Yale magari ya kifahari kwenye makontena bandarini yaliishia wapi?

choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,503
2,000
Wadau habarini za usiku. Kwa siku za karibuni kumekuwa kukitokea matukio mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingne huitingisha serikali au kuikomaza zaidi.

Takribani miezi kadhaa iliyopita wakati mkuu wa nchi yetu akiwa pale bandarini ktk ziara za kushtukiza alikutana na magari ya kifahari yakiwa yameingizwa kwa njia ya kiuhujumu bila kulipia ushuru.

Ni magari mazuri ambayo nilitamani walau nimjue mwenyew maana nadhani ni miongoni mwa mafisadi wanaotufanya Tanzania tukose dawa, elimu ya uhakika, umeme, maji na mengne mengi.

Sasa hoja yangu ni je yale magari yaliishia wapi na mmiliki wake ni nani?

Nawasilisha.
 
MJJ

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
313
500
Ulitaka uletewe kwenye media tena? Watu walipandishwa mahakamani kwa ukwepaji wa kodi na taratibu za kimahakama zinaendelea. Sina akika kama uko serious kuuliza ili swali maana ni kama unataka utangaziwe maendeleo ilo tukio.

Jaribu kujiuliza wakati wa kuoa au kuolewa unaarika watu wanakunywa na kusaza Je uliwahi kushuhudia sherehe ya kuhachana?
 
Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
10,370
2,000
Kwani makinikia yameishia wapi
Tulianza kwa kuwapiga mkwara wafanyakazi wa kigeni! Wakaenda kujificha nairobi kwa wiki mbili Upepo ulipopita wakarudi!! Akaja bandarini na mkwara wa kuvunja bodi na kisha tukaoneshwa jinsi tulivyokuwa tukiibiwa kwa mafuta kushushwa bila kupimwa kwenye mita! Vyeti feki!! Kuondoa fedha za serikali kwenye benki za biashara,kushusha bei ya sukari,kupiga marufuku usafirishwaji wa makinikia! Na kikubwa zaidi Katusomesha namba!!
 
Code Breaker

JF-Expert Member
Mar 2, 2014
1,016
1,500
Kwani makinikia si yamekuwa muted na Escrow! Tuna uwezo wa kunyanyua mguu ila sio kupiga hatua.. Sakata la sukari bado ni kizungumkuti kilichosahaulika na ilihali ahueni yake imekuwa mahututi
 
choupa moting

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
1,503
2,000
Ulitaka uletewe kwenye media tena? Watu walipandishwa mahakamani kwa ukwepaji wa kodi na taratibu za kimahakama zinaendelea. Sina akika kama uko serious kuuliza ili swali maana ni kama unataka utangaziwe maendeleo ilo tukio.

Jaribu kujiuliza wakati wa kuoa au kuolewa unaarika watu wanakunywa na kusaza Je uliwahi kushuhudia sherehe ya kuhachana?

Haya ulioyasema kwenye awamu hii hayapo.
 
MJJ

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
313
500
Kwa nini wao walipokamata walienda na Media na Media ilituletea sisi bila ya wao kuzuia sisi kuletewa na Media!?

Mkuu si kweli. Unafikiria kila kinachorushwa ni wao wamesema rusheni? Kumbuka kazi ya media ni habari so wanatafuta habari.

Unajua nini mkuu labda nisaidie tunaopaswa kuwabana ni izi media maana uwa wanaleta habari hawana muendelezo wa habari kama kuna sector Ina matatizo ni media.

Wanapaswa kufuatilia kila kitu hadi mwisho wake. Wawe wanatupa kipa kinachoendelea. Ikulu ikifanya kazi kwa mfumo mnaoutaka nakuakikishia hatutasonga popote kabisa.

Magufuli ana mapungufu yake lakini ana mazuri mengi kuliko mnavyomchukulia na haijawai kutokea mtawala akasifiwa akiwa madarakani ni kawaida ya wanadamu lakini hii ya kwenu imezidi kila kitu mnapinga.
 
Apr 28, 2017
5
45
Kuna mtu alisema ulikua mpango wa kupunguza speed ya tukio la kuachishwa kazi kwa waziri wa michezo bw. Nape mnauye ndio maana kaa halina muendelezo vile
 
MJJ

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
313
500
Media wafatilie kila tukio lililopita watuletee habari kuusiana na hayo mnayosema. Tofauti na hivyo itabaki kuwa ni maneno ya wivu na mkosaji.
 
mogulnoise

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
2,367
2,000
Ulitaka uletewe kwenye media tena? Watu walipandishwa mahakamani kwa ukwepaji wa kodi na taratibu za kimahakama zinaendelea. Sina akika kama uko serious kuuliza ili swali maana ni kama unataka utangaziwe maendeleo ilo tukio.

Jaribu kujiuliza wakati wa kuoa au kuolewa unaarika watu wanakunywa na kusaza Je uliwahi kushuhudia sherehe ya kuhachana?
Mahakama gani acha ujua
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom