Yajue makao makuu ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Yafuatayo ni makao makuu ya baadhi ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani. Nchi hizi zina sera za uwazi juu ya hizi Mambo kwa hapa kwetu nadhani Mambo haya ni Siri ndio maana nimeepuka makusudi kuyataja ili pia yasikonflict na sheria za jamiiforums.

1. CIA HQ ipo Langley Virginia na jengo lake limepewa jina la George Bush center for intelligence.

2. FSB HQ la urusi lipo mtaa wa lubyanka na jengo linaitwa lubyanka Moscow.

3. MI6 HQ la uingereza lipo vauxhall cross bridge pembeni ya mto thames.

4. Mossad HQ ipo Jerusalem karibu na mtaa ambapo pia ndio makao makuu ya makazi ya waziri mkuu was Israel. Mtaa wa Beit Aghion.

5. BND kirefu chake ni Bundesnachrichtendienst lipo Berlin. Pia ndio shirika la ujasusi lenye majengo mengi kuliko yote duniani.

Waweza ongezea uyajuayo.
 
Yafuatayo ni makao makuu ya baadhi ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani. Nchi hizi zina sera za uwazi juu ya hizi Mambo kwa hapa kwetu nadhani Mambo haya ni Siri ndio maana nimeepuka makusudi kuyataja ili pia yasikonflict na sheria za jamiiforums....
2.FSB HQ la urusi lipo mtaa wa lubyanka na jengo linaitwa lubyanka Moscow.

Panaitwa- --Seven Hills Lubyanka, Moscow.
 
Napenda kujua tofaut Kati Ya CIA, FBI na SWAT

CIA, Central Intelligence Agency hii inahusika sana na usalama wa taifa la Marekani hususani rais.

FBI, Federal Bureau of investigation hii inahusika na uchunguzi sana wa matukio yanayotekea ndani ya Marekani.

SWAT, Special weapons and tactics hii hutumika kwenye matukio yanayohusu vitisho vya magaidi na matukio makubwa ambayo yanazidi polisi wa kawaida wa Marekani.

Bonus
DEA, Drug enforcement administration inahusika na kupambana na madawa ya kulevya ndani na nje ya Marekani
 
Back
Top Bottom