Zijue dalili zinazoashiriwa na muonekano wa kucha zako

kat.ph

JF-Expert Member
Dec 19, 2013
2,222
1,675
Zijue dalili hizi zinazoonyeshwa na kucha.....

1478189910826.jpg


Kucha zikiwa na vidoti vyeupe inaonyesha mtu ana upungufu wa vitamins au reaction ya allergy

1478190028931.jpg


Kucha ikiwa na mstari/mistari mweusi inaweza ikawa inaonyesha dalili ya melanoma (melanoma ni aina ya kansa ya ngozi)

1478190198643.jpg


Kreki kwenye kucha yaweza ikawa inaonyesha ugonjwa wa ngozi

1478190620976.jpg


Kucha zikiwa na rangi ya blue hasa ile sehemu nyeupe mwanzo wa kucha (wanaiita alama ya mwezi) inaonyesha matatizo katika mapafu na mzunguko wa oxygen mwilini. Inaonyesha organs za mwili hazipati oxygen ya kutosha

1478190850549.jpg


Alama nyeupe (alama ya mwezi) mwanzoni mwa kucha ikiwepo, inaonyesha mmeng'enyo mzuri wa chakula mwilini pamoja na afya ya tezi za mwili

1478191137921.jpg


Kutokuwepo kwa ile alama nyeupe kwenye kucha (alama ya mwezi) kunaonyesha afya mbovu/dhaifu ya tezi. Hii husababisha depression, kubadilikabadilika kwa mood ya mtu, kuongezeka uzito na kuwa na nywele nyepesi

1478191441794.jpg


Rangi ya alama nyeupe ya kucha/ mwanzoni mwa kucha (kwenye alama ya mwezi) iliyopauka inaonyesha uwezekano wa kuwa na kisukari.
Kucha za rangi ya njano (kama umepaka hina) huonyesha kupatwa na fangas (fungal infection)
 
MBONA me na vidoti dot vyeupe Lakini Nina Kula mboga za majani Kwa wingi Sana. NINI kinafanya vitamini yangu IWE ndogo
 
MBONA me na vidoti dot vyeupe Lakini Nina Kula mboga za majani Kwa wingi Sana. NINI kinafanya vitamini yangu IWE ndogo
Watu wengi hawajui kupika mboga za majani.
Mboga za majani inapasa zipikwe chini ya joto la nyuzi 30 (correct me kama nimekosea kiwango cha joto) hapo ndio utapata vitamins.
Ila ukizipika kwa joto zaidi ya hapo (labda nyuzi 100 ambapo hizi hufikiwa kitu kikichemka (boiling point)) unaharibu vitamins zote. Means ukila hiyo mboga inakua kama unakula makaratasi tu ili ujaze tumbo.

Ndio maana wenzetu wengine mbogamboga wanaosha tu na maji yamoto halafu wanakula.

Pia kula matunda kwa wingi kwasababu pia wengi hatulagi matunda katika milo yetu. Labda tunaona ni gharama au haina maana sana
 
Back
Top Bottom