Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

Nadhani kuna tofauti kati ya tamko na tahadhari!

Ni kawaida ya balozi nyingi kutoa tahadhari kwa raia wake kwa masuala mbali mbali lakini walichokuwa wanakifanya ni kutoa matamko mpaka ya kiswahili kuhusu Corona nchini.

Ukijiuliza matamko ya kiswahili kuhusu Corona yalikuwa yanamlenga nani au kupeleka ujumbe kwa nani?

Tatizo alikuwa ni yule kaimu balozi ambae alikuwa busy na hao wanaojiita wanaharakati.

Unapochunguza tatizo ni nini na unapoligundua unatafuta tiba.

Yule mwanamke akaitwa Foreign na akaambiwa achague aendelee kuheshimu mkataba wa Vienna au la arudi kwao.

Naona anachagua kurudi kwao.

Tanzania kuna watu wanadhani ni ile ya miaka ya 47 lakini si Tanzania ya leo nayo ina CIA ya kitanzania na yaendeshwa kwa Tanzania style.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Acha uongo kawadanganye wanasaccos wenzako huko. Mlipokuwa mnawadanganya USA kuwa hospitali zetu zimezidiwa? Tena wewe ulikuwa mstari wa mbele kabisa kusema eti tutaisha tunaojitambua tulikuambia uache uongo ukapaniki lakini tukaendelea kukupa vidoge ili upone ugonjwa wako wa slavery mentality. Eti leo unakuja na kusema nchi za Afrika azijaathirika sana na kwamba idadi ya vifo ya Kenya ni ndogo kuliko ya Tanzania eti tulishapita tayari. Kawadanganye familia yako.
Mkuu Tanzania waliokufa ni 21 tu maana tuna rais mahiri hahahaha
 
Jana nilikutana na mdada mmoja mwenye akili kama zako! Akasema korona hakuna Tz.

Nikamwuliza kama virus vya korona viliwezakusafiri kutoka China mpaka Ubeligiji then kutoka Ubeligiji vikafika Arusha -Tz, vitashindwa kutoka Kenya kwenye victim karibu 29,000 kuja Tz?

Jibu: Sisi kwa sababu tuliwahi kufanya maombi na hatukufunga makanisa! Hizi akili au matope!!
 
Pia likataza kupulizia waloita eti ni dawa ya kuua COVID-19 mitaani!

India wamepuliza hiyo dawa na sasa ina wagonjwa walo na COVID-19 wapatao 49,036...
Mkuu matokeo kwetu ni mazuri kwa kuwa tumeamua kujitoa ufahamu Ila ukweli ni kwamba,ukiwa na akili yako timamu utaelewa kile corona inafanya hapa
 
Jana nilikutana na mdada mmoja mwenye akili kama zako! Akasema korona hakuna Tz.

Nikamwuliza kama virus vya korona viliwezakusafiri kutoka China mpaka Ubeligiji then kutoka Ubeligiji vikafika Arusha -Tz, vitashindwa kutoka Kenya kwenye victim karibu 29,000 kuja Tz?

Jibu: Sisi kwa sababu tuliwahi kufanya maombi na hatukufunga makanisa! Hizi akili au matope!!
Mkuu hii Tanzania ya Magu bila kujitoa ufahamu maisha hayawezi kwenda,just relax,watu wameshajitoa ufahamu like their pzidii
 
Acha uongo kawadanganye wanasaccos wenzako huko. Mlipokuwa mnawadanganya USA kuwa hospitali zetu zimezidiwa?...
Wewe na Magufuli ni wamoja: i.e. mlisoma elimu ya kukariri hivyo hamkuelimika. Hiyo projection ya kusema kuwa Africa kutakuwa na casualities wengi wa corona virus ilikuwa ni scientific based projection iliyotolewa na wanasayansi duniani (wakiwemo waliotengeneza computer/simu unayotumia sasa, japo wewe huwezi hata kutengeneza protector yake).

Ilikuwa ni tahadhari sahihi kabisa ili kufanya maandalizi. Kilichofanya vifo viwe vichache kwa nchi nyingi za Africa (siyo Tanzania tu) mpaka sasa ni kitendawili na bado kinafanyiwa utafiti. Magufuli na nyinyi wana mapambio wake hamwezi ku-claim eti mna akili kwa kitu kilichotokea.

Ni kama ile hadithi ya mtu mjinga alivuka kwenye mto wenye mamba wakali na wenye njaa, na kwa bahati akaweza kuvuka halafu akawa anajitapa kuwa ule mto hauna mamba kwa sababu tu hajaliwa!
 
Hapana anangoja ahojiwe na vituo vya kenya ndio anasema hivyo ili kuwafurahisha.
Kupambana na ukweli ni kupoteza muda!

Hata kama vituo vya Kenya vikimuhoji lakini haiwezi kubadilisha ukweli bali ni kujiriwadha nje ya ukweli!
 
Mungu katuepusha kwa miujiza

Vifo vilikuwepo si kwa rate ile iliyosemwa.

Nadhan ki uhalisia sio sisi si mabara mengine wanaojua ni why,

Corona ingekuwepo kwa rate ile iliyokuwa inasemwa, maiti zingelala barabarani
Tuache I utani. Hivi Tanzania watu wanatumia nini.... Maana Haiwezekani yakawa ni maombi tu.
 
Mchawi wa matamko alikuwa ni Kaimu Balozi wa Marekani

Kuondolewa kwa kale kaBetina na "shogaake" balozi wa UK ndo kupotea kwa yale matamko.
Sidhani kama chanzo cha matamko alikuwa ni yule Kaimu balozi!

Nadhani yeye kama Kaimu Balozi alikuwa anapitisha tu maelekezo kutoka sehemu fulani yenye malengo fulani ambayo kwa bahati mbali yameshindwa kuushinda uhalisia!
 
Back
Top Bottom