Yaliyo nikuta mwaka mpya ndani ya CLUB AQ Jijini Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyo nikuta mwaka mpya ndani ya CLUB AQ Jijini Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by B.O.G, Mar 21, 2011.

 1. B.O.G

  B.O.G Senior Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 145
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku ya mwaka mpya mimi pamoja na mwenzangu baada ya kumaliza shughuli zetu zilizo tupeleka Mjini Arusha kwa wakati huo tuliamua kwenda CLUB AQ kwakuwa ipo karibu na stendi ya mabasi ambayo tunge abiria asubuhi yake kurudi Jijini Dar Es Salaam.
  Tulipofika pale tulikuta mabaunsa wawili mlangoni pamoja na mzee mmoja ambaye nahisi alikuwa ni meneja.tukakata tiketi halafu tukaambiwa tusubili lift ije ili tuweze kupandishwa eneo ambalo clubin activities za CLUB AQ zinafanyika. kwa mimi binafsi sijui kwa sababu ni mshamba au ya mazoea niliomba nionyeshwe ngazi ambazo zinge weza kunifikisha huko juu badala ya Lift. Wale mabaunsa wakasema kwenye ngazi kuna matengenezo kidogo hivyo hazitumiki.Hatimaye lift ilipo fika tukaingia ndani mie na mwenzangu tuka pewa maelekezo kuwa tubonyeze button iliyo andikwa No 2.tulipofika kwenye club tulikuta watu wa wasitani. kama ilivyo kawaida umeme ulikuwa una katika na kuwaka tena kama mara tau hivi. mara nyingi napenda kudadisi vitu hiyo nikaanza kuwauliza maswali mbali mbali watu ambao walionekana wenyeji kidogo ndani ya club hiyo ,kitu kimoja nilicho kuja kugundua nikwamba Club hiyo haiko ghorofa ya pili kama nilivyo dhani wakati naambiwa bonyeza button no 2,sina uhakika ila inasemekana iko ghorofa No 7.
  Ilipo fika saa kumi na nusu Umeme ulikatika, Nika mtafuta mwenzangu ambaye tuliingia naye ili tuweze kushuka chini kupitia mlango wa dharula ulio kuwa umeandikwa Emergency door. Mlango ule haukuweza kufunguka basi nikatafuta mlango mwingine nao haukuweza kufuguka ndipo nika muuliza baunsa kuwa kulikoni huu mlango wa dharula haufunguki akanijibu subiri lift, well nika enda nika simama karibu na mlango walift pamoja na mwanzangu hatimaye baada ya takriban dakika ishirini umeme ulirudi ndipo mie na mwenzangu tukaingia ndani ya lift, ndani ya ile fift palikua na tangazo kuwa wasizidi watu saba, mmoja wa mabaunsa alianza ku muru kuwa mda wa kufunga ume fika watu waingie kwenye lift,walipo timia watu saba nika mwabia yule baunsa kuwa tumesha timia watu saba
  aliniangalia yule baunsa kisha akasema nyie watu wa Dar wajuaji sana huku watu wakiendelea kumimijnika ndani ya chomb.hatimaye tulikua watu zaidi ishirini na mbili ndani ya chombo kile.Mimi nikaomba nipite ili niweze kutoka nje ya lift ili kuepuka chochote ambacho kingeweza kutokea, yule baunsa alinivuta na kunirudisha ndani ya Lift. Mlango wa lift ukafunga kisha tukaanza kushuka chini.Lift ilipo fika chini yule baunsa alikuwa mlangoni akapiga hatua moja kutoka nje ya lift kisha akageuka kutataza mlangoni ambapo watu tunatokea akasema nyie watu wa dar wajuaji sana Akanirukia teke kisha akanivuta na kuanza kunizaba vibao ila kweli nilipigika siku hiyo na keep in mind kwamba mimi siyo mlevi labda nilileta fujo yoyote siku hiyo hapo hapana ila hii ndo hali halisi ya Club AQ iliyoko kwenye mji wa kitari arusha.
   
 2. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Pole sana mkuu.
   
 3. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole kwa yaliyokukuata.Club iko ghorofa ya saba si ya pili.
  .....Inawezekana ulionyesha ubishoo sana...ndo maana pia akagundua kuwa wewe ni mtu wa dar,na si mwenyeji.Najaribu kuimagine mpaka baunsa anagundua kuwa we umetokea dar....lazima kuna nyodo ulionyesha kwake na ndo maana akatoa kichapo.Hata hivyo ulitakiwa kucha ukua hatua za kisheria maana ni kosa kwa mtanzania mwenye akili timamu kupiga mwenzie.
   
 4. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  100% true,....

  Mambo uliyoeleza yote ni kweli kabisa,katika klabu ambazo ninazifahamu hapa nchini na ambazo zimekaa kihatarishi na kishari nafikiri club AQ inaongoza,kwanza nikiri tu kwamba nimetembelea club nyingi tu hapa nchi tanzania hasa kwenye mikoa ya dar,mbeya,mwanza na hapa arusha ambapo ninaishi kwa sasa kwa zaidi ya miaka 2,....club haina ngazi ya kupanda/kushuka inayoeleweka kwa wateja,wabaunsa wa pale ni hovyo(wanaharass wateja bila sababu) ingawa kwa hili ndivyo walivyo wababe wote wa arusha,club imejaa waizi wake kwa waume,iko ghorofani halafu emergency exit(doors) ni za geresha,....anyway its not a place 2b while in arusha - you better go to mawingu,maasai camp,new triple 'a' club and the like while in the city and you feel like enjoying.....
   
 5. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,301
  Likes Received: 953
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, pia ungeulizia jina la huyo mbeba vyuma.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,436
  Trophy Points: 280
  siend hapo
   
 7. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  dah hii only in TZ unaenda club halafu baunsa anakupa kichapo duh ningehakikisha hicho ki club kinafungwa outright.
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Acha ushabiki bro, karibu wenyeji wote wa Arusha wana lafudhi inayofanana(kama ile ya Dogo Janja), mtu ukitoka Dar ni rahisi kukutambua kutokana na Kiswahili kilichonyooka, na wala si ubishoo kama unavyodai. Halafu kinachonikera na raia wa Arusha ni usela mavi, ubabe usio na msingi wala nini, thts why matukio ya kuchomana visu hayaishi.
   
 9. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu Arusha wengi ni wa babe mie nshawahi kuitiwa polisi kisa nimekataa kubebewa mzigo stendi.
   
 10. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  na hiyo ndio arusha mzee,.....
   
 11. A

  Anold JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,378
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  Pole sana ila nakushauri maeneo ya club maranyingi ya mambo ambayo yanaweza kuondoa amani yako, ni vizuri ukayaepuka na kutafuta sehemu ambayo haiwezi kukupa usumbufu usio wa lazima.
   
 12. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,823
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
  mpigie wenye ile AQ mpe hizo taarifa
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hivi Arusha hakuna waangalizi wa usalama katika hayo majumba ya starehe. Hii ni ajali inayosubiriwa na watu wanaitazama hivihivi. je kukitokea moto hasa wakati umeme umekatika? Si watu wote humo ndani wataangamia? Kwanza, hawataona wanapolekea, pili hapatakuwa na pa kuelekea kwa vile hakuna milango ya kutokea wakati wa hatari. Inatisha kufikiria hali hiyo. Tunashukuru kwa kutuwekea hii post hapa ili watu waepuke kwenda kwenye club hiyo.
   
 14. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Welcome to Arusha mazee...
  Next time tafuta mwenyegi akupe details za kila kumbi za starehe... Kama walivyosema hapo juu...Arusha wababe wengi lakini they are all cowards...Ukitaka kuenjoy Arusha jifanye **** (act a fool)!! Nachekacheka nao, watakupenda..lol:lol:
   
 15. myao wa tunduru

  myao wa tunduru JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2010
  Messages: 615
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  kwa Tanzania sehemu ambazo kuna wajanja washamba (watabe) wengi ni Arusha na Mbeya...samahani kama kuna mtu nimemkwaza ila experience yangu yaonyesha hivyo
   
 16. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Huoni wasanii wa Arusha kutwa kujisifia , wale jamaa ni washamba na hawajiamini na bado wanaona ubabe ndio dili , waepuke sana wasela wa Arusha maana visu kwao ni jambo dogo sana.
   
 17. m

  mareche JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  kila mahali kuna wajanja ila arusha wamezidi pia kuna babdhai ya sehemu ukitipa usiku lzm wakusachi aq sio mahali pa kwenda ka ama ina ustarabu wako
   
 18. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  teeh teeeeh teeeehhhh woga wako tuu mbona ukikaza wananywea wale:canada:
   
 19. aye

  aye JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  Pole sana mkuu ila hapo hapafai kabisa kwa starehe panaonekana na ikitokea hatari ni balaa watu hawatatosha kwene iyo lifti then wanakwambia bonyeza namba 2 kumbe ni gorofa ya saba du kali kweli
   
 20. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  huko kujifanya una kiswahili kilichonyooka kuliko wenyeji ndo kunazalisha kipigo.Nani kakwambia Arusha wote ni waarusha(wote wana lafudhi moja).Kuna makabilamchanganyiko bwana.
   
Loading...