Yahya Mohamed na 'Songombingo' kwa Dr Ulimboka

Lwesye

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
5,292
1,141
Yahya Mohamed, wewe ni memba hapa JF naomba unipe jibu:

Hivi ni kweli Waandishi wa habari waache kumwandika DR Ulimboka kwa sababu wanampa kichwa na wananchi wamechoka habari zake?
Je, ni kweli madaktari wanamuona Dr Ulimboka anafanya nchi isitawalike na wanamuona ni mchochezi?
Je, uliyosema leo kwenye kipindi cha tuongee asubuhi baada ya kusoma gazeti mtaandaoni la the Citizen, wananchi wamechoka kusikia habari za Dr Ulimboka?
Je, Yahaya wewe ni mwandishi mwanaharakati unafuatilia habari mpaka upate jibu na kuwahabarisha wananchi au wewe una masilahi binafsi?
Je, Yahaya umefanya haki kuwazodoa waandishi wenzako kwamba wanamwendekeza na kumukweza Dr Ulimboka?

Leo umenisikitisha sana, I am one of you fans but I have been deeply disappointed with your today's comments. I think you used a very wrong platform.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Lwesye, Siku hizi kuna kitabia fulani ..kwamba mtazamo wa mtu mmoja(however how powerful, famous, or insignificant in the society he/she might be) kuchukulia "mawazo" yake ndio mtazamo wa wananchi "wote".

Na mara nyingi ni kwa watangazaji a Runinga na Redio.
BADILIKENI.
 
Kweli kabisa,hawa watangazaji wa runinga na radio na baadhi ya waandishi wa habari wa magazeti wanapenda sana kulazimisha jamii ichukue misimamo yao na iwe ya jamii nzima.wanalazimisha wanajamii waamini na kufuata imani zao na misimamo yao.hii kwa kweli ni trend mbaya sana kwa wanahabari wetu.wabadilike haraka
 
Mtu akisha itwa Yahya anakuwa hana tofauti na sheikh magirini, Yahya Hussein
 
Mtu akisha itwa Yahya anakuwa hana tofauti na sheikh magirini, Yahya Hussein
comment za namna hii hazisaidii, fikra nzuri ni kusema kile unachodhani alipaswa kufanya..yahya has been one of gud journalist kwa mtizamo wangu japo nakubali kwamba kama amesema hivyo atkuwa amekosea, anyway tu binadamu ni kawaida kukosea
 
Mtu akisha itwa Yahya anakuwa hana tofauti na sheikh magirini, Yahya Hussein
Kama uligundua,Paul Mabuga alimuona mwenzake anaenda offline akakatiza na kuweka sinema ya baba wa Taifa na baadae kibonzo,Yahaya Hussein uwa ana busara na ni kati ya watangazaji ninao waheshimu,ila inabidi akubali kuwa alipotoka kuanza kuelezea hisia zake binafsi huku akiwakilisha jamii ''watu wamechoka kusikia habari za Dr Ulimboka" angesema mimi nimechoka kusikia habari za Dr Ulimboka,kwani nina uhakika lile alilolisema hajawahi kulifanyia utafiti wowote na haliwakilishi mawazo ya jamii.Kwa stahili hii kuna siku anaweza kusema watu wamechoka kusikia habari za Marehemu Mwangosi
 
Kati ya watangazaji walio makini na neutral Yahya ni mmoja wao nafikiri hapo alipotoka tu akubali niugwana then gurudumu la utangazaji liendelee
 
Mkuu Lwesye, Siku hizi kuna kitabia fulani ..kwamba mtazamo wa mtu mmoja(however how powerful, famous, or insignificant in the society he/she might be) kuchukulia "mawazo" yake ndio mtazamo wa wananchi "wote".

Na mara nyingi ni kwa watangazaji a Runinga na Redio.
BADILIKENI.
Yahaya sijui kapatwa na nini leo ni mtangazaji makini mno,akiwa kwenye kipindi wengi wetu tunapenda tusikose kipindi chake lakini leo kafanya maoni yake eti yawe ndio reality,anasema basi inatosha hakuna sababu ya kureport habari za Dr Ulimboka waandishi wakireport watafanya nchi isitawalike ,hivi kweli yahya anajua kabisa utata wa Mkenya kuwa ndio muuaji,Tume ya KOVA kugeuka bubu bado anahitimisha kuwa wananchi tumechoka kupata ukweli kuhusu Dr Ulimboka
 
Ni mawazo yake na sio ya star tv hata na wewe ni mawazo yako ya kumuanzishia sredi lkn ingekuwa mimi ningem-PM! Tukubaliane ktk kutokukubaliana
 
Kama uligundua,Paul Mabuga alimuona mwenzake anaenda offline akakatiza na kuweka sinema ya baba wa Taifa na baadae kibonzo,Yahaya Hussein uwa ana busara na ni kati ya watangazaji ninao waheshimu,ila inabidi akubali kuwa alipotoka kuanza kuelezea hisia zake binafsi huku akiwakilisha jamii ''watu wamechoka kusikia habari za Dr Ulimboka" angesema mimi nimechoka kusikia habari za Dr Ulimboka,kwani nina uhakika lile alilolisema hajawahi kulifanyia utafiti wowote na haliwakilishi mawazo ya jamii.Kwa stahili hii kuna siku anaweza kusema watu wamechoka kusikia habari za Marehemu Mwangosi
Kweli kabisa Ngonani Paul Mabuga alimwangalia Yahaya Kwa mshangao akapotezea lakini tayari tukamsoma Yahaya na bado tunajiuliza je hii ndio sura halisi ya Yahaya au amepitiwa tuu,Manake kituo chao cha Star TV kinakuja vizuri sana ,je wanataka kuingia kwenye propaganda ,manake nimeskia Faraji Mwegoha akiwa Dodoma anawasemea wananchi wa Dodoma eti ni watu wenye busara wanafikiri kabla ya kutenda hawana ushabiki na jaziba za kisiasa hawaandamani kwani maandamano ni ujinga nakadhalika nakadharika hembu tuwape wiki tuone kama hawa hawatakuwa TBCCM-B na ikiwa hivyo basi watajiungasha kama gunia
 
Ni mawazo yake na sio ya star tv hata na wewe ni mawazo yako ya kumuanzishia sredi lkn ingekuwa mimi ningem-PM! Tukubaliane ktk kutokukubaliana
Ningeweza kumPM kama unavyoshauri hiyo pia ni njia moja wapo lakini kuanzisha thread nimepanua mjadala kwa sababu maoni yake aliyatoa kwenye chombo kinachoonekana Tanzania nzima,Mimi naishi Dar es salaam ,lakini sasa nipo Newala kikazi na nimeangalia Star Tv na KUmsikia Yahaya akisema hayo,ndio maana nikaliweka hapa kwa sababu ni memba mwenzetu hapa alijizolea heshima kubwa
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M
 
Tunahitaji watu kama wewe(Yahya Mohamed) wenye kutambua na kujirekebisha katika pale mtu anapojikwaa.

I am one of your fans na katika hili uko sahihi just be careful next time uweke msisitizo kwa jambo kuwa haya ni maobi binafsi kulingana na nafasi KUBWA uliyonayo katika jamii(kama mwanahabari), otherwise itachukuliwa kuwa ni TABIA YAKO(and at times tabia ya wanahabari).

Kazi njema.
 
Salaam Wakuu,

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M

Mkuu Nimpenda sana sehemu hiii...Safi sana umejizolewa watazamaji 1000 zaidi kwa kuandika haya
 
Safi sana Yahya Mohamed wote wamekusoma kwa kuja kuomba radhi kwa wale uliowakwaza.
 
Salaam Wakuu,

Hatua ya kuanzisha thread si mbaya, kama mnaweza kunisifia publicly si vibaya pia kunikosoa publicly. Yalikuwa maoni binafsi na hayakulenga kumdhihaki mwanahabari yeyote, ama kuufunga mjadala juu ya Dr.Ulimboka kwani si jukumu langu wala sina dhamana hiyo.

Inawezekana kabisa kuna kupishana katika mawazo juu ya jambo fulani, hakumaanishi mtandao wala kumtumikia mtu yeyote kwa manufaa binafsi.

Napenda kutambua na kuheshimu kupishana huko katika fikra, lakini pia kuomba radhi sana kama matamshi yangu yamekwaza harakati muhimu katika sakata hili.

Maangalizo na Ushauri umezingatiwa.

Ahsanteni Wanajamvi

Yahya M

Umetupa faraja mwanaJF mwenzetu kwa hekima na busara zako!
 
Back
Top Bottom