Yajue masharti ya kufuga njiwa: Hawapendi Umbea na Ulevi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,249
21,345
Ukiachana tofauti ya bei ya njiwa huanzia elfu 10 pair moja ya njiwa Wa kawaida, elfu 60 kwa wale weupe, na wengine wapo wanauzwa hadi laki 8 kwa pair moja!

(Kazi moja ya njiwa ni urembo,burudani,kitowewo na baraka)

Kabla ya kufuga njiwa hao ni vyema sasa kutambua masharti yao;
  1. Kwanza kabisa njiwa ukiwanunua kutoka kwa mtu, sharti wawe wawili pair (dume na jike)
  2. Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu, hakikisha unakowapeleka uwaandalia banda la juu, ukiwaweka banda la chini wanaondoka
  3. Kama banda lako la chini, tafta muuzaji mwenye banda chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.
  4. Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili, hawapendi masimango wataondoka!
  5. Ukifuga njiwa nao hufatilia nyendo zako, ukiwa mlevi hawakai wanaondoka kwasababu wanaamini mlevi anaweza sahau kuwafungulia bandani siku moja
  6. Njiwa wana nguvu kiimani, hawapendi mfugaji awe mmbeya kugombana na majilani, kwasababu wakati Wa ugomvi njiwa hukaa juu ya paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena
  7. Njiwa hawapendi kuona Umechinja njiwa mwenzao mbele yao, wakiona wanahama wote kwasababu wanahisi utawachinja.
  8. Njiwa hawapendi Makelele ya kushtukiza kama honi Kali, kuwarushia jiwe na miziki mikubwa, ukifanya hivyo wanahama
  9. Njiwa akifa mmoja, huomboleza, unashauliwa umtaftie mwenza haraka kwa njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka
  10. Hakikisha njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga, wakipararuliwa huondoka mazima.
  11. Njiwa wanaofugwa banda la uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwasababu ya mazingira tulivu
  12. Hakikisha pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako! njiwa hawapatani na paka pori la sivyo wanahama wote!
  13. Inasemekana njiwa ni Wa pili kwa wivu baada ya nyegele! Hakikisha unafuga wawiliwawili.
Hayo ni machache tu kati ya masharti ya njiwa!!!
Screenshot_20190519-104257.png
 
Kama kuna tukio nyumbani kwako au kwa jirani wa karibu, mfano harusi, msiba au sherehe yoyote wajulishe, wakistukia tu watu nyomi, mziki huo au vilio wanasepa wote.

Kuna bibi mmoja aliwafuga wengi na kuwapa taarifa kama kuna tukio nyumbani kwake au kwa majirani, sasa alifiwa na mwanae wa Dar kutokana na uchungu akasahau kuwaambia, siku ya msiba hawakutoka ila siku ya pili alikuta banda tupu. Afu sijui huwa wanaenda wapi maana hupotea tu.
 
Wengine hutafta mabanda ya karibu wakiona wenzao ndio wanaitwa mateka kama una moyo mdogo waweza usiwafuge hawasemwi vibaya kama kuku au mfugo mwengine wanapenda kupeana romance s mchezo
Kama kuna tukio nyumbani kwako au kwa jirani wa karibu, mfano harusi, msiba au sherehe yoyote wajulishe, wakistukia tu watu nyomi, mziki huo au vilio wanasepa wote. Kuna bibi mmoja aliwafuga wengi na kuwapa taarifa kama kuna tukio nyumbani kwake au kwa majirani, sasa alifiwa na mwanae wa Dar kutokana na uchungu akasahau kuwaambia, siku ya msiba hawakutoka ila siku ya pili alikuta banda tupu. Afu sijui huwa wanaenda wapi maana hupotea tu.
 
🤣:D:D wanahamia sehemu tulivu au popote watakapoona njiwa wenzao! lakini siku moj moja hurudi kuchungulia
 
Kama kuna tukio nyumbani kwako au kwa jirani wa karibu, mfano harusi, msiba au sherehe yoyote wajulishe, wakistukia tu watu nyomi, mziki huo au vilio wanasepa wote. Kuna bibi mmoja aliwafuga wengi na kuwapa taarifa kama kuna tukio nyumbani kwake au kwa majirani, sasa alifiwa na mwanae wa Dar kutokana na uchungu akasahau kuwaambia, siku ya msiba hawakutoka ila siku ya pili alikuta banda tupu. Afu sijui huwa wanaenda wapi maana hupotea tu.
Du wana visa si mchezo.
 
Nyongeza:
Hawapendi kusikia sauti za mahaba/za kubanjuana toka kwa binadamu.
Inashauriwa kuweka banda lao mbali na vyumba vya watu wazima ambao daily wanagegedana tena kavukavu.
Usipofanya hivyo njiwa .......sana na kushindwa kupata muda wa kula na hatimaye kufa wote kwa njaa!!
 
Nyongeza:
Hawapendi kusikia sauti za mahaba/za kubanjuana toka kwa binadamu.
Inashauriwa kuweka banda lao mbali na vyumba vya watu wazima ambao daily wanagegedana tena kavukavu.
Usipofanya hivyo njiwa watatomb@n@ sana na kushindwa kupata muda wa kula na hatimaye kufa wote kwa njaa!!
Duuuuh
 
Kama kuna tukio nyumbani kwako au kwa jirani wa karibu, mfano harusi, msiba au sherehe yoyote wajulishe, wakistukia tu watu nyomi, mziki huo au vilio wanasepa wote. Kuna bibi mmoja aliwafuga wengi na kuwapa taarifa kama kuna tukio nyumbani kwake au kwa majirani, sasa alifiwa na mwanae wa Dar kutokana na uchungu akasahau kuwaambia, siku ya msiba hawakutoka ila siku ya pili alikuta banda tupu. Afu sijui huwa wanaenda wapi maana hupotea tu.
Naiskiaga hii tu toka kitambo mkuu, kumbe kuna zaidi ya hii ya kujulishwa msiba ingawa mimi nilisikia kuwa usipowajulisha msiba wanazira kula! Si kuondoka
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom