Ukiachana tofauti ya bei ya njiwa huanzia elfu 10 pair moja ya njiwa Wa kawaida, elfu 60 kwa wale weupe, na wengine wapo wanauzwa hadi laki 8 kwa pair moja!
(Kazi moja ya njiwa ni urembo,burudani,kitowewo na baraka)
Kabla ya kufuga njiwa hao ni vyema sasa kutambua masharti yao;
(Kazi moja ya njiwa ni urembo,burudani,kitowewo na baraka)
Kabla ya kufuga njiwa hao ni vyema sasa kutambua masharti yao;
- Kwanza kabisa njiwa ukiwanunua kutoka kwa mtu, sharti wawe wawili pair (dume na jike)
- Kama muuzaji aliwafuga kwa banda la juu, hakikisha unakowapeleka uwaandalia banda la juu, ukiwaweka banda la chini wanaondoka
- Kama banda lako la chini, tafta muuzaji mwenye banda chini ndipo ununue vinginevyo unashauliwa uwanyonyoe manyoya na kuwafungia siku 40 kabla ya kuwafungulia.
- Njiwa wakiwa mbele yako usipende kuwajadili, hawapendi masimango wataondoka!
- Ukifuga njiwa nao hufatilia nyendo zako, ukiwa mlevi hawakai wanaondoka kwasababu wanaamini mlevi anaweza sahau kuwafungulia bandani siku moja
- Njiwa wana nguvu kiimani, hawapendi mfugaji awe mmbeya kugombana na majilani, kwasababu wakati Wa ugomvi njiwa hukaa juu ya paa wakisikiliza halafu huondoka na hawarudi tena
- Njiwa hawapendi kuona Umechinja njiwa mwenzao mbele yao, wakiona wanahama wote kwasababu wanahisi utawachinja.
- Njiwa hawapendi Makelele ya kushtukiza kama honi Kali, kuwarushia jiwe na miziki mikubwa, ukifanya hivyo wanahama
- Njiwa akifa mmoja, huomboleza, unashauliwa umtaftie mwenza haraka kwa njiwa anaebaki la sivyo wanaondoka
- Hakikisha njiwa huwachanganyi na kuku mwenye vifaranga, wakipararuliwa huondoka mazima.
- Njiwa wanaofugwa banda la uani/nyuma/jikoni huzaliana haraka zaidi kwasababu ya mazingira tulivu
- Hakikisha pakashume hawazoei kufika nyumbani kwako! njiwa hawapatani na paka pori la sivyo wanahama wote!
- Inasemekana njiwa ni Wa pili kwa wivu baada ya nyegele! Hakikisha unafuga wawiliwawili.