Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Kwa mtu anayechanganua masuala kwa undani utagundua kuwa matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu kile walichokuwa wanakiita ''Hali mbaya ya maambukizo nchini'' kimepotea baada ya tamko lao la mwisho la mwezi Mei 2020.

Nadhani Ubalozi wa Marekani umegundua kuwa matamko hayo yalikuwa hayaisaidii Marekani kwa sababu walichokuwa wanakisema kilikuwa hakionekani kwenye uhalisia lakini kikubwa zaidi, balozi zingine kama za umoja wa Ulaya zilikuwa kimya.

Matamko ya mara kwa mara ya Ubalozi wa Marekani yalimuibua mwandishi kutoka Uholanzi wa kampuni ya habari, VOICE OF AMERICA aitwaye Ruud Elmendorp kufanya uchunguzi wa kina nchini ili kujua ukweli. Alitembelea mpaka makaburi mbali mbali nchini mara kwa mara hasa yaliyopo Dar es Salaam kuona kama kuna shughuli nyingi za mazishi lakini aligundua hakuna shughuli hizo.

Ukitaka kusoma habari na kuangalia video yake ya Uchunguzi unaweza kugonga LINK hii >>>COVID-19 Diaries: Can Tanzania Really Be Coronavirus-Free?

Kuna msema usemao, ''mficha maradhi kifo humuumbua''. Hii ina maana kuwa kama serikali ya Tanzania ilikuwa inaficha maradhi yatokanayo na COVID-19 basi vifo vya watu wengi vingeiumbua serikali.

Baada ya maambukizi ya COVID-19 kuanza kusambaa kwa kasi katika nchi za Afrika, nchi nyigi za Afrika zilijikuta zikifuata mfumo uliokuwa umependekezwa na WHO katika kukabiliana na janga hili lakini Serikali ya Tanzania iliamua kufuata mfumo tofauti ambao ulizishangaza nchi nyingi duniani lakini pia umesababisha kuzolota zaidi kwa mahusiano ya serikali ya Tanzania na serikali ya Kenya.

Maamuzi ya serikali sio kwamba yalizua mjadala mkubwa na mkali kwa jumuiya za kimataifa peke yake bali pia hata hapa nchini. Jukwaa la Jamiiforums halikubaki nyuma katika mjadala huo ambapo thread hii;

GONGA LINK>>>Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’ , iliyofunguliwa mwezi wa tatu ilichochea mjadala mkubwa na mkali kuhusu maamuzi ya serikali.

Mwana Jamiiforums Nyani Ngabu alikuwa ni mmoja wa Watanzania wa mwanzo kukubaliana na mtazamo wa Rais Magufuli katika mapambano ya Korona. Mwezi wa tatu alileta mada yenye kichwa cha habari, ''Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/hofu. Baadhi ya wanajamii walipingana naye sana kuhusu mtazamo wake wengine wakimshambulia yeye badala ya hoja yake.

Mada yake hiyo inapatikana hapa, GONGA LINK>>>Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Mwanajamiiforums mwingine Mzee Mwanakijiji alileta pia mada mwezi wa tatu kuhusu kile ambacho alikuwa anakiita maamuzi ya Rais Magufuli kuhusu Corona ni bahati na nasibu lakini akamalizia kwa kuuliza ITALIPA?

Ukitaka kusoma thread hiyo GONGA LINK>>>HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Mijadala hii ilikuwa inakolezwa na matamko yaliyokuwa yanatolewa mara kwa mara na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambayo yalikuwa yakionyesha ''kuna hali mbaya'' ya maambukizi na vifo nchini.

Kwa sasa imepita miezi 6 tokea mijadala mikali itokee nchini na nje ya nchi kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli kuhusiana na korona. Kinachoshangaza kwa sasa hata matamko ya Ubalozi wa Marekani nchini hayatolewi tena na hata wale ambao walikuwa wanakubaliana nayo huku wakimshutumu Rais Magufuli wamebadilisha mwelekeo kimya kimya baada ya kushindwa kupambana na ukweli halisi.

Je, Matamko ya Ubalozi wa Marekani yalikuwa yana malengo gani?

Kama matamko hayo yalikuwa yana malengo, Je, malengo yake yametimia ndio maana hayatolewi tena?

Je, waliokuwa wanakubaliana na matamko ya Ubalozi wa Marekani wamepotelea wapi?
 
Kama ukweli umebainika unafikiri watasema nini?

Ilikuwa kila mara wanaweka mabandiko ya tanzia ili tu kuleta hofu! Yule balozi wa Marekani alikwenda na yake sasa hivi yupo mpya ameenda mwana kwenda.

Wengi wamekuwa hawajui hili Tanzania bado ni taifa linalojielewa ni wachache tu ndio hawajielewi.. na hao ndio huwa wanashupaza mishipa kuwatetea wapuuzi fulani ati tufuate mitazamo Yao!

Hizi sio zama za kushikiwa ubongo maana hata hiyo Marekani ilikosana na WHO kwa madai ya kuwa imeelekea zaidi China n.k

Kama wao wanauwezo wa kujiamulia waonacho sahihi basi hata sisi pia tunaweza, waswahili walisema kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake. Marekani sasa hivi inapambana kurudisha uchumi wake uliodorora.
 
Mungu katuepusha kwa miujiza

Vifo vilikuwepo si kwa rate ile iliyosemwa...
Nakubaliana na angalizo lako.

Ni kama miujiza fulani imetokea Tanzania.

Maamuzi ya serikali ya Tanzania kwa sasa yanaziweka serikali za nchi za Afrika ya Mashariki hasa Kenya katika wakati mgumu kisiasa mpaka inaanza kutafuta baadhi ya Watanzania wa kuisaidia kujibu hoja!
 
Kama ukweli umebainika unafikiri watasema nini? Ilikuwa kila mara wanaweka mabandiko ya tanzia ili tu kuleta hofu!. Yule balozi wa marekani alikwenda na yake sahivi yupo mpya ameenda mwana kwenda...
Ninakubaliana na maoni yako.

Nadhani hofu ilikuwa ni kubwa kuliko uhalisia!

Serikali haikuyumba katika msimamo wake pamoja na uwepo wa hofu kubwa katika jamii.
 
Corona imepaishwa sana, hususan huko Marekani.

Na sababu kuu ni uchaguzi wao mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu.

Inatumiwa kama fimbo ya kisiasa ya kumchapia Rais Donald Trump.

Ila kwa sasa ninachokiona huko Marekani ni kuna ‘pandemic fatigue’.

Watu wammeanza kuzichoka hizo habari za Corona.

Kama ugonjwa ungekuwa ni hatari kama tulivyoaminishwa, basi sisi tungeathirika kupita maelezo.

Hata huyo Tundu Lissu mwenyewe naona amekubaliana na hali halisi.

Kwenye matembezi yake huko kusaka wadhamini hachukui tahadhari zozote zile zilizopendekezwa na bado anaonekana mzima mwenye afya tele.

Dunia nzima, labda ukitoa Tanzania, imelishwa tango pori.
 
Afsa wake mwandamizi mkuu yupo kwenye ziara mikoani kutafuta wadhamini ila kila akipata muda wa kuongea na media za kenya anasisitiza korona inaua na watu wanazikwa usiku!
Huyo ni mwanaharakati!

Kama unavyojua wanaharakati ni wazuri sana katika kudandia na kushadadia masuala mbali mbali na wepesi wa kusahau kile walichokuwa wanakishadadia!
 
Huyo ni mwanaharakati!

Kama unavyojua wanaharakati ni wazuri sana katika kudandia na kushadadia masuala mbali mbali na wepesi wa kusahau kile walichokuwa wanakishadadia!
Kweli kabsa anachosema sicho anachokifanya sasa anajizodoa mwenyewe kila uchao wanarusha picha kuonyesha hicho wanachokiamini nyomi la watu dunia inamuona na kumshangaa umati ule hakuna tahadhari yetote za kiafya zinafuata hata yeye hana mask sasa mwendawazimu sijui ni nani hapo kama si yeye!
 
Corona imepaishwa sana, hususan huko Marekani.

Na sababu kuu ni uchaguzi wao mkuu wa mwezi Novemba mwaka huu...
Ninakubaliana na angalizo lako.

Kesi ya Marekani ninaifananisha na kesi ya Kenya kwenye hili suala la Corona.

Serikali ya Kenya ilipaisha sana Corona kwa wananchi wake kiasi kwamba uoga na hofu ilikuwa kubwa.

Kwa sasa wananchi wameanza kuchoka na hata wanasiasa wameanza kuvunja masharti kwa kufanya mikusanyiko isiyo na tahadhari.

Tatizo kwa serikali ya Kenya maambukizi yanazidi kila siku huku wananchi wakionekana kuchoka. Kibaya zaidi hata pesa za mkopo ili kushughurikia Corona zimepigwa na wajanja!

Tundu Lissu hakujua kuwa wananchi wengi wanaungana na msimamo wa serikali kuhusu corona ndio maana kwa sasa ameanza kuachana na hoja zake kuhusu corona baada ya kugundua hoja zake hazilipi kisiasa!
 
Mpiga zumari wao wa Corona Lissu kasahau kazi aliyotumwa ya kueneza uongo na uvumi kuhusu corona anatafuta wadhamini nchi nzima akiwa havai hata hiyo barakoa. U SA, Lissu na WHO wameaibika sana kuhusu corona Tanzania.
Mimi nadhani amegundua biashara ya siasa za Corona nchini hazilipi ndio maana kwa sasa huwezi kumsikia tena akisema kuna Corona nchini na watu wanazikwa usiku!
 
Tahadhari bado zinatolewa na ubalozi wa Marekani, nadhani walitoa moja wiki iliyopita na unaweza kuangalia hapa Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania
Nadhani kuna tofauti kati ya tamko na tahadhari!

Ni kawaida ya balozi nyingi kutoa tahadhari kwa raia wake kwa masuala mbali mbali lakini walichokuwa wanakifanya ni kutoa matamko mpaka ya kiswahili kuhusu Corona nchini.

Ukijiuliza matamko ya kiswahili kuhusu Corona yalikuwa yanamlenga nani au kupeleka ujumbe kwa nani?
 
Kweli kabsa anachosema sicho anachokifanya sasa anajizodoa mwenyewe kila uchao wanarusha picha kuonyesha hicho wanachokiamini nyomi la watu dunia inamuona na kumshangaa umati ule hakuna tahadhari yetote za kiafya zinafuata hata yeye hana mask sasa mwendawazimu sijui ni nani hapo kama si yeye!
Kwa anayoyafanya kwa sasa huwezi kumsikia tena akisema kuna vifo vingi nchini vinavyosababishwa na Corona na watu wanazikwa usiku!
 
Back
Top Bottom