Yakudai hivi sasa Wz,bar ni nchi na sio katiba wala mafuta vilivyomo Z'bar vitajilinda wenyewe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yakudai hivi sasa Wz,bar ni nchi na sio katiba wala mafuta vilivyomo Z'bar vitajilinda wenyewe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jul 8, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by amini // 08/07/2011 // Habari // No comments

  [​IMG]Uhuru wa Tanganyika leo umekuwa wa Tanzania 9/Dec/1961,Bado smz muna tongo za macho?

  [caption id="attachment_31480" align="alignnone" width="128" caption="Nembo ya Taifa la Tanzania/Tanganyika"][​IMG][/caption]Wzanzibar hakuna isie juwa kuwa Muungano fake na ccm/smz wameifikisha nchi pabaya na kuikwamua kunahitaji Uzalendo na umoja ktk Baraza la Uwakilishi ambacho kitu hicho bado kina sua sua ktk BLW.
  Nilazima Wajumbe wa Baraza la Uwakilishi (they have to stick as one for sake of Zanzibar benefit) na hili halito fanyika kama kutakuwa na watu wataweka maslahi ya chama mbele kuliko maslahi ya Zanzibar na watu wake ambao wamekuwa muhanga wa nchi yao.
  Kama kweli SUK watakuwa na mapenzi na nchi yao na wananchi wake basi Zanzibar inaweza kuvuka katika mkondo huu, kivipi? nikusimama kizalendo na kuwacha tafauti na itikadi za chama kuwa kitu kimoja kuigombania Zanzibar for sake of Zanzibar people as all?.
  Mbona wenzetu wa Tanganyika penye maslahi ya nchi yao husimama kitu kimoja na hata kuto kujali chama wala mkataba wa Muungano unasema nini ? mimi nasema asari za sasa kuindelea Wzanzibar na Muungano huu nikubwa kuliko kuufumua upya Muungano na kulizwa watu wa pande zote husika wanataka Muungano au mfumo gani wa Muungano? hii ni haki na sio nguvu ya viongozi kutumia.
  Hivi sasa viongozi wa Bara na watu wake wa Bara wengi wanapendelea Muungano uwepo na uendelee kuwepo? lakini sehemu moja ya Muungano ambayo ni Zanzibar watu wake wengi wanataka Muungano uvunjike na usije tena?.
  Yote haya yamekuja kwa nini? kuna mambo mengi tu ambayo yanawafanya Wzanzibar wenyewe kutokuwa na imani ya Muungano huu na mfumo wake ulivyo badilika, kwanza nipale Tanganyika kuondoka ktk macho ya Muungano na badae kuja Tanzania kuchuhulikia maswala ya Tanganyika hii imeleta chaka kwa Wzanzibar kusema kufa katiba ya Tanganyika na badae katiba ya Muungano ndio inayo chuhulikia mambo ya Tanganyika yasio ya Muungano na yamungano nimoja ya chaka kubwa kuwa Muungano una kasoro na katiba ya Muungano inaleta utatanishi kwa mambo yasio ya Muungano.
  Laiti kuwa kungekuwa na Serekali 3 yani Tanganyika na katiba yake ya Tanganyika kwa maswala ya Tanganyika yasio ya Muungano basi Wzanzibar presha ingepungua kidogo na kusingekuwa na manuguniko ya kusema katiba ya Muungano inaingilia mambo yasio ya Muungano kwa Zanzibar.
  Lakini hili wenzetu ccm Bara hawalitaki hili ?. na swali jengine ni kuchukuwa mambo yote ya Zanzibar all adminisration za SMZ kuongozwa kichama na kuamuliwa kichama hata rasilimali za Zanzibar zisizo za Muungano huamuliwa kichama hili linakera sana kwa Wzanzibar wakawaida na kusubutu kusema kuwa viongozi wao wa ccm/smz ni wanafiki kwa kukubali kutii mambo yasio ya Muungano kuya sacrifice ktk mikona ya chama.
  Lakini Bara ku-sacrifice yao hawafanyi hivyo rasilimali zao na utawalawao na nafasi zao nyeti ziko vile vile bila kuasirika vyoyote, wamebadilicha tu mfumo wa Tanganyika kuja Tanzania ni jina tu lililo badilika.
  Sasa hili linawakera sana Wzanzibar na kuona viongozi wao wanatumiliwa na kujipendekeza na chama haliyakuwa mtazamo wa wenziwao sio hivyo, hivi sasa kuna mbinu kutokana na Wzanzibar kuja juu na kusema hawautaki Muungano, mbinu ilopo ni kuchukuliwa ziara za nje badhi ya viongozi wetu wa GNU ili kupunguzwa makali na kutaka Bara wapate Bless ya Muungano kutoka kwao.
  Ndio ukaona bado viongozi niwakaidi kuwaskiliza raia wa Zanzibar matakwa yao na maoni yao kitu gani wanataka?. utaona viongozi wanajitahiti kufichua kero za Muungano lakini end of that huwasisitiza Wzanzibar kuulinda na Kuuenzi kwa nguvu zote Muungano usivunjike na ukiuliza sababu kubwa utambiwa kuna Wzanzibar wafanya biashara kule Bara?.
  Mimi nasema hii sio reson strong, tukubali kuiza nchi yetu tulio pigania uhuru kwa faida ya kizazi chetu halafu tuseme tuiuze ktk mikono ya Muungano fake wa Tannganyika yenye kujita Tanzania kwa sababu ya 2% ya Wzanzibar waloko Bara au viongozi kuwa na miradi yao ya biashara? hii sio haki viongozi wanayo watendea Wzanzibar waloko ndani ya ardhi ya Zanzibar na wala sio Uzalendo.
  Kama kweli Muungano ni mzuri kama anavyosema Mh Mohammed Abudu? basi ajaribu kuwambia upande wapili kuwe na Tanganyika na katiba ya Tanganyika kwa mambo ya Tanganyika yesio ya Muungano kama vile katiba ya Zanzibar? hii itaondocha ulalamichi wa Tanganyika kujifichia mwevuli wa Tanzania kwa kuiasiri Zanzibar kiuchumi na kimaendeleo.
  Sisi Wzanzibar hatuna uchoyo na hilo ikiwa Tanganyika itasimamia mombo yake wenyewe kwa jina lake la Tanganyika mambo yao yasio ya Muungano kama vile Meneral zao Mikopo kwa jina la Tanganyika na shuhuli za miradi isio ya Muungano hapa patapunguza malalamiko, hivi sasa kuna mikopo mingi hukopwa kwa jina la Tanzania lakini ifikapo nchini hutumika kwa jina la Tanganyika, sasa Muungano ni kama urafiki nchi ngapi zimeungana na hivi sasa zimevunja Muungano wao kwa mambo haya haya ya kuto kutendeana haki au mkubwa kujifanya Super Power.
  Sasa jalia mungano uvunjike leo mikopo hii ya Tanzania italipwa na sehemu gani na itakuwa Tanzania haipo tena? hii itakuwa kugawana harama zisizo tuhusu? sasa kama wenzetu wamestik ktk Tanganyika tunajuwa mkopo utakuwa wa Tanganyika hauhusu Muungano wala Zanzibar?, jengine ni kuwa zulma za Serekali ya Tanganyika kwa jina la Tanzania.
  Zanzibar kimataifa haijulikani kuwa ni nchi, nchi ni Tanzania? hata ikitaka kwenda kuomba mikopo kuimarisha uchumi wake wa ndani wa watu wake kwa vile ina population ndogo na uchumi mdogo hua inachimtwa mpaka ipate kibali kutoka Serekali ya Tanzania kwa mambo ya nchi za nje na huambiwa Zanzibar sio nchi kimataifa na nchi ni Tanzania hata mambo ya sports tumeambiwa hivyo hivyo? lakini chakuchangaza na kujiuliza vipi viongozi wetu wanaficha marazi ambayo yatawambukiza vijukuu vyao na wao kubebe jukumu mbele ya m/mungu na laana za Wzanzibar wanazo walani?.
  Maana hakuna chaka kuwa jina Tanzania linawanufaicha sana Tanganyika kuwa ni nchi full right yakukopa mikopo popote na wakati wwt bila misuko suko wala tabu?, maana huu mwevuli wa Tanganyika kujichomeka ktk Tanzania unawapa faraja kubwa kwa mikopo ya Tanganyika, huku Zanzibar ikiambukia patupu au wasubiri kugaiwa kwa kusumbuliwa 4.5%.
  Kuna faza kwa jina la Tanzania lakini hutumika Tanganyika bila kufaidika chochote Zanzibar, mfano realway Zanzibar huambukia patupu hapa na huambiwa Zanzibar hakuna rail, lakini mkopo ni wa Tanzania ambayo Zanzibar ni Sehemu moja ya Muungano?.
  Takribani asilimia 70% ya Baget ya Tanzania husaidiwa kutoka nje sasa Zanzibar tokea enzi wao ni 4.5% au patupu, hii ni uonevu vile vile tokea Zanzibar ina population ya watu laki 8 hupewa 4.5% mpaka leo sasa hii ni choyo na uonevu wa hali ya Juu.
  Jee ikiwa Tanganyika ipo na inaomba Pesa hio kivyake na Zanzibar kivyake si kutakuwa na unafuu bila uchoyo wa kuwa tusubiri kupewa 4.5%? au ktk jumuia ya Africa mashariki Zanzibar haimo imo Tanzania /Tanganyika hii nikunyima haki na sauti ya watu wa Zanzibar ktk uchirika wa africa machariki kama Zanzibar kuwa nchi.
  Jengine ni uiano wa kazi ktk Sehemu za Balozi zetu ulimwenguni, takribani Balozi nyingi 98% kuanzia ngazi ya juu mpaka chini basi hata wafagiaji ni watu kutoka Tanganyika au ndivyo Mh Mohammed Abudu alivyo sema kuwa hatuna elimu na sifa za kuwa mabalozi Wzanzibar? mimi huyu simti akilini naona ajizalilicha na kujifezehecha ikiwa yeye kifuu sio Wzanzibar wote vifuu.
  Zanzibar ina watu kidogo lakini wasomi ni wengi kuliko Bara tukenda kwa %? lakini hili Mh Abudu halijuwi? na hawa ndio wagonjwa tulio nao Zanzibar twazidi kuwalea ndani ya BLW, yeye anahisi njia ya kuganga njaa ni kuiuza nchi alioshiwa na Baba ake?.
  Kwa hio Wzanzibar nilazima kambla ya kurekebiswa mswada mpya Tanganyika irudi ili kuja kutatua utata huu wa Muungano, sihivyo basi wenzetu watatuokota kwa magoli na kutuona Blind mazuzu, Zanzibar ina watu kidogo ukilinganicha hata na mikowa ya Tanganyika ? ina Ardhi ndogo? lakini ni nchi na hatuwezi kuwa wahanga wa Tanganyika kuza nchi yetu kutokana na udogo wetu, hatari iloko mbeleni ni viongozi wetu kama hawakuwa makini kuweka mipaka ya Muungano basi mfumo huu wa Serekali moja yani Reblic of Tanzania unaweza kuua Identity ya Zanzibar.
  Ambayo kwa njia hii au nyingine wenzetu ndio wakaikataa Tanganyika ili kujitambulicha kimataifa kuwa Tanzania ambayo ndio hio Tanganyika sisi tukafunikwa na kuvugwa vugwa viongozi wetu kwa ilani na sera.
  M/Mungu ibariki Zanzibar na kizazi chake.
   
Loading...