Yalitaka kutokea mauaji ya Halaiki Hapa Magomeni muda huu

Kama nyumbani unawaacha vizuri kimsosi akuna shida, ila watu mmebarikiwa matumbo, yani supu ya mbuzi+ chapati nne tena unakuta nizile kubwa kama sikio la tembo + maziwa fresh? Aisee mm siwezi ata kunyanyuka nikatembea nitalala hapo juu mezani.
 
Kuna kitu nimejifunza humu Kuna Watu uislam unawauma Sana na sijui kwanini,hii story Ni ya kutunga kabisa,inaonekana ukubwa na utukufu wa mwezi huu unawapa shida Sana huu Ni miongoni mwa miezi mitukufu ambayo waislam huwa tunakuwa pamoja na hatutofautiani,hakuna anaefunga kwa kuacha kitu flani ila wote tunafunga sawa! Ishawekwa picha humu ya miaka mitatu nyuma tukaambiwa limetokea Zanzibar juzi! Poleni Sana kwa mnaoumia kwa mwezi huu na Uislam kwa ujumla
 
huwezi kula supu (ya nyama) na maziwa fresh usiharishe. Huwa haishauriwi.
ni kama kulamba asali na muda huohuo utafune tango, lazima uage dunia.
Kwenye Tango na Asali sijui (ila ipo siku nitajaribu)

Sasa hapo kwenye Maziwa na Supu siwezi kupasahau na sikuwahi kujua sababu mpaka leo umeandika.

Masaa machache kabla ya safari DOM-DAR nikiwa na masela wangu tushakamatia boom niligonga hiyo megamix.

Chombo imekula gia, mpaka tunatoka gairo tu, tumbo lishaitika mzee.. Nilimaliza mikao yote .

Ilifika kipindi nikamuomba konda nishuke tu wao waendekee na safari, abiria wamekodoa machoo. Kondo akanikazia.

Mateso niliyopata mpaka nafika Moro yalikua ni balaa. …

Maziwa plus nyama hapa kwa kweli
 
Kosa lako kuvaa vazi la kiislam na huku unakula hadharani. Dini inaruhusu wasiofunga kutokana na sabab mbalimbali wale kama kawaida ila sio HADHARANI.Ungevaa vazi neutral hakuna ambaye angekusogelea
 
Si vizuri kula barabarani manyama na chapati afu nyumban wanashindia ugali wa Matembele.

Ni vizuri mtu ukaacha nyumbani mambi safi ,sio kwenda kuchoma nyama kilo barabaran afu nyumban wanapika dagaa wa mafuta
Ndugu yangu ni wachache wanatambua hilo.
 
Leo nimeamka nikiwa simple tu nilipigiwa simu ofisini nielekee sehemu moja Magomeni kwa shughuli za kikazi. Nilivaa vazi ambalo wengi husema asili yake ni uarabuni. Lakini mimi nilinunua duka la kihindi wanaita Punjab Style.

Ni mpenzi wa kuvaa hivyo huvaa nguo tofauti tofauti za tamaduni mbalimbali.Kuna siku unaweza nikuta nimevaa kimasai.

Nikiwa navuta muda kuweza onana na mtu wangu nikaona nishuke kwenye gari nikae sehemu moja wanauza chakula na nikaagiza soup ya mbuzi na chapati nne na maziwa fresh.

Nimekaa nakula akaja jamaa mmoja ananiita mimi kobe? Sukumwelewa anamaanisha nini.Baadaye mwingine pembeni ndo akanambia kwanini nakula hadharani? Nilimjibu ni haki yangu kula popote kwa wakati wowote.

Jamaa yule wa kwanza alitoka akaja na wenzie watatu wameshika bakora etu kuniadabisha kwa kuudhalilisha Uislamu. Jamaa wamekomaa hasa na bakora zao na imekuwa zogo.

Niliwaambia nataka nimwone wa kwanza kunichapa bakora.Nikasimama maana ndani ya ile nguo nimevaa kisuruali ambacho kina mifuko.Nikatoa silaha maana nilihisi wale jamaa wanataka kuhatarisha maisha yangu.

Hiyo ndo imekuwa ponea yangu sababu jamaa waliona nipo serious nami ningelazimika kufanya mauaji ya halaiki kwa wale jamaa maana walisha paniki bila sababu wanataka kuniadhibu for no reason.

Nauliza waungwana kuna kosa gani mimi kula mchana nikiwa nimevaa mavazi ambayo leo nimeambiwa ni ya kiislamu?mimi nafahamu wayahudi wanavaa hivi huko Israel. Nafahamu kuna wakristo wa kiarabu wanavaa hivi.

Kwanini hili vazi lionekane ni la dini fulani? Mimi binafsi sifungwi na dini nina imani yangu kwa Mungu lakini sibanwi na dini, sipendi unafiki.

Why waone nadhalilisha uislam wakati sikuongea neno lolote la kiislamu au sikufanya ishara yoyote ya kuonesha mimi ni mkristo au muislam?

Hizi akili hawa jamaa walitoa wapi kuona wanastahili kuniadhibu acha kuniita kobe sikuona issue sababu hata ukiniita shetani ikiwa najua mi si shetani siwezi gombana nawe.

Mi nadhani tuheshimiane na tuheshimu haki za watu wengine. Mimi nimekulia ktk mazingira ya kiislam naufahamu uislamu some how naufahamu ukristo some how. Tusitake kuendesheana maisha.

Leo kweli ngemchapa mtu risasi ya mguuni na ingekuwa gumzo. Najua kuna watu watakuwa wamechukua video tukio hilo. I dont care but nawaambia watu wasio na ustaarabu wasitumie dini vibaya.
We muongo!
 
Umekosea sana, ingekuwa heri kama wangekuua kabisa, unavaa vazi lenye taswira ya uislam alafu unakula hadharani wakt wenzio wako kwenye swaumu kama sio kuwadhiaki ninini.
 
Mkuu ungefyatua hata 2 tu za hewani story ingenoga kweli hii.Maana inge andikwa ......watu kadhaa wakoswakoswa kwa risasi huko Magomeni. Mtuhumiwa aliyefyatua alitaka kuadhibiwa kwa kukutwa akiwa amevalia kanzu na huku akila chakula hadharani mchana kipindi mfungo wa ramadhani
 
Aiseee.... Hapa ulitumia logic sijui kama walikuelewa.... Mimi hawa watu wanaodhani wanazijua dini sana kuliko wengine
Ila sometime sisi wafuasi wa Muddy tuna tabu. Yaani mtu anaacha kufunga anaanza kutamani chakula cha wasiofunga hata kudiriki kutaka kumpora kwa bakora. Ukifunga usitamani kula mchana.
 
Back
Top Bottom