, idadi ya kura halali, idadi ya kura zilizokataliwa. Hii inaweka takwimu za wapiga kura. Sehemu ya mwisho (4); uthibitisho sections=sehemu.Jaji: sio row tatu?

Mnyika: ni tatu Mheshimiwa Jaji; ya mwisho ni sehemu yaani section

Wakili J: Row ya matokeo ina mapungufu gani?

Mnyika: 2[SUP]nd[/SUP] row ya matokeo haina mapungufu yoyoteWakili J: Bali?Mnyika: Row yenye takwimu za wapiga kura

Wakili J: unaimabia nini mahakama?

Mnyika: Ningeomba mahakama yako tukufu izingatie matokeo yaliyotangazwa kutokana na row ya pili. Yaliyoeleza; mimi Mnyika John John toka CHADEMA nimepata kura 66,742 na katika row hii ya matokeo nimepewa alama ya vema kama mgombea aliyeshinda wakati mlalamikaji; Hawa Mgonja Nghumbi amepata kura 50,544Wakili J: Shahidi namba 3 aliomba fomu ya malalamiko hakupewa unaelezeaje hilo?

Mnyika: ninachokumbuka kwenye saa tatuWakili J: Usiende kwenye detailsMnyika: Wakati matokeo yanatangazwa sikuona wakala wa CCM, wala kumuona mtu analalamika, ndani ya chumba cha majumuisho hakukutokea jambo hili Mheshimiwa Jaji.

Wakili J: Kuhusu upungufu wa vifaa una lolote la kuiambia mahakama?

Mnyika: Kadiri ya kitabu cha maelekezo cha Tume, kadiri aidha chumba cha kupigia kura au majumuisho una hakiki vifaa kabla

Wakili J: Je mli hakiki?

Mnyika: Ndiyo, tulifanya tukajiridhisha.Jaji: Uhakiki ulifanyika saa ngapi?

Mnyika: Saa moja asubuhi 01/11/2010 kwani awali tulitaka usiku tuhakiki wakasema ni vyema tusubiri asubuhi kila kitu kitakapo fika. Naomba nieleze pia kabla ya majumuisho Msimamizi alitueleza hawajapata malalamiko au kasoro toka vituo, 01/11/2010 asu sisi tuliwaambia vifaa na fomu zimechelewa kukusanywa tulitarajia tuanze majumuisho 31/10/2010 Mawakala wengine na vyama vyao nao hawakuwa na malalamiko. Ndipo tukaendelea na zoezi.

Wakili J: Unaiambia mahakama nini kuhusu haya yote?

Mnyika Mahakama tukufu isizingatie madai na malalamiko. Izingatie matokeo ya kura. Na itupilie mbali kwa gharama.Jaji: Ulipoingia katika chumba cha majumuisho kulikuwa na taratibu gani?

Mnyika: Kadiri ya 31/10/2010 usiku mimi sikuulizwa kitambulisho chochote. Ila wakala wangu aliulizwa barua ya utambulisho ambayo aliitoa. Sisi tulianza kufika. Baadhi ya mawakala walifata kuna niliona wakiulizwa barua ya utambulishoJaji: Je kulikuwa na identity cards? Beji?

Mnyika: waliokuwa na beji walikuwa waangalizi wa uchaguzi. Wasimamizi wa Tume walikuwa na T-shirts za Tume nyeupe. Askari walikuwa na sare zao.

Wakili J: Nashukuru Mheshimiwa Jaji.

Wakili G: uliongelea ukaaji juu na chini, na ukaaji. Unaweza kueleza distance?

Mnyika: Tuki assume hiki ndicho chumba ambapo huo ni ukumbi wa shule Loyola. Juu katika steji kulikuwa na maafisa wa tume huku chini kulikuwa na mawakala na wagombea. Baada ya system ya tume

Jaji: Maafisa walikuwa katika steji?

Mnyika: wagonbea, mawakala, waangalizi walikuwa wamekaa upande wa chini wa stageJaji: Hivyo ndivyo mlikuwa mmekaa kabla ya zoezi kubadilika?

Mnyika: Ndiyo Mheshimiwa Jaji. Baada tukatakiwa kusogea karibu na stage, kwa kuwa hatukuwa tunatumia vipaza sauti ili kuweza kusikia na kufatilia ili tulinganishe vizuri taarifa.


Wakili G: Je kulikuwa na uingiliano wowote wa watu na Tume?

Mnyika: Baada ya ule wa awali na kina Kiravu hakukuwa na mwingiliano wowote mwingine Mheshimiwa Jaji.

Wakili G: Mlijiridhishaje kila kilichosemwa ni sahihi?

Mnyika: Kwanza; tulikuwa tuna sikiliza fomu za matokeo kama ni sahihi. Pili; tunaingiza katika fomu zetu ili kuendelea kupata jumla na Tatu; baada ya wao kujumlisha na kusema tarakimu zao. Kutokana na laptop central na tukalinganisha na sisi tulichokipata, wakaenda katika hatua ya kujaza fomu 24 (b) ambayo ni exhibit P.1, walipoijaza wakaita mawakala na wagombea. Tukaenda mbele tukaizunguka fomu, tukatakiwa kuiangalia, kuhakiki kwamba tulichotamkiwa ndicho kilichoandikwa.

Wakili G: Katika ngazi hiyo kuna malalamiko?

Mnyika: Hakukuwa na malalamikoWakili G: Nashukuru mheshimiwa Jaji.

Wakili H: unataka mahakama iamini fomu ni sahihi?Mnyika: Nimesema iamini rowas nilizotaja ni sahihi.


Wakili H: Unazungumzia fomu P.1 yenye sahihi mahakama iamini ni sahihi?Mnyika: Mheshimiwa Jaji Nilisema kwa ujumla iaminiwe ni sahihi ilijazwa katika chumba cha majumuisho. Si ya kughushi. Pili matokeo ya wagombea ni sahihi.

Wakili H: Kura za wagombea 16 zilipaswa zioane na idadi gani?

Mnyika: Idadi halali Mheshimiwa Jaji.

Wakili H: ambayo ni ngapi?

Mnyika: 117,639

Wakili H: utakubaliana kura za wagombea 16 zimezidi kura halali?

Mnyika: Kura halali ziliandikwa 117,639 kura halali kwa mujibu wa wagombea ni
117…….. nilitaja

Jaji: rudia swali ajibu swali

Wakili H: Kura halali zinazidiwa zaidi elfu 14 kama ilivyojazwa hapo?

Mnyika: Kwa zipi?

Wakili H: Hapo

Mnyika: Kwa mujibu wa row ya
pili;…….. na row 3; 117,639 ukilinganisha row kuna tofauti ya kura 14,757

Wakili H: Ukiondoa matokeo yaliyokuwa recorded una kielelezo gani kingine kuthibitisha?

Mnyika: Mheshimiwa Jaji nina vielelezo viwili; kwanza fomu za matokeo. Pili; mleta madai hajaleta kielelezo kura 66,……. Na yeye 50,544. Tena amekiri kuwa hana taarifa na kura zilizopp na idadi ya wapiga kura.

Wakili H: wakati una saini katika exhibit P.1 uligundua idadi au utofauti?

Mnyika: Sijasaini. Amesaini wakala wangu Eric Ongara Mheshimiwa JajiWakili H: Labda niulize hivi; wakati, wakala wako amesaini ulishagundua tofauti zaidi ya kura elfu 14?

Mnyika: Mambo mawili…
Wakili H: Mligundua?

Mnyika: HatukugunduaWakili H: ndiyo, hamkugundua!

Wakili H: Kama mgeona tofauti, mgeendelea kusaini?

Mnyika: Tusingeweka saini. Ni kasoro ndogo za kuweza kurekebishaWakili H: Nani mwenye mamlaka ya kurekebisha?

Mnyika: Kabla ya matokeo?Wakili H: nazungumzia sahivi yameshatangazwaMnyika
: Kama ikiletwa ushahidi bila shaka itabidi iletwe fomu toka vituo kisha….

Wakili H: Umejibu swali, najua unajua vitu vingi nitauliza wakati wake.

Wakili H: Unajua tofauti ya kura elfu 14 zilipotoka?

Mnyika: Nimesikia hoja iliyotolewa. Ni kweli walifanya consultation kwetu. Wakawa watu wanaingiza. Ni kweli walitusomea taarifa hyo.

Wakili H: Jibu

Mnyika: Mheshimiwa Jaji nilinde bado naendelea kutoa maelezo yangu

Wakili H: Unaweza kuthibitisha kura elfu 14?

Mnyika: sina majibu

Wakili H: Unaweza au huwezi?Jaji: Jibu swali

Mnyika: Siwezi

Wakili H: Ieleze mahakama laptop iliyotumika kabla na baada ya abandonment ya ujumlishaji

Mnyika: Kabla kwa kujumlisha matokeo yetu sisi toka katika vituo na kulinganishaJaji: Jibu swali

Mnyika: Nilieleza…..Jaji: Jibu swali

Mnyika: Naomba arudie swali Mheshimiwa Jaji

H: Laptop ilitumika kabla na baada ya zoezi la ujumlishaji?

Mnyika: Tulitumia kuingiza matokeo katika system zamani ikitumika. Na baada ya matokeo kuwa abadon.

Jaji: Matokeo mlikuwa mnayapata wapi?

Mnyika: Tume ilikuwa inataja namba ya fomu na jina la kituo. Sisi tunaingiza ile fomu katika laptop zetu.

Jaji: Fomu gani? 21 (b) toka vituoni? Kwa hiyo mlikuwa mnatumia fomu?Mnyika: Ndiyo, toka vituoni. Kwa upande wa pili Mheshimiwa Jaji tulijumlisha pia nao waliyotusomea matokeo tukawa tunaingiza ili kuyaanisha matokeo hayo.

Wakili H: unasema laptop ya wakala mlikuwa mnaitumia ninyi wawili?

Mnyika: Ndiyo

Wakili H: Ma utaratibu walikuwa wanatumia kurekodi ulikuwa upi?

Mnyika: Walikuwa na laptop nne. Walikuwa wamekaa wawili katika laptop mmoja. Mmoja alisema mwingine anaingiza. Kwa maeneo mengine yenye maafisa watatu; yule wa tatu alikuwa akihakiki. Ila meza ilijaa makarani, watu wao wa IT, wasimamizi na kwa upande wetu tulikaa mawakala na wagombea.

Wakili H: Katika laptop kila laptop ilitumika kujaza fomu 21 (b) tofauti tofauti ndivyo sivyo?

Mnyika: Ndivyo

Wakili H: Kama ndivyo mliwezaje kusikia kila watu wakijaza katika laptop?

Mnyika: Wale watu walikuwa wanajaza kila laptop kufatana na chama moja kwa moja. Ila kwa uharaka ilibidi wawe wanafanya hivyo sawa

Wakili H:Naomba nikuonyeshe exhibit 21 (b). Ndiyo hiyo?

Mnyika: NdiyoWakili H: Hebu eleza uwezekano wa kujaza matokeo ya watu 16 kadiri ya watu

Mnyika: Tulitumia system excel spread sheet unataja majina ya watu, wagombea na vyama. Takwimu ikitajwa inainigzwa namba, jina la mgombea na chama. Napenda Mahakama yako tukufu Mheshimiwa Jaji ifahamu sisi baada ya kupitia matokeo tulishatengeeza systems tatu. Tulikuta tukiondoa CCM, CUF na sisi kura nyingine ni negligible.

Jaji: Hujajibu swali

Wakili H: Mlisikiaje matokeoJaji: wasoma matokeo walikuwa wanasomaje?

Mnyika: walikuwa wanapokezana Mheshimiwa Jaji

Jaji: swali limejibiwa?

Wakili H: Ndiyo. Naomba afafanue Mheshimiwa Jaji

Mnyika: wa CHADEMA alikuwa anasoma ya CHADEMA na wa CCM alikuwa anasoma ya CCM nk. Kisha anatransfer kwa anayefuata. Sisi interest ilikuwa inaposomwa entry ya CHADEMA, CCM na CUF.

Wakili H: Je hamkuwa na matokeo ya vyama vingine?

Mnyika: Tulikuwa na matokeo ya vyama vyote ila sisi baada ya kureview tuliona most occurring ni CCM, CHADEMA na CUF. Hivyo tukawa tunarekodi vyama hivyo. Tulijua kwa kupata matokeo hayo tulijihakikishia tutajua nani mshindi. Tulifanya hivyo kwa sababu speed yetu zaidi ya speed ya watu wanne. Tulijua mapema.

Wakili H: Unataka kuiambia mahakama laptop ya CHADEMA ilikuwa moja?

Mnyika: Ndivyo nilivyoeleza na ndivyo ilivyokuwa

Wakili H: Na CCM walikuwa na moja?

Mnyika: Sijaona ya CCM. CCM alikuja alikuwa kaelwa na kuondoka

Wakili H: Naomba urudie Tume ilikuwa na laptop ngapi kwa CHADEMA?CUF na CCM?Mnyika: CCM-1, CHADEMA-1 na CUF sijui ilikuwaje sababu na vyama vingine vidogo. Ila ukiacha mbili hizo kulikuwa na nyingine mbili kwa vyama vingine.

Wakili H: Katika ukaguzi unakumbuka mlikuta vifaa gani?

Mnyika: a. Fomu 24 (b), scanner 1, fomu namba 16, laptop 2, kulikuwa na series nyingine kama tatu siwezi kurecall namba zake kwa sasa kulikuwa na fomu za matokeo ya mgombea urais ambazo namba zake pia kwa sasa sikumbuki. Interest yetu ilikuwa fomu 24 (b) na 16.Jaji: Fomu 16 inahusu nini? Maana fomu 24 (b) imetajwa sana.

Mnyika: Fomu namba 16 inahusu fomu ya malalamiko. Tuliuliza kama fomu ya malalamiko zipo tukaambiwa zipo Mheshimiwa Jaji.

Wakili H: Fomu za malalamiko zilikuwa zimejazwa?

Mnyika: Kuna hatua mbili….Jaji: fomu 16?

Mnyika: Hatua ya kwanza tuliona lakini uhakiki wa kina tukaambiwa tutahakiki kesho asubuhi 01/11/2010. Naweza sema zoezi la uhakiki lilifanyika rasmi 01/11/2010. Tulihakiki kwa kina, vifaa toka kata ambavyo ni pamoja na masanduku yakikuwa na ceiled na vingine siwezi kukumbuka in details. Msimamizi alitumbia katika kuanza hakuna fomu ya malalamiko yenye jambo la kushughulikiwa katika majumuisho. Fomu alizopokea ni kuonyesha zoezi lilienda vizuri. Akatuuliza wahgombea na mawakala je kuna taarifa za malalamiko.

Wakili H: ajibu swali

Mnyika: Nido najibu Mheshimiwa Jaji na nimeeleza alisema hakukuwa na malalamiko ya kutufanya tushughulikie.

Wakili H: Ulisema wakala wa CCM alikuwa amelewa na ananuka pombe. Tuelezee

Mnyika: alikuja ananuka pombe ni mlevi.

Wakili H: Hivyo kilichokufanya uone ni harufu ya pombe?Mnyika: Ndiyo

Wakili H: Kitu gani ungethibitisha kama alikuwa ndani?

Mnyika: Mimi kama mgombea nilikuwapo na wakala. Mashahidi wote wamenitaja nilikuwapo. Pia wakala wangu amesaini.


Wakili H: Unaweza kuwakumbuka mawakala?

Mnyika: Kwa majina au kwa sura? Kwa majina wote isipokuwa mmoja. Kwa sura nakumbuka watatu na wagombea wawili waliokuwepo kituoni.

Wakili H: Mawakala waliokuwemo ni wangapi?

Mnyika: Ninaojua walio sainiJaji: unakumbuka walikuwepo wangapi?

Mnyika: Watatu na wa CUFF wanne na wagombea

Wakili H: wakala tu

Mnyika: Pamoja na wagombea wawiliJaji; wa chama gani?

Mnyika: CHADEMA, AFP, CHAUSTA na CUF na wagombea Mheshimiwa JajiJaji: Umeulizwa wakala

Wakili H: Ulijuaje wakala kwa jina na si sura?

Mnyika: Tulitambulishwa kisha majina yakawa yanaendelea kutajwa tajwa

Wakili H: Huoni kuna uwezekano kama uliona sura. Yule hajasaini ni kwa sababu hajasaini?

Mnyika: Hakutambulishwa. Siwezi kukumbuka jina la wakala wa CCM. Wengine tulitambulishwa.

Wakili H: Unataka kusema wakala ambaye hakutambulishwa hakuwepo?

Mnyika: Nimesema nilitambulishwa kwa wale waliokuwepo. Yule aliyenuka pombe baada ya kuondoka sikumuona tena.Wakili H: Nikuulize wakala Michael John Dalali wa CHAUSTA mna uhusiano upi?

Mnyika: Michael John Dalali ni ndugu yangu. Ni mdogo wangu.Wakili H: Je na Alex Mayunga wa AFP?

Mnyika: Ni mtu ninaye mfahamu na tukakutana naye katika uchaguzi.Wakili H: Huna uhusiano nae wa kindugu?

Mnyika: Sina uhusiano nae wa kinduguWakili H: Hivyo hawa umeweza kuwatambua kwa sababu una uhusiano nao?

Mnyika: Nilisema nilitambulishwa. Hawa wengine kama
Kambona na wa CUF nina ufahamu kwa sura. CCM namkumbuka kwa ulevi wake. Pia wakala si lazima umfahamu kisa ni ndugu yako.

Wakili H: Shahidi wa kwanza alisema amepigiwa simu kuwa laptop zimepatika kwa Mnyika

Mnyika: Nakumbuka. Hivyo hayakuwa si sahihi.

Wakili H: Hayakuwa ya uongo?

Mnyika: Nilisema si sahihi

Wakili H: Hivyo si uongo?

Mnyika: Nilisema si sahihi

Wakili H: Mahakama imeelewa.


Wakili H: Kampeni ilianza lini Ubungo?

Mnyika: Agosti 21 Ubungo Mheshimiwa Jaji.

Wakili H: Ilikuwa juma ngapi?

Mnyika: Sikumbuki Mheshimiwa jaji najua tu ilikuwa siku yangu ya kuzaliwa.

Wakili H: Kama ndivyo, shahidi aliyesema ilikuwa jumapili alikosa si ajabu wewe umeshindwa hapo

Mnyika: Yeye aliandaa shauri. Alikuwa nalo muda mrefu. Anajua. Mimi nimeulizwa hapa hapa tu.

Wakili H: Unakumbuka ulifanya mkutano Riverside?

Mnyika: Ninavyokumbuka ni Agosti 21 tu

Wakili H: Inawezekana unakumbuka Agosti 21, je 11/09/2010 ulifanya Riverside?

Mnyika: Nakumbuka juu ya Agosti 21, 2010 si Riverside


Wakili H: 09/10/2010 mlifanya mkutano Riverside na mkakashifu

Mnyika: wewe unaniambia

Jaji: Kweli au si kweli?

Mnyika: Sikuwa na mkutano Mheshimiwa Jaji, nilikuwa Saranga

Wakili H: Laptop haitaji kama kifaa kama ulivyosema

Mnyika: Sheria haitaji

Wakili H: sheria nnayo inataja instruments

Mnyika: Na maanisha vifaa vyote vya uchaguzi

Wakili H: Shahidi unaweza kukumbuka masanduku ya mwisho yalifika saa ngapi?Mnyika: Kati ya saa 3 asu hadi saa 4 asu. Siwezi kukumbuka exactly

Wakili H: Kata zipi?

Mnyika: Siwezi kukumbuka kata exactly ila ni kati ya kata 14 za jimbo la Ubungo. Ukitaja naweza kuzitaja.

Wakili H: Michael Dalali, mdogo wako inasemwa alikuja na laptop na kukupa

Mnyika: Inashangaza maelezo haya ninayojua hapa ni kuwa ilitajwa niliingia nazo nimezikumbatia kifuani

Jaji: Wakili ongea na mteja wako John Mnyika mueleze namna ya kujibu. Maana majibu mengine inaweza kutafsiriwa kama dharau kwa mahakama.Wakili J: Nimemweleza tayari Mheshimiwa Jaji

Wakili H: Dr.Sixtus alikuja saa ngapi?

Mnyika: Sikumbuki muda Mheshimiwa Jaji.

Wakili H: Kati yake na Mkurugenzi alitangulia nani?

Mnyika: Alitangulia Mkurugenzi

Wakili H: Walipishanaje?

Mnyika: Siwezi kukadiria

Wakili H: kama dakika 30 au 40 hivi

Mnyika: Haiwezi kuzidi nusu saaWakili H: Unakumbuka nani alitaka laptop zitumike?

Mnyika: Msimamizi wa uchaguzi Bwana Nduguru baada ya kushauriana na wenzake

Wakili H: Unakumbuka laptops zilihakikiwa vipi?

Mnyika: Walikuwa wanawasha laptops moja baada ya nyingine. Wakifanya kitu wanachojua wao pale kisha wakasema laptops hazina tofauti.

Wakili H: Maelezo ambayo ulitoa hapa na nakala uliyowasilisha mahakamani. Hakukuwa na tofauti ya kura. Je haya nayo ni sahihi?

Mnyika: Nilikamilisha na kueleza kura nilizopata ndizo nilizopata na si zaidi.

Wakili H: Je maelezo ya tofauti ya kura zilizopigwa, kura halali?

Mnyika: Nilisema kura zilizotajwa zangu ndizo Mheshimiwa Jaji.Re-examination:

Wakili J: Kuwepo au kutokuwapo shahidi namba 3 imekuwa mzozo mkubwa hapa mahakamani. Je angekuwapo ungejuaje?

Mnyika: Ningejua kwa vitu viwili. Kwanza; Ningemuona na ningeshuhudia nilichokiona. Pili, angesaini na ningethibitisha alikuwepo.

Wakili J: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji.Jaji: kesi itaendelea kusikilizwa 02/04/2012
 
Tunashukuru kwa kutuletea taarifa hiyo, lakini ungejaribu kuipanga vizuri ili isomeke kwa ufasaha. Inatuchosha wasomaji, na mimi nimeshindwa kusoma mpaka mwisho.
 
Back
Top Bottom