Yajue maeneo matano duniani ambapo ndege haziruhusiwi kuruka juu yake

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,454
154,316
1. Antarctica:
Antarctica inajulikana sana kwa hali yake ya baridi kali sana ambapo barafu na theluji hulifunika eneo hili kwa mwaka mzima.
Eneo hili lina nguvu kubwa sana ya usumaku ambapo huweza kuathiri mifumo ya ndege na hivyo kuisababishia hatari ya kuanguka.

1613117485466.png



2. The Bermuda Triangle:
Kwa miaka mingi eneo hili limekuwa likijulikana zaidi kwa matukio ya ndege na meli kupotea kimaajabu mara zipitapo eneo hili.
Wanacho fanya marubani ni kuhakikisha wanalikwepa eneo hili lenye vimbunga vya hatari na pepo za kutisha sana.

1613118635335.png


3. Buckingham Palace:
Hii ni kasri na makazi ya Malkia na utawala wa Kifalme wa Uingereza. Ndege haziruhusiwi kuruka juu ya anga hili kwa sababu za kiusalama.

1613117863771.png


4. Disney Theme parks:
Hili eneo lina upekee wa kipekee duniani; nyumbani kwa kina Mickey Mouse na vikaragosi vingine vingi ambavyo watu wote duniani hupenda kuviangalia kipindi Cha ukuaji wetu.

Eneo hili liko Florida na California na limekuwa kivutio kwa wageni wengi ambao wamekuwa wakilitembelea kwa kipindi chote cha mwaka mzima.

Ndege haziruhusiwi kupita juu ya anga hili kwa ajili ya usalama wa wageni wanaitembelea eneo hili.

1613118728776.png


5. Mecca:
Ndege haziruhusiwi kuruka kwenye hili anga takatifu kwasababu ya ukuu na utakatifu wake. Kwenye nguzo za Uislam ni lazima japo mara moja maishani, Muislamu aje mahali hapa kufanya ibada ya hija.

1613121280354.png
 
Ndege zinapita sana tu juu ya kilele na watalii wanafurahia sana...ingekuwa ni kweli sasa wale wanaopanda si wangekuwa hawarudi
Nasikia kuna ndege ya watalii ilinasa hapo walikuwa wanapiga hapo picha eti ikavutwa na sumaku alafu ikafunikwa na barafu
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom