Yahusu mapambano ya madawa ya kulevya

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Kumekuwepo na vita inayoitwa ya madawa ya kulevya vyovyote tutakavyoita ikiwa kama wapiganaji wanapigana sababu ya kupata umaarufu wa kisiasa, au kwasababu ya nia yao ya dhati na dhamira ya dhati ya kutaka kuona vijana wetu hawapati madhara yatokanayo na madawa ya kulevya, vyovyote vile vita hii ni muhimu lakini ni pana mno ni zaidi ya kupambana na wafanyabiashara ya madawa ya kulevya.

Matumaini yetu ya kushinda vita ya madawa ya kulevya ni madogo kama hatutapambana uovu wote. Madawa ya ulevya ni zao la uovu mwingine ambao upo katika jamii. Kama tunataka kupambana na madawa ya kulevya kwa kutumia nguvu pekee hatutashinda ni lazima kuwe na approach zaidi ya moja.

Ni lazima tuangalie tunavyoishi ndani ya familia zetu wazazi lazima wawajibike ipasavyo katika kuwalea watoto katika njia zilizobora na kujua wajibu wao kwao binafsi na kwa jamii inayomzunguka. Vijana wasipojua wajibu wao kwa kijamii na wajibu wao wa kitaifa hakuna cha maana tutakachojenga.

Vijana wetu kuuza madawa au kufanya mambo mengine yenye madhara kwa jamii ni kutokujua wajibu wao au kutokuwa na elimu ya kutosha na kutokujua nafasi yao katika jamii. Order katika nchi yetu itategemea sana jinsi tunavyowalea vijana wetu. Nidhamu yao inategemea hilo pekee. Kwa kijana kujiingiza kwenye uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya kuna matatizo katika malezi. Na katika jamii tatizo ambalo tunatakiwa kuliangalia kwa ukaribu sana kwenye mifumo yetu.

Sawa tuna polisi lakini tusipoelimisha watoto wetu na kuwalea vijana wetu vyema kila siku tutaongeza pesa kwenye bajeti ya kuongeza polisi na vituo vya polisi, kuongeza mahakama na kufunga vijana wetu wengi. Haya matatizo ya kijamii lazima yaelezwe na yatafutiwe njia ya kuyatatua ili yasiwe yanaibuka ibuka.

Hatuwezi kumaliza suala la madawa ya kulevya kwa nguvu peke yake. Matatizo ya kijamii ambayo tunayokabiliana nayo sasa ni lazima tunayaangalie katika mifumo yetu ya makuzi na malezi na mahusiano yetu. Lazima tuangalie katika tabia tunazozijenga kwa watoto wetu na vijana wetu. Kuwafunga watu kwasababu ya kutenda visivyo sahihi pasipo kuwa na mifumo mizuri ya malezi na makuzi ni kuendelea kila siku kuongeza gharama katika kujenga vituo vya polisi na jela wakati tunaweza kuzuia haya mambo kama tukiwa na malezi na makuzi mazuri. Na kama tutatoa elimu bora ya maadili kwa watu wetu. Ni lazima tufanye hivi ili kupunguza uhalifu na matumizi ya hela nyingi kwenye kudhibiti uhalifu.

Ni lazima tuangalie upya mahusiano yetu na mashirikiano yetu. Kwasababu bila kuwa na mahusiano mazuri na mashirikiano mazuri matatizo mengi ya kijamii hatutaweza kuyatatua ikiwemo suala la madawa ya kulevya ambalo linahitaji nguvu ya pamoja ili kulimaliza. Hatutaweza kumaliza matatizo ya kijamii ikiwa kila mtu atajifungia nyumbani kwake na kama hakutakuwepo muda wa kuyajadili na kutafuta ufumbuzi wake. Kama tunataka tutibu matatizo ya jamii yetu hatuna budi kuwa watu wamoja katika mawazo yetu na matendo yetu. Kama hatutakuwa wamoja katika mawazo yetu na matendo yetu, changamoto nyingi ambazo zinatukabili kama taifa hatutaweza kuzitatua kama mawazo yetu tutayaelekeza kwenye ubinafsi na sio kwenye utatuzi wa changamoto zinazotukabili pamoja kama taifa.

Kama kila mtu akiangalia maslahi yake binafsi na sio maslahi ya taifa hatutaweza kujenga hili taifa, na hapatakuwa sehemu nzuri ya kuishi. Kama tunataka kujenga jamii nzuri ni lazima tuangalie tabia za watu wetu na mahusiano yao.

Mahusiano yetu ni muhimu katika ujenzi wa taifa imara. Ni lazima tuangalie malezi ya watoto wetu kwa ukaribu na kuwafanya wawe watii kama wazazi wakishindwa kuwaongoza na kuwatawala watoto wao vyema hakuna jamii itakayobaki na mfumo mzima wa kijamii utaharibika.

Ni lazima wazazi wawe na uwezo wa kuwatiisha watoto wao na kuwaongoza katika njia yenye maadili. Kama wazazi wakiwa wamekengeuka tutegemee nini kama jamii? Sio kuharibika kwa taifa letu na mfumo mzima wa kijamii?

Leo tunahangaika kuhusu madawa ya kulevya na hata kuongezeka na tabia za mbaya ndani ya jamii ni malezi yetu yaliyotufikisha hapa. Tumeshindwa kuwatiisha watoto wetu kuwa na adabu na nidhamu na kuheshimu masuala ya msingi yanayohusu maisha.

Kama ndoa zetu haziko imara tusitegemee kwamba ndoa za watoto wetu zitakuwa imara. Tunawafunza nini watoto wetu kama hatuheshimu ndoa zetu? Kama tusipokuwa wakali kwa watoto wetu tusahau kitu kinachoitwa maadili. Tuongeze tu vituo vya polisi na mahakama badala ya kuwalea vizuri tukawafunge huko lakini matatizo yataendelea kuwepo kwkaakuwa hatujatoa kiini cha matatizo yetu.

Tatizo jingine ni ubinafsi kila mtu anajiangalia mwenyewe na sio jamii na matatizo yanayohusu jamii. Kama kitu hakijakutokea wewe hujali. Kama mtoto wako hatumii hujali. Tunaona kitu ambacho si sahihi kinatokea mitaani kwetu hatuchukui hatui hata kama bhangi zinauzwa kwenye mitaa yetu. Ili haya mambo yaishe ni lazima tuwe na dhamira ya dhati ya kutaka kuondokana na uovu. Na wenyeviti wa mitaa ambao wamepewa wajibu wa kuona haya mambo hayapo lazima wawajibike.

Kama uovu ukiongezeka na kama hatua hazitachukuliwa mapema, kila wakati njia ambazo zitakuja kuchukuliwa baadae huwa ni ngumu za kusikitisha za kuogofya. Ni muhimu kuzifanya roho za vijana wetu kuwa nzuri na njema kabla njia kali na za kusikitisha hazijaja kuchukuliwa wakati jamii itakapokuwa imeharibika sana. Tunajifunza hili kila wakati na historia ni mwalimu mzuri.

Naungana mkono na mapambano ya madawa ya kulevya lakini zaidi ya yote moral education ipewe kipaumbele kwenye mashule yetu na katika familia zetu kwasababu our very foundation of our state depend on our morality. Doing what is right, just and fair and not harm to another fellow human being. Ikiwemo kumuuzia madawa raia mwenzako na kutokujali maisha ya mwenzako.
 
Back
Top Bottom