Yajue Madhara ya Vipodozi vyenye Kemikali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,303
atharivipodozi.jpg


Zaidi ya asilimia 52 ya wanawake hutumia vipodozi vyenye sumu ambavyo huwasababishia matatizo mbalimbali ikiwamo kansa ya ngozi, figo pamoja na kuharibika kwa mimba kwa mama mjamzito. Aidha katika utafiti uliofanywa na Asasi isiyokuwa ya kiserikali Envirocare mwaka jana inaonyesha mikoa ambayo imeathirika zaidi na matumizi ya vipondozi hivyo ambayo ni Tanga, Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha, Mbeya na Kilimanjaro.

Meneja wa Mradi huo, Elfansia Shayo, alisema Envirocare imeandaa kampeni kwaajili ya kupinga matumizi ya vibodozi hivyo itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam. "Envirocare kwa kushirikiana na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imefanya utafiti ulionyesha zaidi ya asilimia 52 ya watumiaji wa vipodozi hivyo ni wanawake na baadhi yao wanajua madhara yake," alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi hiyo, Loyce Lema, alisema kampeni hiyo inahusu kutoa elimu kwa jamii kuhusu matumizi ya vipodozi hivyo na ambazo viambato hivi husababisha madhara kwa watumiaji na mazingira. Alisema pamoja na TFDA kuweka mfumo thabiti wa udhibiti wa vipodozi ambao unatumia njia mbalimbali ikiwamo usajili wa vipodozi, utoaji wa vibali vya biashara, na ukaguzi wa maduka bado mfumo huo unachangamoto kwani vipodozi vimekuwa vikiingizwa nchini kwa kutumia njia zisizo rasmi.


Tathmini kuhusu usalama wa vipodozi kwa bahati mbaya hufanyika wakati tayari vipodozi viko sokoni na vinatumiwa na binadamu.

Nchini Marekani Mamlaka ya Udhibiti wa Vyakula na Dawa (The U.S Food and Drug Administration - FDA) hufanya majaribio ya kimaabara kwa vipodozi ambavyo vimelalamikiwa na wateja na kufunguliwa shauri la kisheria. Kinyume na hapo hakuna!

Aidha, inachukua miaka mingi mpaka kufikia huo mchakato kwa mamlaka hiyo kuzishauri mamlaka za kisheria kutoa idhini ya kuanza kufanyika majaribio hadi kuyapiga marufuku makampuni yanayozalisha vipodozi vinavyolalamikiwa. Hivyo kutokana na kadhia hiyo FDA mara nyingi hufanya mashauriano na makampuni hayo ili ama yasitishe kuzalisha vipodozi hivyo au yabadiri formula inayotumiwa kuzalisha vipodozi hivyo. Hii yote ni kukwepa mlolongo mrefu wa kisheria.

FDA imekadiria kwamba ni asilimia 3 tu ya wasambazaji wakubwa wa vipodozi wapatao 4,000 na 5,000 ndo wamewahi kutoa taarifa kuhusu madhara ya baadhi ya vipodozi vilivyolalamikiwa na watumiaji. Yaani asilimia 97 wala hawatoi taarifa na wanasambaza vipodozi vingine vikiwa na sumu. Sasa kama US hali iko hivyo hapa Tanzania si tuna hali mbaya sana!

Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Tanzania (TFDA) kimsingi huwa inafuatilia ripoti za WHO na nchi zilizoendelea kuhusu vipodozi vilivyopigwa marufuku. Ndio maana wakipata ripoti ndio wanahangaika na operesheni za kushtukiza za kukagua maduka ya vipodozi. Usalama wetu uko wapi?

Nisiwaache bila kuwapa habari kuhusu madhara ya kemikali mbili japo zipo nyingi zenye madhara kwa binadamu. Kemikali hizo ni 1,4-Dioxane na Phthalates. Ukiangalia label kwenye chupa ya vipodozi iwe ni toner, shampoo, cleanser, conditioner, mafuta ya nywele, baby lotion, soaps, etc hutoona imeandikwa 1,4-Dioxane kama kiambata (ingredient).

Ni kwamba sumu hiyo ipo katika vipodozi vingi. Ukiona kwenye lebel kuna viambata vyenye majina yenye herufi..eth…ujue kiambata hicho kinatengeneza sumu ya 1,4-Dioxane kwenye vipodozi hivyo ulivyonavyo. Mathalani Sodiumm laureth, Polyethyleneglycol, Oleth, Myreth, Ceteareth, nk.1,4-Dioxane inaitwa ‘Silent Killer' na husababisha saratani (Cancer). Sasa chunguza labels za vipodozi ulivyonavyo je kuna ambavyo vina viambata vyenye majina yenye eth?

Nakuja kwenye sumu ya pili – Phthalates. Asilimia 80 ya vipodozi kufuatia utafiti uliofanywa na Women's Environmental Network, Swedish Society for Nature Conservation and Health Care Without Harm, vina sumu aina ya Phthalates.

Unataka kujua harufu ya hiyo sumu? Egesha gari lako juani kwa masaa kadhaa ukiwa umefunga milango na vioo vyote. Then nenda kafungue mlango, harufu utakayosikia ndio hiyo sumu! Hiyo sumu inatoka kwenye dashboard na viti vya gari yako (plastics). Hii ndio maana baadhi ya madaktari wanashauri wanawake wajawazito ama wasinunue magari mapya au wasipande magari hayo hususan katika kipindi cha wiki chache za kwanza za ujauzito. Kwa nini…nitaeleza!

Mwaka 2000 University of Puerto Rico katika utafiti wake ilihusisha sumu ya Phthalates katika vipodozi na kuwahi kubalehe kwa mabinti. Usishangae siku hizi vibinti vinabalehe vikiwa katika umri mdogo sana. Sasa akina mama wajawazito mnaotumia vipodozi vyenye hiyo sumu jueni mnahatarisha afya za watoto wenu wa kiume ambao bado hawajazaliwa (unborn baby boys).

Sumu hiyo inahatarisha ukuaji kamilifu wa pumbu za watoto wa kiume, madhara yake ni low sperm count, upungufu wa nguvu za kiume (sexual dysfunction) na hormonal imbalance! Unakuta katoto ka kiume kanajisikia zaidi kuwa ka kike kuliko ka kiume!!! Ushoga ndo namaanisha!

Siku hizi pia tatizo la nguvu za kiume linazidi kila siku ienda! Kijana wa miaka 20 tu anaanza kutafuta madawa ya kuongeza nguvu za kiume…je akifikisha 40? Halafu matatizo haya yanashika kasi mijini kuliko vijijini…Hatujiulizi why?! Matatizo ndo kama haya ya vipodozi na aina ya vyakula plus our life style!

Mwaka 2007 University of Rochester School of Medicine, New York ilifanya utafiti kuhusu sumu hiyo na kugundua kuwa inaleta adnominal obesity kwa wanawake!

Hatushangai siku hizi lipo ongezeko la wanawake wenye vitambi na ndevu? Hiyo ni afya au matatizi! Na sisi wanaume hatuko salama na hiyo sumu maana tunatumia pia vipodozi vyenye hiyo sumu.

Halafu hata hizi MP3 player earphones zina hiyo sumu. Siku hizi ni fasheni kutembea na nazo muda wote. Pamoja na kwamba zinaleta tatizo la usikivu baada ya matumizi ya muda mrefu pia check nguvu za kiume… wanaume tunahitaji kufunga magoli na ufundi haswa.

Ngoja niwambie jambo la mwisho kwa leo.

Vipodozi vinavyouzwa katika nchi za Ulaya havina sumu hizo kwa kiwango kama vile vinavyouzwa nchi za Afrika! Aina ni ile ile ya vipodozi lakini kwao mambo safi kwetu tunatupiwa uchafu wa vipodozi. Why? Kwa sababu sheria na kanuni zinazosimamia vipodozi zimekaza…sisi kwetu legelege! Kama sio legelege…fake fake kwa kila bidhaa huku kwetu yatoka wapi?

Next time nitaongelea madhara ya hizo mnazopaka kwenye makwapa ili kukata jasho. Hatutaki kunuka vikwapa je hizo antiperspirants ni salama kwa afya zetu? Mind you sipingani na biashara za watu za hivyo vipodozi bali tunaelemishana tu.


Use At Your Own Risk!



Aina nyingi ya vipodozi vya viwandani (synthetic beauty products) vimetengenezwa kwa viambato (ingredients) vyenye sumu (toxins) ndani yake. Sumu hizi huleta uharibifu kwenye ini na pia huleta saratani (liver-damaging and cancer causing toxins) vinapotumiwa kwa muda mrefu.

Kadhalika vipodozi vya viwandani hutengenezwa kwa viambata vinavyosaidia ufyonzaji wa vipodozi ndani kabisa ya ngozi kwa lengo la kuleta uzuri wa ngozi uliokusudiwa kwa mujibu wa kampuni husika ya vipodozi. Viambata hivi ambavyo kitalaam huitwa ‘penetration enhancers/sorption promoters/accellerants' ni pamoja na alcohol (ethanol), glycols (propylene glycol), sulfactants, nk.


Sasa mtumiaji wa vipodozi hivi anapopaka kwenye ngozi sumu hupenya ndani ya ngozi na kusafirishwa kwa njia ya damu kwenda kwenye viungo vya ndani (internal organs). Mwilini uchujaji hufanyika ambapo ini huusika na hutolewa nje (flushed out) ya mwili na figo. Hata hivyo baadhi ya sumu hubaki mwilini na huendelea kuongezeka kiwango chake kadiri tunavyoendelea kutumia vipodozi.

Kwa vile ngozi ndio kiungo kikubwa katika miili yetu sumu nyingi kukaa ndani ya ngozi. Ndani ya miili yetu sumu hizi kuchangamana na kemikali za asili za miili yetu na kusababisha mabdiriko ya ukuaji wa chembe chembe za miili yetu hali inayopelekea saratani. Madhara mengine ya kiafya yanayosababisha na vipodozi vya viwandani ni pamoja na mzio (allergies), kutokupata ujauzito (infertility), kuzeeka kabla ya wakati (aging prematurely), diabetes, na mengineyo ikiwa ni pamoja na wanawake kuota ndevu! Siku hizi kuna ongezeko kubwa la wanawake kuota ndevu…

Tuwe makini na utunzaji na kujali ngozi za miili yetu. Vipodozi vya viwandani ni hatari wandugu zangu. Ngozi ya binadamu kiasi cha ‘square inch' ina sweat glands 650, blood vessels 20, chembe chembe 60,000 zinazotengeneza rangi ya ngozi na zaidi ya 1,000,000 ya nerve endings. Ngozi ina midomo mingi (skin pores) iliyo tayari tayari kula chochote kinachogusana na ngozi kama vile vipodozi. Hapo ndo uone jinsi gani ngozi inapaswa kuangaliwa sana!

Katika zama zetu hizi zipo zaidi ya aina 100,000 za kemikali zinazotumika kutengeneza aina mbalimbali ya bidhaa tunazotumia kama vile rangi na vipodozi. Bahati mbaya sana ni asilimia 5 tu ya kemikali hizo zimefanyiwa majaribio ya kimaabara ili kujua madhara yake kwa afya ya binadamu. Hii ina maana asilimia 95 ya kemikali hizo bado hazijafanyiwa majaribio ya kitalaam na tunazitumia kupitia vitu kama vipodozi. Mathalani zebaki (mercury) ilikuwa ikitumika katika vipodozi kwa muda mrefu mpaka hivi karibuni ilipopigwa marufuku baada ya kufanyika utafiti kuhusu madhara yake.

Jambo jingine baya ni kwamba majaribio kuhusu athari za viambata vilivyomo katika vipodozi kufanywa kwa wanyama kama vile panya. Hakujawahi kufanywa majaribio hayo kwa binadamu ambaye ndiye mtumiaji! Halafu kuna makampuni mengine wanatufanyia hujuma za makusudi. Yanatengeneza vipodozi kwa viambata ambavyo havijafanyiwa majaribio halafu hawaanzi kuviuza huko kwao bali wanavileta Afrika.

Halafu wanafuatilia matokeo ya vipodozi vyao kwenye miili ya waafrika. Kwa nini wanatumia miili yetu? Kwanza wao ni wabaguzi wa rangi, pili sheria na kanuni zetu ama ni dhaifu au hazisimamiwi ipasavyo na mamlaka husika za Serikali.

Kwa leo na-stop hapa ndugu zangu, sasa mwenye sikio la kusikia asikie. Sifanyi kampeni ya kuzuia watu kutumia vipodozi vya viwandani au kuzuia biashara za watu au makampuni! Keep using at your own risk! Kwa yeyote atapenda kuelekezwa namna ya kutengeneza vipodozi uwasiliane kupitia


Email: alex.peter_75@yahoo.com

Mob: +255 688 308840



mkorogo.jpg

"Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini."Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha." Euphrasia Shayo

KWA UFUPI
Kuna watu ambao hujitoa mhanga kwa vipodozi vilivyopigwa marufuku ilimradi wanaamini wakivitumia wanapendeza zaidi mbele ya macho ya watu na kupendwa.

Nuru Masoud, mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, amekuwa akijishughulisha na biashara za vipodozi vya asili, maarufu kama mkorogo.

Hata hivyo, biashara hiyo aliisitisha mwaka 2013 baada ya kupata madhara makubwa ya ngozi ambayo yaliambukiza pia familia yake.

"Nilianza kuwashwa ngozi mfululizo, nikadhani nimeathirika na Ukimwi," anasema akikumbuka jinsi ugonjwa huo ulivyomtesa.

"Niliamua kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa daktari wa ngozi ambaye alichukua kipande cha ngozi yangu na kwenda kuipima na kubaini tatizo ni mkorogo."

Nuru anasema alipewa dawa aina ya scaboma ambayo ilimsaidia na inaendelea kumsaidia hadi sasa. Kwa sasa ameachana na biashara hiyo na badala yake anatoa ushuhuda wa madhara ya dawa hizi.

Akizungumzia biashara hiyo, Nuru anasema licha ya kusitisha biashara iliyokuwa ikimpa fedha za kujikimu kimaisha, sasa amekuwa balozi wa kueleza madhara ya mkorogo kwa jamii.

Alianza biashara hiyo mwaka 1998 baada ya kufanya majaribio ya kupaka losheni hizo na kuona zinampendeza na watu wanazipenda na hivyo akawa anachanganya na kuuza.

"Kwa kipimo kimoja nilikuwa nauza kati ya Sh25,000 hadi 30,000 na ningeweza kupata hadi Sh400,000 kwa mwezi," anasema.

Hata hivyo, mwaka 2013, mambo yalianza kwenda vibaya baada ya kujikuta akiwashwa ngozi na kuharibika ikawa kavu, yenye mikunjo na kubadilika rangi.

Licha ya Serikali kupambana na utengenezaji na matumizi ya vipodozi vyenye sumu, imeelezwa kuwa zaidi ya nusu ya Watanzania hutumia vipodozi hivyo kwa lengo la kuongeza urembo.

Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Evirocare ya Dar es Salaam mwaka 2013 umeonyesha bado tatizo hilo ni kubwa.

Utafiti huo ulifanyika kwa kuhusisha mkoa mmoja katika kanda sita nchini. Mikoa hiyo ni Dar es Salaam ukiwakilisha Kanda ya Mashariki, Mbeya (Kanda ya Nyanda za Juu Kusini), Tanga (Kanda ya Kaskazini) na Dodoma (Kanda ya Kati).

Katika utafiti huo ambao watu 785,000 walihojiwa, asilimia 46.77 (asilimia 66 kati yao ni wanawake) walikiri kumiliki maduka ya vipodozi huku asilimia 27.38 walikuwa waajiriwa kwenye maduka hayo.

Utafiti huo pia umeonyesha kuwa maduka mengi ya vipodozi yako kwenye wilaya za Tanga (maduka 28), Ilala–Dar es Salaam maduka 27, Dodoma 23, Mbeya 22 na Kondoa maduka 20.

"Wilaya za Kinondoni na Temeke za Dar es Salaam zina maduka mengi lakini hazikuweza kuifikia wilaya ya Kondoa. Uwepo wa maduka mengi humaanisha kuwa hata watumiaji pia ni wengi japo ubora wa vipodozi katika mgawanyo na upatikanaji unatofautiana kati ya mtumiaji mmoja hadi mwingine," inasema sehemu ya utafiti huo.

Kuhusu uelewa wa watumiaji ilionekana kuwa asilimia 57.4 wanatumia kujipodoa uso, asilimia 30 wanaona kama kitu cha kujipaka mwilini na asilimia 12.6 wanaona kuwa inaimarisha mwonekano wa ngozi.


Vipodozi vinavyouzwa zaidi
Walipoulizwa kuhusu vipodozi vinavyouzwa zaidi, watu 118 walisema ni losheni, 44 walisema mafuta ya nywele, 38 vipodozi vinavyobadilisha nywele, 37 mafuta ya mwili, 26 walisema krimu na 19 walisema manukato.

Wakati matumizi ya losheni yakiwa juu kwa watu wengi hivyo kuwaweka hatarini watumiaji hao, uchanganyaji wa manukato nao unaelezwa kuwa na athari zaidi kwani huweza kuumba kemikali nyingine kutokana na zile zilizochanganywa jambo linaloweza kuzalisha usugu wa matibabu.

"Matumizi ya losheni pia yanaiweka ngozi kwenye nafasi kubwa ya kuathirika na kemikali hasa kama mtumiaji atapaka vipodozi vilivyopigwa marufuku vya Carolite na Extra light."


Waliopo hatarini zaidi
Kati ya idadi ya watu wanaotumia kwa wingi vipodozi sumu, imeonekana kuwa asilimia 67.6 ni wanawake.

"Kwa wanawake kutumia zaidi vipodozi hivyo, inamaanisha kuwa wengi wako kwenye hatari ya kuathirika.

"Kwa mfano kuna rangi za midomo, kama mwanamke atambusu au kugusana mara kwa mara na mwanaume, wote wawili wataathirika," unaeleza utafiti huo.

"Watoto wanaoathirika zaidi ni wale wanaonyonyeshwa na wanawake wanaotumia mkorogo."


Wengi hawajui madhara yake
Walipoulizwa kuhusu aina ya kemikali zilizomo kwenye vipodozi wanavyotumia, asilimia 62.4 ya watu 263 walisema hawajui huku asilimia 34 wakisema wanajua.

Unasema pia nusu ya wauzaji walisema hawajui kemikali zitumiwazo katika vipodozi wanavyouza, achilia mbali madhara yatokanayo na vipodozi, hivyo kipaumbele chao ni kupata faida kuliko afya za watumiaji.

Akizungumzia utafiti huo, meneja mradi wa kupambana na vipodozi vyenye sumu, Euphrasia Shayo anasema hali ni mbaya kwa Tanzania ndiyo maana Envirocare wameanzisha kampeni ya kupambana na vipodozi hivyo.

"Tunafanya kampeni ya kupambana na vipodozi vyenye sumu kwa sababu tatizo ni kubwa nchini. Hadi sasa asilimia 52 ya Watanzania hutumia kati ya Sh35,000 hadi 50,000 kwa mwezi kununua mkorogo. matokeo yake wengi wameathirika na wanashindwa kuacha," anasema Euphrasia na kuongeza:

"Kichocheo kikubwa ni wanaume ambao huwashawishi wanawake watumie ili wawapende. Tunatoa elimu kwa wanawake kujiamini na uzuri walionao na kutumia vipodozi visivyo na sumu."


Madhara ya vipodozi
Akizungumzia madhara ya vipodozi hivyo, Shayo anasema kwa kiasi kikubwa cha mikorogo husababisha saratani ya ngozi na kupunguza nguvu za kiume.

Madhara haya pia huwaathiri wale ambao wenzi wao wanatumia vipodozi vyenye viambata vya sumu.

"Kwa mtu aliyeathirika na matumizi ya mkorogo inabidi atumie dawa kwa miaka mitatu mfululizo huku akipewa ushauri wa kitaalamu.

Siyo rahisi kuacha kwani kwa siku mtu hutumia hadi dawa tisa, hivyo itabidi kuacha moja baada ya nyingine, vinginevyo ataharibika kabisa mwili wake," anasema.

Ofisa Habari wa Taasisi ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza anasema wamekuwa wakishirikiana na wadau kama Envirocare kupambana na tatizo la matumizi ya vipodozi vyenye sumu.

Anasema TFDA vile viel, imekuwa ikifuatilia na kukamata vipodozi vyenye sumu vinavyoingizwa nchini mbali na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu athari zake.

Ametaja baadhi ya viambata vya sumu vinavyotumika katika miongopni mwa vipodozi walivyovipiga marufuku ni pamoja na Bithionol, Hexachlorophene, zebaki, Vinylchloride, Zirconium, Halogenated salicylanilides (di-,tri-metabromsalan na tetrachlorosalicynilide), Chloroquinone na viambata vyake, Steroid, Chlofluorocarbon za kupuliza na Methyelene chloride.

CHANZO: Mwananchi
 
VIPODOZI VYENYE VIAMBATA VYENYE SUMU

Viambata vifuatavyo havitakiwi kuwepo kwenye bidhaa za vipodozi (Vimepigwa Marufuku kwa Matumizi ya Binadamu)

1. Bithionol
2.Hexachlorophene
3. Mercury compounds
4. Vinyl chloride
5. Zirconium – containing complexes in aerosol products
6. Halogenated salicylanilides (di-, tri- metabromsalan and tetrachlorosalicynilide)
7. Chloroquinone and its derivatives
8. Steroids in any proportions
9. Chloroform
10. Chlofluorocarbon propellants (fully halogenated chlorofluoroalkanes) in cosmetic aerosol products
11. Methyelene chloride

Tunapenda kutaarifu jamii kwa ujumla na wadau wote wanaojishughulisha na maswala ya vipodozi kuwa vipdozi vifutavvo vimepigwa marufuku

(ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU) LIST OF BANNED COSMETICS (2004-2005)

(vipodozi vyenye hydrokwinoni) "Cream" and "lotions" containing "Hydroquinone"

1. Mekako Cream.
2. Rico Complexion Cream
3. Princess Cream
4. Butone Cream
5. Extra Clear Cream
6. Mic Cream
7. Viva Super Lemon Cream
8. Ultra Skin Tone Cream
9. Fade - Out Cream
10. Palmer`s Skin Success (pack) Cream
11. Fair & white Active Lightening Cream
12. Fair & White Whitening Cream
13. Fair & White Strong Bleaching
Treatment Cream
14. Fair & white Body Clearing milk –tight Cream
15. Maxi – Tone fade Cream
16. Nadinola Fade Cream
17. Clear Essence Medicated fade Cream
18. Peau Claire Body Lotion
19. Reine Clair Rico Super Body Lotion
20. Immediat Claire Maxi – Beuty lotion
21. Tura Lotion
22. Ikb Medicated Cream
23. Crusader Skin Toning Cream
24. Tura Bright & Even Cream
25. Claire Cream
26. Miki Beauty Cream
27. Peau Claire Crème Eclaircissante
28. Sivoclair lightening Body Lotion
29. Extra Clair lightening Body Lotion
30. Precieux Treatment Beauty Lotion
31. Clear Essence Skin Beautifying Milk
32. Tura Skin Toning Cream
33. Madonna Medicated Beauty Cream
34. Mrembo Medicated Beauty Cream
35. Shirley Cream
36. Kiss – Medicated Beauty Cream
37. UNO21 Cream
38. Princess Patra Luxury Complexion Cream
39. Envi Skin Toner - Cream
40. Zarina Medicated Skin Lightener - Cream
41. Ambi Special Complexion - Cream
42. Lolane Cream
43. Glotone Complexion Cream
44. Nindola Cream
45. Tonight Night Beauty Cream
46. Fulani Cream Eclaircissante
47. Clere Lemon Cream
48. Clere Extra Cream
49. Binti Jambo Cream
50. Malaika Medicated Beauty Cream
51. Dear Heart with Hydroquinone Cream
52. Nish Medicated Cream
53. Island Beauty Skin Fade Cream
54. Malibu Medicated Cream
55. Care plus Fairness Cream
56. Topiclear Cream
57. Carekako Medicated Cream
58. Body Clear Cream
59. A3 Skin Lightening Cream
60. Ambi American Formula Cream
61. Dream Successful Cream
62. Symba crème Skin Lite ‘N' Smooth Cream
63. Cleartone Skin Toning Cream
64. Ambi Extra Complexion Cream for men
65. Cleartone Extra Skin Toning Cream
66. O`Nyi Skin Crème
67. A3 Tripple action Cream Pearl Light
68. Elegance Skin Lightening Cream
69. Mr. Clere Cream
70. Clear Touch Cream
71. Crusader Ultra Brand Cream
72. Ultime Skin Lightening Cream
73. Rico Skin Tone Cream
74. Baraka Skin Lightening Cream
75. Fairlady Skin Lightening Cream
76. Immediat Claire Lightening Body Cream
77. Skin Lightening Lotions Containing
Hydroquinone
78. Jaribu Skin Lightening Lotion
79. Amira Skin Lightening lotion
80. A3 Cleartouch Complexion Lotion
81. A3 Lemon Skin Lightening Lotion
82. Kiss Lotion
83. Princess Lotion
84. Clear Touch Lotion
85. Super Max – Tone Lotion
86 No Mark Cream

Gel with "Hydroquinone"

1. Body Clear
2. Topi Clear
3. Ultra Clear

Lotion containing "Hydroquinone"

1. Peau Claire Lightening Body Oil

Soaps containing "Hydroquinone"

1. Body Clear Medicated Antiseptic Soap
2. Blackstar Soap
3. Cherie Claire Body Beauty Lightening & Treating Soap
4. Immediate Clair Lightening Beauty Soap
5. Lady Claire Soap
6. M.G.C Extra Clear Soap
7. Topi Clear Beauty Complexion Soap
8. Ultra Clear Soap

Soaps containing Mercury and its compounds

1. Movate Soap
2. Miki Soap
3. Jaribu Soap
4. Binti Jambo Soap
5. Amira Soap
6. Mekako Soap
7. Rico Soap
8. Tura Soap
9. Acura Soap
10. Fair Lady Soap
11. Elegance Soap

Cream containing Mercury and its Compounds

1. Pimplex Medicated Cream
2. New Shirley Medicated Cream

Cream containing (hormones in steroids)

1. Amira Cream
2. Jaribu Cream
3. Fair & Lovely Super Cream
4. Neu Clear Cream Plus (spot Remover)
5. Age renewal Cream
6. Visible Difference Cream (Neu Clear – Spots Remover)
7. Body Clear Cream
8. Sivo Clair Fade Cream
9. Skin Balance Lemon Cream
10. Peau Claire Cream
11. Skin Success Cream
12. M & C DynamiClair Cream
13. Skin Success Fade Cream
14. Fairly White Cream
15. Clear Essence Cream
16. Miss Caroline Cream
17. Lemonvate Cream
18. Movate Cream
19. Soft & Beautiful Cream
20. Mediven Cream
21. Body treat Cream (spot remover)
22. Dark & Lovely Cream
23. SivoClair Cream
24. Musk – Clear Cream
25. Fair & Beautiful Cream
26. Beautiful Beginning Cream
27. Diproson Cream
28. Dermovate Cream
29. Top Lemon Plus
30. Lemon Cream
31. Beta Lemon Cream
32. Tenovate
33. Unic Clear Super Cream
34. Topiflam Cream
35. First Class Lady Cream

Gel containing steroids

1. Fashion Fair Gel Plus
2. Hot Movate Gel
3. Hyprogel
4. Mova Gel Plus
5. Secret Gel Cream
6. Peau Claire Gel Plus
7. Hot Proson Gel
8. Skin Success Gel Plus
9. Skin Clear Gel Plus
10. Soft & Beautiful Gel
11. Skin Fade Gel Plus
12. Ultra – Gel Plus
13. Zarina Plus Top Gel
14. Action Dermovate Gel Plus
15. Prosone Gel
16. Skin Balance Gel Wrinkle Remover
17. TCB Gel plus
18. Demo – Gel Plus
19. Regge Lemon Gel
20. Ultimate Lady Gel
21. Topifram Gel Plus
22. Clair & Lovely Gel

(ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU) LIST OF BANNED COSMETICS (2005-2006)

Cosmetics containing "Hydroquinone"
1. Body White Lotion
2. Bio Claire Cream
3. Forever Aloe MSM Gel
4. Kroyons baby oil

Cosmetics containing drug ingredients
1. Blue cap spray
2. Blue cap cream
3. Blue cap Shampoo
4. Marhaba Anti- Dandruff hair Cream

Hair cosmetic containing prohibited extract from "Apocynum Cannabium root extract"
1. African Gold Super Gro

Cosmetic containing potential carcinogenic extract from "Tussilago
farfara"
1. Sofn` Free Hair Food


(ORODHA YA VIPODOZI VILIVYOPIGWA MARUFUKU) LIST OF BANNED COSMETICS (2007-2008)

(vipodozi vyenye hydrokwinoni na steroid) Cosmetics containing "Hydroquinone & Steroid"

1. Clear Essence skin beautifying milk for sensitive skin
2. Fair & White Clarifiance fade cream
3. Fair & White Exclusive Whitenizer body lotion
4. Fair & White exclusive whitenizer cream gel
5. Fair & White Maxitone Lightening Lotion sun block
6. Fair & White So White Skin Perfector Gel

(vipodozi vyenye hydrokwinoni pekee) Cosmetics containing "Hydroquinone"

1. Fair & White Powder (Exclusive whitenizer & Serum)
2. New Youth Tinted Vanishing Cream
3. Skin Success Fade Cream Regular
4. Teint Clair Clear Complexion Body Lotion
5. Mareme Cream
6. Si Claire Plus Cream
7. Clair & White Body Cream

(vipodozi vyenye steroid pekee) Cosmetics containing "Steroid"

1. Fair & White serum exclusive Whitenizer
2. Maxi White Lightening Body Milk
3. Maxitone Cleansing Milk
4. Avoderm Cream
5. Niomre Cream
6. Niomre Lotion
7. Nyala Lightening Body Cream
8. Si Claire Cream
9. Cute Press White Beauty Lotion
10. White SPA Rose Lotion
11. White SPA UV Lightening Cream

Cosmetic containing extract from "Arctostaphylos UVA URSI (bearberry extract)"Plant containing "Hydroquinone" na "Arbutin".

1. Bio Light Cream
2. Salon DermaPlex Amazon Clay Normal to Dry Skin
3. Beauty Secrets Body Cream
4. Swiss Soft N White Lightening Gel
5. Whitening Complex Mask

Cosmetic containing potential carcinogenic extract from "Tussilago farfara"

1. Elasta-QP- (DPR-11) Hair Conditioner
2. Fanrasia- Pure Tea Gro for Hair

(vipodozi vyenye kiasi kikubwa cha madini ya zinki pyrithione, zaidi ya 1%) Cosmetic containing high concentration of Zinc Pyrithione 48% instead of Zinc Pyrithione 1%

1. Venus Solutions Soothing Scalp Treatment

Cosmetics containing Tin Oxide ingredient that associate with irritation when used around the area of the eye.


1. Eye Shadow Gel 10
2. Eye Shadow Gel 02 (Pearl Brown Gel with chaaracterisric odor)
3. Eye Shadow Gel 07 (Pearl Pink gel with characteristic odor)
4. Eye Shadow Gel 08 (Pearl Dark Red gel with characteristic odor)
5. Eye Shadow Gel 09 (Purple Dark Red gel with characteristic odor)
6. Eye Shadow Gel

Cosmetics containing malic acid and tartric acid that have property of peeling out skin cells causing whitening effect

1. AHA Whitening Cream


Source:TANZANIA FOOD AND DRUGS AUTHORITY
 
Asante sana Baba Mtu!!Kinachonishangaza mbona bado vipo madukani!!kweli ufisadi kila kona cjui itakuwaje,Kibaya zaidi vipodozi vilivyokatazwa mijini vinauzwa vijijini kwa bei poa kabisa,nilikuwa kwenye research nikayaona haya!!Who will save us jaman these people are killing women!!!
 
Actually it is suggested people use natural or herbal products; the above ones and perhaps many more could lead to skin cancer in a long run. Eating vegetables and drinking a lot of water is good for one's skin....lets avoid chemicals friends, ladies and gentlemen?
 
Asante sana Baba Mtu!!Kinachonishangaza mbona bado vipo madukani!!kweli ufisadi kila kona cjui itakuwaje,Kibaya zaidi vipodozi vilivyokatazwa mijini vinauzwa vijijini kwa bei poa kabisa,nilikuwa kwenye research nikayaona haya!!Who will save us jaman these people are killing women!!!

Kinachotakiwa ni kutoa taarifa tfda(mamlaka ya chakula na dawa tanzania). Vile kuwaelimisha akina mama na akina dada juu ya madhara ya kutumia vipodozi hivi. Kulikuwa na thread moja hapa jf ikitueleza jinsi dada yetu alivyoharibiwa ngozi yake na dawa/vipodozi.
 
Wengi wa wanaosoma hapa utakuta hawatumii ila wale dada zetu wa mtaani....
Na TFDA wanaweka kwenye website badala ya kukazania kutoa elimu kwa umma juu ya madhara ya vipodozi hivyo. Kibaya zaidi vimejaa tele Kariakoo, Ilala, Sinza na mtaani kwetu.
 
Duh!!! Hadi Clear Essence ndani tumekwisha halafu alomst vipodozi vyote bado viko dukani na watu wataendelea kununua kama kawa
 
Wanawake nchini wametakiwa kubadilika kwa kuacha kutumia vipodozi vyenye madhara mwilini na kuachana na dhana kuwa ukiwa mweupe au kuwa na mapaja manene unapendwa zaidi. Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Kanda ya Kati, Florent Kyomo.

Kyomo amesema kuwa, asilimia kubwa ya waathirika wa vipodozi ni wanawake hasa wale wenye uelewa mdogo ambao hawataki kubadilika kwa kudhani kuwa weupe ni moja ya mafanikio na kupendwa zaidi na wanaume.

Ameongeza kuwa, changamoto kubwa wanayokabiliana nayo ni uelewa wa wananchi juu ya matumizi ya vipodozi vyenye madhara ambapo wengi wao wanashindwa kuacha kutumia kutokana na kutumia madawa hayo kwa muda mrefu na kufafanua kuwa, hata hivyo kuwa wataendelea na mikakati ya kutoa elimu zaidi ili watu wengi wajue madhara na kuwa na dhamira ya kuacha kutumia vipodozi hivyo.
 
KWELI kabisa mtu unatakiwa ujikubali jinsi MUNGU alivyokuumba na sio kujikoboa koboa
 
teh hata wanaume siku hz wanajichubua tena sana tu, so siyo vizur kusema ni wanawake tu, cha msingi ni kuwa hili jambo lina madhara na wahusike wanapaswa kushauriwa waache kujichubua, na wahusika wenyewe ni wanawake na wanaume wanaotumia hyo mivipodozi na siyo wanawake peke yao.
 
mimi napingana na kauli ya uelewa mdogo. Kuna wasomi kibao na wengine ni doctors na wanajichubua. Pia ni kweli kuna wanaume wengi tu siku hizi wanajichubua.
 
mimi napingana na kauli ya uelewa mdogo. Kuna wasomi kibao na wengine ni doctors na wanajichubua. Pia ni kweli kuna wanaume wengi tu siku hizi wanajichubua.

Unaweza ukawa msomi ila ukawa haujajitambua, suala la msingi wapewe elimu ya kujitambua ili waweze kujikubali jinsi walivyo!!
 
ila tuache maskhara bwana MWANAMKE MWENYE MAPAJA MANENE(figure bomba) NA MWEUPE anavutia wakuu..hasa for single night affair
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom