Yajue Maajabu ya Kunywa glass ya Maji ya Uvuguvugu Asubuhi.

Fabian the Jr

JF-Expert Member
Aug 4, 2012
756
743
Kuna mambo mengi sana ambayo binadamu huwa tunayapuuzia ambayo ki msingi ni msaadaa mkubwa sana kwa afya zetu na badala yake tunakimbilia madawa ya pesa nyingi sana mahospitalini. Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeamini na ni shahidi wa Maajabu makubwa sana yaliyopo katika Glass ya maji ya uvuguvugu asubuhi kabla hujala chochote kile.

Ukijenga mazoea ya kufanya hivyo kila asubuhi ni tiba nzuri sana kwa magonjwa mengi mfano Kansa, Uchovu mwilini, Homa za mara kwa mara, Lakini pia utashangaa mwili wako utakavyokuwa fit wakati wote. Kwa maelezo zaidi nimekuwekea link ya video hapo naamini itakusaidia kujua baadhi ya faida za maji ya Uvuguvugu asubuhi. Uwe na Afya njema.

Tabia hii ya kunywa maji ya vugu vugu au ya moto pamoja na kunywa kinyuaji cha moto pamoja na chakula nimekiona nchi nyingi hapa Asia.

Wanasema inayayusha mafuta katika tumbo na kufanya mwili usigandishe hayo mafuta yanayoweza kusababisha magonjwa kama ugonjwa wa moyo.

Hii tabia ipo sana Japan, Malaysia, Indonesia, China na Korea.
 
Naaam ni kweli kabisa mkuu umenena vyema, Na hata mimi nilianza kui adapt hii tabia waakati nimesafiri kikazi Canada. Wenzetu kidogo washaufanya huu kama utaratibu wao.
 
Kanada kuna watu kutoka sehemu zote duniani. Ukienda hoteli zilizo Chinatown, utapewa chai ya moto ya kijani bila maziwa wala sukari kabla ya chakula chako kuja.

Kama hujui, utaagiza soda na kuiacha dawa mezani.

Kusafiri nchi za watu unapata elimu sana.
 
Tabia hii ya kunywa maji ya vugu vugu au ya moto pamoja na kunywa kinyuaji cha moto pamoja na chakula nimekiona nchi nyingi hapa Asia.

Wanasema inayayusha mafuta katika tumbo na kufanya mwili usigandishe hayo mafuta yanayoweza kusababisha magonjwa kama ugonjwa wa moyo.

Hii tabia ipo sana Japan, Malaysia, Indonesia, China na Korea.
kwel kabisa ndug kwan na nasisi tukifanya hiv uke msongamano wa kwenda mahospitalini utapungua pia
 
Kanada kuna watu kutoka sehemu zote duniani. Ukienda hoteli zilizo Chinatown, utapewa chai ya moto ya kijani bila maziwa wala sukari kabla ya chakula chako kuja.

Kama hujui, utaagiza soda na kuiacha dawa mezani.

Kusafiri nchi za watu unapata elimu sana.
Hahahahahaaaa Duuuh mkuu nimejikuta nacheka tu maana umenikumbusha kitu kama vile ulikuwepo. Hahahaaaa
 
VIPI KWA MIMI NINAYEKUNYWA YA KAWAIDA TU AMBAYO SIYO YA MOTO AU BARIDI
Kunywa maji ni Muhimuu. Ingawa inategemea unakunywa kwa wakati gani na kiasi gani. Kuna wakati ukinywa maji unakuwa unaupunguzia mwili uwezo wake wa kufanya kazi mfano kunywa maji wakati unakula. Ndio maana inapendekezwa sana hii ya Kunywa maji asubuhi mara tu unapoamka na kabla hujatia mdomoni kitu chochote. Hapo maji hayo yanakuwa yanafanya kazi vizuri sana mwilini kwa sababu mwili unakuwa tayari kwa ajili ya maji. Na haitakiwi kuwa maji ya baridi yaliyotoka kwenye friji. Yakiwa ya uvuguvugu inakuwa bora zaidi ndugu.
 
Kiasi cha maji

Unywe angalao lita moja
Kwa mda wa dakika moja
kila siku asubuhi kama ilivyoelezwa hapo juu

Ni kweli inasaidia kuwa na afya njema
Safi sana, nafurahi kuona at least kuna watu pia wanalifahamu hili.
 
Nilishawahi ambiwa hili na mjomba wangu fulani anafanya kazi na shirika fulani kuna wachina!
Eti huwa wana vichupa fulani havipozi maji basi ndio wanaweka hayo maji!

Nikaimagine na joto la dar nikajua uongo!

Leo kupitia uzi huu ndio nimethibitisha
 
VIPI KWA MIMI NINAYEKUNYWA YA KAWAIDA TU AMBAYO SIYO YA MOTO AU BARIDI
Maji ni bora sana kwa afya kuliko kinywaji chochote.

Maji ya vugu vugu ni bora zaidi lakini hata ya kawaida yasiyo baridi ni bora kuliko juice au maji baridi.

Juice nyingi zina acid na husababisha vidonda tumboni ukinywa sana. Maji yanasaidia kukupa choo haraka, digestive system zinakuwa active haraka hasa ukila na oatmeal badala ya mkate. Oatmeal ina fiber, inasaidia kupata choo haraka asubuhi.
 
Kunywa maji ni Muhimuu. Ingawa inategemea unakunywa kwa wakati gani na kiasi gani. Kuna wakati ukinywa maji unakuwa unaupunguzia mwili uwezo wake wa kufanya kazi mfano kunywa maji wakati unakula. Ndio maana inapendekezwa sana hii ya Kunywa maji asubuhi mara tu unapoamka na kabla hujatia mdomoni kitu chochote. Hapo maji hayo yanakuwa yanafanya kazi vizuri sana mwilini kwa sababu mwili unakuwa tayari kwa ajili ya maji. Na haitakiwi kuwa maji ya baridi yaliyotoka kwenye friji. Yakiwa ya uvuguvugu inakuwa bora zaidi ndugu.

Hapo sawa nimekupata....vipi usiku yashauriwa kunywa maji mara ngapi?
 
Maji ni bora sana kwa afya kuliko kinywaji chochote.

Maji ya vugu vugu ni bora zaidi lakini hata ya kawaida yasiyo baridi ni bora kuliko juice au maji baridi.

Juice nyingi zina acid na husababisha vidonda tumboni ukinywa sana. Maji yanasaidia kukupa choo haraka, digestive system zinakuwa active haraka hasa ukila na oatmeal badala ya mkate. Oatmeal ina fiber, inasaidia kupata choo haraka asubuhi.
HAPO NIMEKUPATA NA NIMESHAYASHUHUDIA PIA..MAJI YANA UMUHIMU WAKE
 
Back
Top Bottom