Yale mafunzo ya VETA yaliyotangazwa na serikali yatakuwa ya muda gani?

Napenda kufahamishwa yale mafunzo ya VETA yaliyotangazwa na serikali yatakuwa ya muda gani.

Mimi nina kadigrii kamoja lakini bado sijaona matunda yake hadi sasa, nimechoka kusikia ahadi hewa za ajira tangu enzi za mwendazake na sasa kipindi cha Bimkubwa ambapo alitaja ajira 6000 za walimu lakini sijui zimefikia wapi, naona zingine pia zinatajwa kule mjengoni kwenye kudemka.

Nimeamua nitimkie kusoma ujuzi VETA ili niweze kuyamudu mazingira ya mtaani nikiwa na uhakika wa kupata hata jero ya maji ya kunywa.

Tayari nishatuma maombi ya ujuzi wa umeme majumbani ila sijajua hayo mafunzo yatakuwa kwa muda gani ili niweze kujiandaa kisaikolojia endapo zile ajira zinazotajwa mjengoni zikitoka nisiweze kuzikosa kisa endapo nitakuwa naendelea na mafunzo ya ufundi.
 
Niliongea na jamaa 1 akasema wapo bado na mchakato maombi yalikua mengi Sana ila watatoa majina yatatangazwa na ofisi ya wazir mkuu na kwenye magazeti pia
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom