Yale Yaleee

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Hii picha inapatikana kwenye gazeti la Mwananchi la leo. Huyu Mheshimiwa bado anaendeleza mbonji bungeni na posho anachukua vile vile.

attachment.php



bungeni.jpg
 
Halafu hapa tutegemee mijadala ya maana na yenye tija kwa wananchi. Watu hawa wakiwa Dodoma wanakuwa kama wawindaji. Hapo usikute usiku kucha wamekesha kwenye maulevi au kuwinda vimwana halafu kunapokucha anatafuta namna ya kulipizia. Na kwa vile posho hupati mpaka usaini mahudhurio ndo wanalazimika kuja kulalia ukumbini. Aibu tupu!
 
Hebu nijuzeni, ni nani huyu babu?...Watu kama hawa ndio kweli uwaambie posho zifutwe atakubali, wakati kwa kulala namna hiyo analipwa!
Bongo safari ndefu sana!
 
Kama Waziri anelala katika vikao vikubwa vya kimataifa, kwanini mbunge naye asichape usingizi.
Viongozi wetu hawapo serious hata kwenye mambo ya msingi.
 
Kachaguliwa na huyu amwakilishe huko bungeni.

7.jpg
 
Kweli safari ya kuelekea kwenye Maendeleo bado ni ndefu sana..
 
Nchi inataia aibu sana hii..yaani ukiangalia jinsi watu tuko nyuma kimaendeleo bado haya majamaa yanalilia posho eti huyu PM dhaifu nae anasema eti posho ni mhimu zinagawiwa wapiga kura!! shame
 
Yuko kwenye deep reflection ya matters of great nashunal importance, kama hutaki mtafute kwa komenti
 
Kachaguliwa na huyu amwakilishe huko bungeni.

7.jpg

Hamjui huyu mpaka uchaguzi mwingine, atakapopita akijipiga kifua kwamba ametekeleza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni, as if kulala bungeni ilikuwa ni moja ya hizo ahadi!
 
Nchi inataia aibu sana hii..yaani ukiangalia jinsi watu tuko nyuma kimaendeleo bado haya majamaa yanalilia posho eti huyu PM dhaifu nae anasema eti posho ni mhimu zinagawiwa wapiga kura!! shame

Na mfuko wa jimbo una kazi gani?
 
Ingekuwa ni vizuri Wabunge wote wakapimwa afya zao,kila siku kabla ya kuingia kwenye vikao vya bunge.Itakapogunduliwa ni wachovu,wana hangover,wasiruhusiwe mpaka hapo afya zao zitakapo kuwa safi.Hatuwalipi kwa kazi ya kusinzia au kupiga porojo.Hawa ni watumishi wetu,wameajiriwa na wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom