Yajue madhara ya kukanda wazazi kwa maji ya moto

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
410
1,000
Wakati wanawake walio wengi wanaamini kukandwa maji ya moto baada ya kujifungua ni tiba, wataalamu wa afya ya uzazi wanaonya kuwa kufanya hivyo kuna madhara zaidi ikilinganishwa na faida ambazo zimekuwa zikiainishwa.

Miongoni mwa madhara yanayotajwa ni pamoja na kumsababishia mama maumivu makali, kuharibu maumbile yake, kulegeza misuli, majeraha yanayosababishwa na maji ya moto, kuzuia uponyaji wa haraka, kusababisha maambukizi na tatizo la kisaikolojia kwa hofu ya kukandwa.

Pamoja na madhara hayo, jamii inaamini kwamba maji ya moto ni tiba ya kurejesha maumbile ya asili kwa aliyejifungua. Kati ya wanawake waliozungumza na gazeti hili, wote wanasema maji ya moto ni tiba, japo hawana ushahidi wa kitaalamu.

Mkunga wa jadi kutoka kijiji cha Minyaa kilichopo Kata ya Kinyeto, Halmashauri ya Singida, Onolata Kisaka (67) alisema kukanda maji moto ni kitu muhimu kwa mama aliyejifungua ili kuondoa uchafu uliosalia tumboni baada ya mtoto kutoka.

“Miaka mingi mama lazima akandwe na ndiyo uhai. Asipokandwa wengi walifariki kutokana na uchafu tumboni. Haya mambo ya kutokandwa yanakuja sasa hivi wakati kuna hospitali kila mahali,” alisema Onolata.

Lulu Khatibu alisema walizoea kuona wanawake wakifanyiwa hiyo mila inayoendelezwa na wanafamilia baada ya kujifungua. “Hata nilipokuwa msichana baada ya kujifungua nilikandwa na nilikuwa naona afadhali nikifanyiwa hivyo, hii ni desturi yetu sisi wanawake hasa wa Afrika.”

Hata hivyo, wapo waliopata madhara baada ya kukandwa maji moto, akiwamo Arafa Juma (26) ambaye alivuja damu nyingi na baadaye kuvimba mwili baada ya kukandwa kwa maji moto.

“Nilijifungua vizuri, baada ya siku moja nikarudi nyumbani. Nilipofika kitu cha kwanza ilikuwa kwenda bafuni kukandwa. Ghafla nilianza kutokwa damu nyingi, mabonge mabonge na bibi yangu alisema ni uchafu unatoka, lakini baada ya muda mwili ukaanza kuvimba.

“Nilirudishwa hospitali walisema ni madhara ya kukandwa maji moto, nilichomwa sindano damu ikakata na baada ya matibabu mwili ulirudi sawa,” alisema Arafa, mama wa mtoto mmoja.

Madhara ya kukandwa
Wakunga na madaktari bingwa wa kinamama na magonjwa ya uzazi waliozungumza na gazeti hili wamesema hakuna uchafu unaotakiwa kutolewa na maji ya moto kwa kukandwa na kuminywa na kwamba uke haurudi kwa kukandwa bali huharibika zaidi.

“Mara zote jamii hudhani damu zinazotoka mara baada ya kumkanda mama ni uchafu uliobaki baada ya kujifungua. Ni makosa makubwa, kwani maji moto hufungua mishipa ya damu iliyojifunga mara baada ya mtoto kutoka na pale damu huanza kuvuja upya,” alisema mkunga mtaalamu, Agnes Ndunguru.

Alisema hatua za kujifungua ni za asili na hivyo hata baada ya kujifungua kila hatua huwa ni asili, hivyo hakuna sababu ya kutumia nguvu kubwa kuurudisha mwili wa mama.

“Taarifa hupelekwa katika ubongo kwamba mtoto ameshatoka, yanahitajika maziwa kwa ajili ya mtoto na sehemu ya mji wa mimba inatakiwa kurudi na kushuka kwenye pango la nyonga kuwa ya kawaida kama mtu ambaye hana mimba,” alisema.

Agnes ambaye miaka saba ya kazi yake ameshazalisha wanawake 6,000, alisema vitu hivyo vyote vinatokea kiasili na kwamba hakuna haja ya kukanda kwa maji moto eti kutoa uchafu.

“Mjamzito akishajifungua kondo la nyuma au placenta inapotolewa tunahakikisha tunaondoa mabaki yote, hivyo hakuna uchafu anaobaki nao mama kwa sababu ukibaki husababisha kutokwa na damu nyingi sana,” alisema.

Alisema ingawaje kuna utafiti ambao unaendelea kufanyika, kina mama wengi wamekuwa wakirudi hospitalini baada ya kupata athari ya kukandwa maji moto na wengine hupoteza maisha.

Alisema wamekuwa wakiwabaini kinamama wengi baada ya kufika hospitalini kwa ajili ya kupimwa ujauzito wa pili. “Wapo wanaokuja maziwa hayatoki, wamepata malengelenge ukeni, ukiwachunguza tayari wametanuka misuli ya uke kwa kuwa wengine anawekewa kwenye kigoda anakalia maji, hawa tunawabaini.

“Ukimuuliza anakiri alikandwa, kwani kuna utofauti kwa ambaye hakukandwa maji moto ambaye uke wake unakuwa wa kawaida, ile mikunjo mikunjo kwenye kuta za uke inakuwepo, tofauti na aliyekandwa,” alisema.

Mbali na hayo, alisema wapo kinamama ambao hubainika kupata athari za kufumuka kwa mishono na hao huwa na uwazi kwenye uke kwa chini, “kama mama aliongezwa njia, akikandwa zile nyuzi hulainika na kuachia, hivyo kidonda hakitafunga na wengine huwa hashtuki unakuja kubaini anapojifungua mtoto mwingine.”

Katibu wa Chama cha Wakunga Tanzania (Tama), Nicodem Komba alisema ijapokuwa utafiti unaendelea kufanywa, lakini athari zake zinaonekana, kwani wengine wanapoteza maisha.

Alisema maji moto hutanua mishipa ya damu na hivyo husababisha athari kubwa mpaka kwenye moyo. “Ni hali ambayo huwa tunaishuhudia kwa wagonjwa wa aina hiyo, mama akijifungua kiasi kikubwa cha maji hupungua mwilini, hivyo kufanya mishipa kusinyaa, sasa kukandwa na maji ya moto huzidi kulainisha mishipa ya damu na kufanya itanuke, kitu ambacho husababisha presha ya damu kupungua na kusababisha tatizo la ‘postpartum carsiomypathy’ (maradhi ya moyo baada ya kujifungua),” alisema.

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi katika Hospitali ya Aga Khan, Manuwar Kaguta alisema kwa wazazi tiba ya maji ya moto inatia hofu inavyotumika na ndiyo maana vituo vya afya havijawahi kumshauri mama au ndugu kwamba mama akandwe kwa maji moto kutokana na madhara yaliyopo.

Dk Kaguta alisema wengine hukanda mpaka sehemu za uke na kwamba hospitalini wamekuwa wakipokea kinamama waliopata athari za kukandwa na maji moto.

Husababisha vifo
Mwaka 2019 wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Jiongeze Tuwavushe Salama, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilisema mtindo wa kuwakanda na maji ya moto wanawake wakishajifungua ni hatari.

Wizara iliainisha kuwa kukandwa na maji ya moto kunaweza kusababisha mama kutokwa na damu nyingi na hata kifo.
“Hatuwezi kushauri wanawake waliojifungua kukandwa maji ya moto, japo suala hilo limezoeleka kwa wengi, lakini hakuna uthibitisho wa kitaalamu wa kumponya mwanamke kwa kutumia maji hayo isipokuwa kumletea madhara,” ilielezwa

images - 2021-11-12T162900.782.jpeg
 

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,121
2,000
Mimi ni baba ila nachojua nitakielezea

Mwanamke akijifungua kwa operation mara nyingi dokta mwenye mapenzi na kazi yake huwa wanasafisha kizazi vizuri kabisa. Hata akirudi kula uzazi nyumbani uchafu huwa unatoka damu nyepesi tu ya kidonda. Sio damu nyingi wala nzito

Kwa wale wanaojifungua kawaida, mara nyingi hao ndo hupata kutoka damu nyingi tena mabuje mabuje kama ya ugali au uji uliotelekezwa. Kwa asili yetu sisi waafrica wengi wanaamini ila mwili uyatoe yale mabuje buje lazima ukandwe na maji ya moto. Sijawahi kufikiri hii inaleta athari kubwa kiasi gani ila uzi huu umenifungua.

Nafikiri tatizo hapa ni watu wanakuwa na nadharia zao kichwani, inawezekana maji ya moto yamewasaidia wanawake wengi sana ila watu wanachubuana kama kuku. Kumbe maji ya moto kawaida yengeweza kusaidia. Nishaona wazungu wakivaa heating pad baada ya kujifungua kupunguza maumivu ya tumbo la uzazi, so it might be important kuruhusu mzunguko wa damu vizuri...

Huyu dada Agness Nduguru ni classmate wa secondary school nilisoma nae shule ya jeshi Dar O level. Ila nilisikia ni mkunga Hospital flani hivi ya serikali pande za Sinza. Ile hospital ni nzuri sana kwa kufungilisha hainaga record mbaya. Shida tu kila mtu katika hospital yoyote ya serikali lazima uende kujifungua na zana za kilimo. Wakinamama chukueni taadhari sana kujichua na maji ya moto makali, tumieni maji yenye joto lisiloumiza. .

NB:
Huko kwetu Rombo wakunga huwa wanashauri mama kuweka mafuta mengi kwenye chakula kwa madai yanatoa uchafu uliobakia tumbo la uzazi. Pia wanashauri wajawazito watumie vyakula vya moto. Wachaga wanapenda kutumia vyakula vya ndizi na maziwa mtindi (mfano kena) wamama wajawazito, na supu yenye mafuta, mtori, kiburu cha kunde (mbere) nk.

WANAWAKE WA KICHAGA WANAZAA WATOTO WENGI NA HAWAZEEKI MAPEMA, HAPA KWENYE CHAKULA JAMII INATAKIWA IJIFUNZE KWA WACHAGA. Hususani ndugu zetu wapemba wale wa kula rojo rojo wajifunze sana kutokana na tamaduni za wachaga. .
 

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,121
2,000
Umenikumbusha mkuu asee wachaga wanajali sana wazazi.
Huku Dar siku 40 mwanamke anaenda kwa bwana. Ndo mana waswahili wanazaa kama kuku

Kilimanjaro mwanamke anakaa ndani miezi mitatu marufuku kwenda kwa bwana, Huku anahudumiwa kila kitu. Sema waswahili wanadai mwanamke akikaa ndani anatoka kama puto.

Mie nimeoa mswahili, mwanangu kazaliwa 29 september mwaka huu. Yani week moja tu anaona yuko kifungoni hahahah
 

saci

Member
Mar 4, 2014
71
150
Huku Dar siku 40 mwanamke anaenda kwa bwana. Ndo mana waswahili wanazaa kama kuku

Kilimanjaro mwanamke anakaa ndani miezi mitatu marufuku kwenda kwa bwana, Huku anahudumiwa kila kitu. Sema waswahili wanadai mwanamke akikaa ndani anatoka kama puto.

Mie nimeoa mswahili, mwanangu kazaliwa 29 september mwaka huu. Yani week moja tu anaona yuko kifungoni hahahah
Na ndio maana wanakosa nguvu maana kwa mazingira ya dar hakuna vyakula vya asili, mzazi anatakiwa awe anakula nyama nusu maziwa lita kila siku.

Akitoka amependeza na pia mtoto anapata maziwa ya kutosha, na pia mama akijifungua atatafutiwa mtu wa kumpikia.

Hata mtoto anayetumwa tumwa vitu nayeye ananenepa hahah

Kama uko dar mkeo akijifungua mpeleke nyumbani akale mapochopocho miezi mi3 arudi.
 

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,121
2,000
Na ndio maana wanakosa nguvu maana kwa mazingira ya dar hakuna vyakula vya asili, mzazi anatakiwa awe anakula nyama nusu maziwa lita kila siku.

Akitoka amependeza na pia mtoto anapata maziwa ya kutosha, na pia mama akijifungua atatafutiwa mtu wa kumpikia.

Hata mtoto anayetumwa tumwa vitu nayeye ananenepa hahah

Kama uko dar mkeo akijifungua mpeleke nyumbani akale mapochopocho miezi mi3 arudi.
Hata hivyo wazazi wangu wako Dar. Mama anamwanglia kichaga zaid

Si unajua ukiwa home ukienda nunua nyama wanakupa na utumbo mchanganyo humo humo. Mjini tumbo unauzwa kivyake nyama inauzwa kivyake.

Aisee sijajua sababu ni nini, either utumbo uko very cheap ndo mana unawahi kuisha, ama wazaramo hawana hela ya kununua nyama kilo elfu 8 wananunua utumbo bei cheee. Ukienda buchani saa nne utumbo wote umenunuliwa na waaramo hupati kitu mzee
 

Lily Tony

JF-Expert Member
Feb 6, 2019
2,454
2,000
Mmmhh!haya mambo jamani...Mimi bado ntakandwa kama ntaendeleza kuzaa...kila Siku wanaleta mambo mapyaaa...nani alikufa kwa kukanda maji ya moto?au kuharibika...
Waangalie takwimu za walokufa na walopona watuachie na njia zetu za asili
Jasiri haachi asili😁.
Mimi nilikandwa maji ya moto kwa muda wa wiki moja tu,ingawa kabla ya kukandwa nilipakwa mafuta mengi ya mgando tumboni ili kupunguza maumivu.
Sikupata madhara yoyote
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,574
2,000
Huku Dar siku 40 mwanamke anaenda kwa bwana. Ndo mana waswahili wanazaa kama kuku

Kilimanjaro mwanamke anakaa ndani miezi mitatu marufuku kwenda kwa bwana, Huku anahudumiwa kila kitu. Sema waswahili wanadai mwanamke akikaa ndani anatoka kama puto.

Mie nimeoa mswahili, mwanangu kazaliwa 29 september mwaka huu. Yani week moja tu anaona yuko kifungoni hahahah
Huyo wa kwako tu Mimi nimezaa Dar sitoki mpk clinic sindano!!!wa kwako umemzoesha kuzurura ndo maana!kwanza kidini wengine ukiwa na nifasi unapaswa kutulia huruhusiwi kuzururazurura maana waweza kumbwa na upepo mbaya...
Muambie atulie alee
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,574
2,000
Jasiri haachi asili.
Mimi nilikandwa maji ya moto kwa muda wa wiki moja tu,ingawa kabla ya kukandwa nilipakwa mafuta mengi ya mgando tumboni ili kupunguza maumivu.
Sikupata madhara yoyote
Umeonaa eehhh!!mimaji wiki tu fresshh!!

Kama athari wangepata mabibi,mama na waliotangulia..hawa wanasayansi kila siku mambo mpaya,hivi Sindano hazina madhara kwa mwanadamu?au mzungu akisema ndo kasema. !!!!
 

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,121
2,000
Huyo wa kwako tu Mimi nimezaa Dar sitoki mpk clinic sindano!!!wa kwako umemzoesha kuzurura ndo maana!kwanza kidini wengine ukiwa na nifasi unapaswa kutulia huruhusiwi kuzururazurura maana waweza kumbwa na upepo mbaya...
Muambie atulie alee
Sio kwamba anazurura barabarani, wala
Unajua anaambiwa akazane kulala na mgongo bado hajakaa sawa
Yeye mara anataka akae sebuleni
Mara unaona anahangaika na kazi za nyumbani
Hajazoea tu kukaa sehemu moja mda mrefu

Ila namkazania sana, kwa faida zake. Nimepata mtoto wa kike. Mungu ni Mwema sana. Na mimi naitwa baba sasa. .
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,574
2,000
Sio kwamba anazurura barabarani, wala
Unajua anaambiwa akazane kulala na mgongo bado hajakaa sawa
Yeye mara anataka akae sebuleni
Mara unaona anahangaika na kazi za nyumbani
Hajazoea tu kukaa sehemu moja mda mrefu

Ila namkazania sana, kwa faida zake. Nimepata mtoto wa kike. Mungu ni Mwema sana. Na mimi naitwa baba sasa. .
Hongera sana kwa kubarikiwa bebi gelo.

Kulala ndo mpango mzima na kupumzika yaani Mimi nikitoka kujifungua nashukuru kwangu wanajaa watu kama kituo cha polisi nalala mda wote kwa kweli hilo nazingatia na uzuri wale ni ndugu zangu baasi wanaelewa.

Mkeo may be anaona haya kwa kua yupo mkwe anadhani ataonekana mvivu au anadeka ndo maana lakini kama angekua kwao kwa wazazi wake angepumzika vzr tu!
 

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,121
2,000
Hongera sana kwa kubarikiwa bebi gelo...
Kulala ndo mpango mzima na kupumzika yaani Mimi nikitoka kujifungua nashukuru kwangu wanajaa watu kama kituo cha polisi nalala mda wote kwa kweli hilo nazingatia na uzuri wale ni ndugu zangu baasi wanaelewa...
Mkeo may be anaona haya kwa kua yupo mkwe anadhani ataonekana mvivu au anadeka ndo maana lakini kama angekua kwao kwa wazazi wake angepumzika vzr tu!
Mungu ni mwema sana
Wengine wakipiga bao tu mtoto huyo
Sie wengine sijui sperm zina slow run
Zinachukua mda kufikia egg si mchezo

Unajitambua kwa kweli. Hongera mno
Inashauriwa mtu alale mda mrefu mpaka mgongo urudi
Yeye mwenyew hajazoea tu kulala
Mkwewe anakuja na kuondoka na mtu yuko kwake. Najitahidi kumkazania, si unajua first time mom wanavyokuwa
 

reymage

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,574
2,000
Mungu ni mwema sana
Wengine wakipiga bao tu mtoto huyo
Sie wengine sijui sperm zina slow run
Zinachukua mda kufikia egg si mchezo

Unajitambua kwa kweli. Hongera mno
Inashauriwa mtu alale mda mrefu mpaka mgongo urudi
Yeye mwenyew hajazoea tu kulala
Mkwewe anakuja na kuondoka na mtu yuko kwake. Najitahidi kumkazania, si unajua first time mom wanavyokuwa
Mungu mwema wakati sahihi ni wakati wa ktk maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa huo ndo mda wenu ulikua wa kupata mtoto kaka

Muambia akilazimisha kazi ataumwa mgongo akae apumzike mda mrefu walau hata zile 40days consecutively!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom