Mhere Mwita
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 235
- 1,275
Hadi tuongeavyo, marais wa Mauritania na Guinea wako nchini Gambia ambako wamekuwa wakimsihi Yahya Jammeh aondoke kwa salama na amani (wanambembeleza).
Dakika chache kutoka sasa wanatarajiwa kumpa machaguo mawili tu yaliyobakia. Moja ni Jammeh akubali kuondoka na Marais hao wawili na kwenda nje ya Gambia (Ambako nchi kadhaa ziko tayari kumpa makazi).
Mbili ni Jammeh akubali kuondolewa kwa nguvu ya majeshi ya ECOWAS. Dakika chache zijazo, ECOWAS inaweza kumuongezea Jammeh muda wa msamaha wa saa moja hadi mbili kabla ya kuanza kutumia nguvu.
Note; Majeshi ya ECOWAS tayari yako Banjul huku vikosi vya majeshi ya Gambia vikitii amri ya Rais mpya, Adam Barrow ya kusalia makambini na kutofanya chochote.