Yakitokea Tanganyika huwa Majambazi, Zanzibar huwa ni Uwamsho!!!

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wamevamia ofisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa King'ongo, Kimara Dar es Salaam na kupora vitu mbalimbali ikiwamo laptop na fedha Sh. 250,000.
Tukio hilo lilitokea saa 4:00 usiku wa kuamkia jana, baada ya majambazi kumjeruhi kwa rungu mlinzi wa kanisa hilo sehemu ya kichwani kisha kumfunga kamba mikononi na miguuni.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa msako wa kuwakamata waliohusika unaendelea.
Alisema majambazi wakiwa na silaha walivamia kanisa hilo na kupora baadhi ya vitu na kiasi hicho cha fedha.

Kiongozi wa usharika huo, mchungaji Joseph Kyaka, alisema alitapa taarifa za kuvamiwa kwa usharika huo saa tisa usiku kutoka kwa mmoja wa majirani na kanisa hilo.
Alisema alipofika kanisani alimkuta mlinzi akiwa amefungwa kamba sehemu za miguuni na mikononi huku akitokwa na damu sehemu za kichwani.
"Nilifika haraka kanisani na kumkuta mlinzi akiwa amefungwa kamba na mlango wa ofisi yangu na wa mhasibu ukiwa umevunjwa, laptop yangu imechukuliwa," alisema Mchungaji Kyaka.

Mlinzi wa Kanisa, Zakaria Mwangole, alisema walifika majambazi saba waliobeba silaha mbalimbali mmoja akiwa na bunduki, wakamvamia, wakamfunga kamba, wakamlaza chini na kuanza kubomoa milango ya ofisi ya mchungaji na mhasibu.
Shuhuda wa tukio hilo, Mlunge Macha, alisema alisikia kishindo eneo la kanisani, muda mfupi akasikia mlio wa risasi mbili zikipigwa hewani na kelele za mlinzi

Written by Wamtambwe // 05/02/2013 // Habari //
 
Sawa, uhusiano uliopo ni kwamba, Viongozi wa uamsho walikamatwa baada ya watu kuvamia Makanisa, kupora mali za Kanisa, kuchoma moto na kupora vilabu vya pombe na kunywa pombe yote! sasa hao wanatofauti gani na hao majambazi yaliyovamia Makanisa na kupora huku bara?

La kuchekesha badala ya Polisi kuwasaka hao Majambazi yaliyoiba na kunywa Pombe za watu walienda majumbani kwa Viongozi wa Uamsho na kuwatia mbaroni Mashehe hao! Jamani ni lini Shehe amekuwa mporaji na mwizi wa pombe na kuinywa kabisa kilevi hicho haramu?
 
wewe zubeda unawaza kwa ku2mia kiungo chako gani?mbona hujagusia kuchomwa makanisa mbagala?ma2kio ya uhalifu yenye mkono wa kidini yanajulikana na yaujambazi wa kawaida yanafahamika so usi2letee hoja-pumba kama hii tena....kajadili na v-laza wenzako wa mzalendo.
 
kwani majambaz uwa wanachoma makanisa? wanaochoma makanisa ni uamsho na wale wenye misimamo mibaya,,bara majambaz uwa wanaiba ela
 
wewe zubeda unawaza kwa ku2mia kiungo chako gani?mbona hujagusia kuchomwa makanisa mbagala?ma2kio ya uhalifu yenye mkono wa kidini yanajulikana na yaujambazi wa kawaida yanafahamika so usi2letee hoja-pumba kama hii tena....kajadili na v-laza wenzako wa mzalendo.

Mimi sina muda wa kutukanana na wewe hiyo ni tabia yenu ya ukosefu wa maadili! Kuhusu uchomwaji wa Makanisa ya Mbagala hakuna anaeunga mkono uhalifu wa aina yoyote! Lakini mbona wale Mashehe waliokamatwa na tuhuma za uhalifu huo wamefunguliwa kesi nyingine tofauti na hayo bali wanatuhumiwa na uvamizi wa Mali ya Bakwata!

Hata na dhamana ambayo kikatiba ni haki yao wamekataliwa!

Si ni Kizungumkuti hicho!
 
hizi kesi unafuatilia au unahadithiwa?hapo kuna kesi mbili
1. waliovamia chang'ombe markazi(kina ponda)
2. walochoma makanisa mbagala.(Hawana umaarufu sana)

kuna swali mpaka hapo?
 
Si kweli kwani wote walikamatwa siku moja na kesi kufunguliwa ya aina moja! ila baada ya kuwaachilia watuhumiwa 48 kwa dhamana, kesi ikabadilishwa kwa akina Ponda na kuwa uhalifu wa kuvamia mali za Bakwata!
 
We kweli ni zuzu, beda! Kwani baada ya kuiba je wamechomaa? Unaonekana unatumia kiungo cha kati kufikiri!
 
wewe zubeda unawaza kwa ku2mia kiungo chako gani?mbona hujagusia kuchomwa makanisa mbagala?ma2kio ya uhalifu yenye mkono wa kidini yanajulikana na yaujambazi wa kawaida yanafahamika so usi2letee hoja-pumba kama hii tena....kajadili na v-laza wenzako wa mzalendo.

Mkuu tuende taratibu. Hao wanaosadikiwa kuchoma makanisa mbagala ambao inadaiwa ni waislamu je,walishakamatwa na kufikishwa mahakamani? Nauliza tu.
 
angalia comment zangu za juu nimeweka link utapata jibu la swali lako.
 
Back
Top Bottom