Yajue majeshi yetu na maana halisi ya neno"mwanajeshi"

Nyakibimbili

Senior Member
May 4, 2019
185
287
Tumsifu yesu kristu.

Tanzania tunayo majeshi mbali mbali ya ulinzi na usalama hapa nitainukuu katiba ya jamhuri,,,,,,,Ibara ya 147 (1) Ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, Isipokuwa serikali kuunda au kuweka Tanzania jeshi la aina yoyote.

(4)kwa madhumuni ya ibara hii ,MWANAJESHI"maana yake ni askari aliyeajiriwa kwa mashariti ya muda au ya kudumu katika jeshi la ulinzi,jeshi la polisi, jeshi la magereza au jeshi la kujenga taiga.

Nimeamua kufanya hivi ili kutoa elimu kwa watu mbali mbali ambao wamekuwa wakichanganya mambo yahusuyo majeshi,,kwa mfano unakuta mtu anaripoti tukio anasema "walikuwepo wanajeshi na askari" katika maana halisi hakuna kitu kama hicho,,, askari wa majeshi yote nchini ni "wanajeshi" isipokuwa kila mwanajeshi ana jeshi lake mfano Jwtz,polisi,magereza au jeshi la kujenga taifa.

Twende mbele zaidi tuone maana ya askari kwa mujibu wa katiba "askari" likitumika kuhusiana na jeshi lolote, maana yake ni pamoja na askari yeyote ambaye kwa mujibu wa amri ya jeshi hilo ni mtu anayewajibika kinidhamu;
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom