Yale matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu COVID-19 nchini yameishia wapi?

Tatizo alikuwa ni yule kaimu balozi ambae alikuwa busy na hao wanaojiita wanaharakati.

Unapochunguza tatizo ni nini na unapoligundua unatafuta tiba.

Yule mwanamke akaitwa Foreign na akaambiwa achague aendelee kuheshimu mkataba wa Vienna au la arudi kwao.

Naona anachagua kurudi kwao.

Tanzania kuna watu wanadhani ni ile ya miaka ya 47 lakini si Tanzania ya leo nayo ina CIA ya kitanzania na yaendeshwa kwa Tanzania style.

Ni mtazamo wangu tu.
Mtazamo wako unaweza kuwa ni kweli!
 
Jana nilikutana na mdada mmoja mwenye akili kama zako! Akasema korona hakuna Tz.

Nikamwuliza kama virus vya korona viliwezakusafiri kutoka China mpaka Ubeligiji then kutoka Ubeligiji vikafika Arusha -Tz, vitashindwa kutoka Kenya kwenye victim karibu 29,000 kuja Tz?

Jibu: Sisi kwa sababu tuliwahi kufanya maombi na hatukufunga makanisa! Hizi akili au matope!!
Corona ipo lakini sio kwa kiwango kikubwa na hatarishi kama ilivyokuwa inadaiwa!
 
Tahadhari bado zinatolewa na ubalozi wa Marekani, nadhani walitoa moja wiki iliyopita na unaweza kuangalia hapa Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania

Hiyo ni habari mbaya sana kwa baadhi ya watu kuwa hizi alert zingalipo palepale.

Ni uzwazwa wa kutosha kuhusianisha hali ya ugonjwa na lolote liwe tamko au hata pongezi.

Ugonjwa? Aseme au asiseme nani au nini hali halisi kuhusu wenyewe iko palepale.

Mengine ni kujilisha upepo tu.
 
Naona SA Leo wame lift ban ya kuuza pombe na sigara na kusema itachukua miaka kadha kufidia loss ya lock down
Pesa za mkopo kwa ajili ya kupambana na COVID-19 zimeanza kuisha! Lazima waondoe lockdown
 
Corona ipo lakini sio kwa kiwango kikubwa na hatarishi kama ilivyokuwa inadaiwa!
Inawezekana vp Kenya iwe inaoneka kuwepo corona ambayo hatarishi ila Tz kuwe shwari hakuna hatari ya corona? ni taratibu zipi tulizofanya hadi sie tusiwe na hatari ya corona kama Kenya? au Kenya ni kipi wanachofanya chenye kuwafanya wawe kwenye hatari ya corona?
 
Kwa mtu anayechanganua masuala kwa undani utagundua kuwa matamko ya Ubalozi wa Marekani kuhusu kile walichokuwa wanakiita ''Hali mbaya ya maambukizo nchini'' kimepotea baada ya tamko lao la mwisho la mwezi Mei 2020.

Nadhani Ubalozi wa Marekani umegundua kuwa matamko hayo yalikuwa hayaisaidii Marekani kwa sababu walichokuwa wanakisema kilikuwa hakionekani kwenye uhalisia lakini kikubwa zaidi, balozi zingine kama za umoja wa Ulaya zilikuwa kimya.

Matamko ya mara kwa mara ya Ubalozi wa Marekani yalimuibua mwandishi kutoka Uholanzi wa kampuni ya habari, VOICE OF AMERICA aitwaye Ruud Elmendorp kufanya uchunguzi wa kina nchini ili kujua ukweli. Alitembelea mpaka makaburi mbali mbali nchini mara kwa mara hasa yaliyopo Dar es Salaam kuona kama kuna shughuli nyingi za mazishi lakini aligundua hakuna shughuli hizo.

Ukitaka kusoma habari na kuangalia video yake ya Uchunguzi unaweza kugonga LINK hii >>>COVID-19 Diaries: Can Tanzania Really Be Coronavirus-Free?

Kuna msema usemao, ''mficha maradhi kifo humuumbua''. Hii ina maana kuwa kama serikali ya Tanzania ilikuwa inaficha maradhi yatokanayo na COVID-19 basi vifo vya watu wengi vingeiumbua serikali.

Baada ya maambukizi ya COVID-19 kuanza kusambaa kwa kasi katika nchi za Afrika, nchi nyigi za Afrika zilijikuta zikifuata mfumo uliokuwa umependekezwa na WHO katika kukabiliana na janga hili lakini Serikali ya Tanzania iliamua kufuata mfumo tofauti ambao ulizishangaza nchi nyingi duniani lakini pia umesababisha kuzolota zaidi kwa mahusiano ya serikali ya Tanzania na serikali ya Kenya.

Maamuzi ya serikali sio kwamba yalizua mjadala mkubwa na mkali kwa jumuiya za kimataifa peke yake bali pia hata hapa nchini. Jukwaa la Jamiiforums halikubaki nyuma katika mjadala huo ambapo thread hii;

GONGA LINK>>>Janga la COVID-19: Naipongeza Serikali kwa kukataa kuiga baadhi ya mbinu za ’Nchi za Magharibi’ , iliyofunguliwa mwezi wa tatu ilichochea mjadala mkubwa na mkali kuhusu maamuzi ya serikali.

Mwana Jamiiforums Nyani Ngabu alikuwa ni mmoja wa Watanzania wa mwanzo kukubaliana na mtazamo wa Rais Magufuli katika mapambano ya Korona. Mwezi wa tatu alileta mada yenye kichwa cha habari, ''Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/hofu. Baadhi ya wanajamii walipingana naye sana kuhusu mtazamo wake wengine wakimshambulia yeye badala ya hoja yake.

Mada yake hiyo inapatikana hapa, GONGA LINK>>>Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Mwanajamiiforums mwingine Mzee Mwanakijiji alileta pia mada mwezi wa tatu kuhusu kile ambacho alikuwa anakiita maamuzi ya Rais Magufuli kuhusu Corona ni bahati na nasibu lakini akamalizia kwa kuuliza ITALIPA?

Ukitaka kusoma thread hiyo GONGA LINK>>>HOJA NDANI YA HOJA: Rais Magufuli na bahati nasibu ya korona - ITALIPA?

Mijadala hii ilikuwa inakolezwa na matamko yaliyokuwa yanatolewa mara kwa mara na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ambayo yalikuwa yakionyesha ''kuna hali mbaya'' ya maambukizi na vifo nchini.

Kwa sasa imepita miezi 6 tokea mijadala mikali itokee nchini na nje ya nchi kuhusu maamuzi ya Rais Magufuli kuhusiana na korona. Kinachoshangaza kwa sasa hata matamko ya Ubalozi wa Marekani nchini hayatolewi tena na hata wale ambao walikuwa wanakubaliana nayo huku wakimshutumu Rais Magufuli wamebadilisha mwelekeo kimya kimya baada ya kushindwa kupambana na ukweli halisi.

Je, Matamko ya Ubalozi wa Marekani yalikuwa yana malengo gani?

Kama matamko hayo yalikuwa yana malengo, Je, malengo yake yametimia ndio maana hayatolewi tena?

Je, waliokuwa wanakubaliana na matamko ya Ubalozi wa Marekani wamepotelea wapi?
Watakuja kutuomba msamaha karibuni wakidai kuwa yalikuwa ni auto print,ila kwa sasa wamesharekebisha hiyo shida...
 
Hiyo ni habari mbaya sana kwa baadhi ya watu kuwa hizi alert zingalipo palepale.

Ni uzwazwa wa kutosha kuhusianisha hali ya ugonjwa na lolote liwe tamko au hata pongezi.

Ugonjwa? Aseme au asiseme nani au nini hali halisi kuhusu wenyewe iko palepale.

Mengine ni kujilisha upepo tu.
Wewe unaleta siasa tu na ndio maana ule mkusanyiko wa watu pale Airport kumpokea Lissu et unausifia wakati umekuwa unapiga kelele kuhusu corona.
 
Covid-19 Brief: August 19, 2020

An increase in the number of Covid-19 tests across the UK, Oldham on the brink of lockdown, and an investigation into the UK government’s PPE contracts. Here are today’s latest figures and headlines, curated by upday.

The FiguresUK
Daily deaths: 28
Total deaths: 41,397
Daily cases: 812
Total cases: 321,098
Figures provided by Public Health England after they are released at around 4pm BST.
 
Back
Top Bottom