Yajue makosa yaliyoainishwa kupitia Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
7jh.png

SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAO,
Sheria ya makosa ya mtandao imetungwa 2015, Sheria hii inahusu makosa yanayohusiana na mifumo ya kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA); na uchunguzi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na unaohusiana na hayo.

Vipengele muhimu na athari zake kwa tasnia ya habari ni pamoja na:

Makosa na Adhabu
Vifungu vya 4-29 vinaeleza kuhusu makosa na adhabu kuhusiana na mifumo ya kompyuta [kifaa au mchanganyiko wa vifaa, ikijumuisha mtandao, vifaa vya kuingizia na vya kutolea na ambavyo vinaweza kutumika pamoja na majalada yaliyo na programu za kompyuta, maelezo ya kielektroniki, data za kuingizia na data za kutolea zinazotunza data za hesabu zilizo na mantiki na udhibiti wa utolewaji wa mawasiliano na majukumu mengine] na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA). Makosa yanajumuisha kupata, kuingilia, kumiliki, kukwepa mawasiliano isivyo halali, na kuingilia mfumo wa komyuta au taarifa (data).

Vifungu vya 13 na 14 kwa ujumla vinazuia uchapishaji wa picha za ngono zinazohusisha watoto wadogo na watu wazima (ponografia).

Kifungu cha 16 kinazuia uchapishaji wa taarifa au data ya uongo, ya kilaughai, yenye kupotosha au isiyo sahihi kwa nia ya kukashifu, kutishia, kutukana, au kupotosha jamii kwa namna yoyote.

• Kifungu cha 20 kinaainisha makosa kwa kusambaza, au kurusha au kusambaza tena taarifa zinazotumwa bila ridhaa, au kughushi taarifa za utambulisho na kuzituma bila ridhaa, yaani taarifa au data za kielektroniki ambazo hajaikuombwa na mpokeaji.

• Kifungu cha 23 kinazuia kutumia mawasiliano ya kielektroniki kwa lengo la kulazimisha, kunyanyasa, au kusababisha madhara ya kiakili kwa mpokeaji.

Mamlaka ya Polisi
• Kifungu cha 31 kinawapa mamlaka polisi au watekelezaji wa sheria wanaosimamia kitu cha polisi au wenye cheo kinachofanana kutoa amri inayoruhusu kuingia, kupekua, au kutwaa vifaa na mifumo ya kompyuta, na kutwaa data au taarifa zilizohifadhiwa kwenye kompyuta, iwapo watajiridhisha kwamba kuna sababu za msingi kuamini kwamba mfumo huo wa kompyuta unaweza kutumika kama sehemu ya ushahidi kwa husika au ni matokeo ya kosa hilo.

• Kwa mujibu wa Kifungu cha 32, afisa wa utekelezaji sheria anaweza kumtaka mtu anayemiliki data au taarifa zinazohitajika katika uchunguzi wa makosa au uendeshaji wa mashauri ya jinai kuweka wazi taarifa hizo.

• Kifungu cha 34 kinawapa mamlaka maafisa wa polisi kumtaka mtu anayemiliki taarifa au data zinazohitajika kwa ajili ya uchunguzi kuweka wazi, kukusanya, au kurekodi mwenendo wa taarifa au data za mawasiliano ya aina fulani, au kumruhusu na kumsaidia afisa wa utekelezaji sheria kukusanya au kurekodi taarifa hizo. Taarifa au data hizo ni zile zinazoonesha chanzo, mwisho, njia, na muda wa mawasiliano husika.

• Chini ya Kifungu cha 35, polisi wanaweza kutoa amri ya kukusanya, kurekodi, kuruhusu au kusaidia mamlaka sahihi kukusanya au kurekodi data au taarifa yenye maudhui yanayoainisha mawasilianofulani ikiwemo matumizi ya njia za kiufundi, kitaalam au kiteknolojia. Kifungu cha 37 kinaruhusu polisi kutumia kifaa cha uchunguzi katika kukusanya data au taarifa kwa ruhusa ya mahakama, mwanzoni kwa muda wa siku kumi na nne .

Wajibu wa Watoa Huduma
• Kifungu cha 39 kinazuia watoa huduma kufuatilia data au taarifa anayoisambaza au kuihifadhi, au kutafuta taarifa za viashiria vya shughuli zinazohusisha uvunjaji wa sheria. Waziri (mwenye dhamana ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano) anaweza kuwataka watoa huduma kuziarifu mamlaka kuhusu shughuli zozote zinazodaiwa kuhusisha uvunjanji wa sheria au kutoa taarifa zinazoanisha watumiaji kwa mamlaka husika pindi wanapoombwa kufanya hivyo.

Notisi ya Kuondoa Taarifa
Kifungu cha 45 kinasema kwamba mtu anaweza, kupitia notisi ya kuondoa maudhui, kumuarifu mtoa huduma kuhusu data, taarifa, au shughuli inayomnyima mpokeaji au mtu mwingine haki ya huduma, vitu au shughuli ambayo ni kinyume cha sheria, au suala lolote linalotekelezwa au kutolewa kinyume cha sheria. Mtoa huduma analazimika kuchukua hatua kuhusiana na notisi ya kuondoa maudhui atakayoipokea.

Mamlaka ya TCRA
4 (1) (a) kinaitaka TCRA kuwa na rekodi ya wachapishaji blogu, majukwaa ya mtandaoni, redio na televisheni za mtandaoni. Usajili wa wachapishaji blogu na majukwaa ya mtandaoni ni kinyume na matakwa ya intaneti iliyo bure na wazi, na itakuwa na athari kubwa kwa uhuru wa kujieleza, maoni na maongezi ambapo itasababisha kuongezeka kwa uwoga wa kufanya haya kwa wananchi.

4 (1) (b) kinazipa nguvu kubwa mamlaka husika kuchukua hatua dhidi ya wasiofuata taratibu hizi, ikiwa ni pamoja na kuamuru uondolewaji wa “maudhui yaliyokatazwa”.

JamiiTalks
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom