Yahitaji kichwa ngumu kuielewa CCM kama ni ndege fuata upepo

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
Ni wana ccm wachache sana ambao ni wasoma nyakati na wenye busara au wenye utashi wa kisiasa kama Mama Samia Suluhu Hasaan au Jakaya Kikwete

Kundi kubwa la wana ccm ni fuata upepo hawajui wanachokisimamia wala wasimame kwa msimamo upi?

Waliopinga katiba mpya na kuharibu makongamano ya Katiba ni wana ccm fuata upepo ambao hawaelewi hata maana ya katiba na utawala wa sheria

Wana ccm wanaojielewa kama akina Jaji Warioba waliposimama na kuwaambia wana ccm fuata upepo kuwa Katiba ni muhimu na lazima kuna siku nguvu ya uma itazidi nguvu ya chama, Warioba aliitwa kila aina ya majina ya msaliti lakini Leo ndio shujaa

Wana ccm fuata upepo ndio walitamka hadharani katiba sio chakula wala kipaumbele cha Taifa, Kipaumbe Chao kilikuwa tarumbeta kuwa na atawale daima na milele kumbe wakasahau mwanadamu ana lifespan ya kuishi na haizidi miaka 100.Wenye bahati zao hufika miaka 120 wakiwa hoi na taabani na Wengine wameanza kutambaa kama watoto

Wana ccm walipaswa kuwaomba msamaha Chadema hadharani , Baadhi ya viongozi wa dini na wana ccm wenye utashi wa kisiasa kama Jaji Warioba kwa kuwadhalilisha waliposimama kupigania katiba mpya

Leo ccm kwa utashi wa Mama Samia Suluhu Hassan na baadhi ya wazee wenye heshima imewakumbusha ccm fuata upepo kuwa mchakato wa katiba ni muhimu sana

Wana CCM fuata upepo wamejitengeneza ili kuweza kupata teuzi mbalimbali na kukumbukwa, wana ccm fuata upepo ni vigeugeu, wanafiki na hawana mishipa ya aibu hata kidogo

Rais Samia hatakumbukwa kwa lolote lile bali atakumbukwa na kusomwa kwenye vitabu vya Taifa hili kama atafanikisha mchakato wa nchi kuwa na Katiba Mpya safi na ya kisasa

Hakuna anayemkumbuka Nyerere kwa kujenga reli ya Tazara au kuanzisha University of Dar es Salaam bali anakumbukwa kwa kuliunganisha Taifa lililokuwa na tamaduni na mila tofauti kuwa Taifa moja
 
Walivyo mbumbu nao wataanza kuimba tena ;nani kama Samia
 
Hata JK nae ni fuata upepo vile vile, kama kweli angekuwa anajitambua angehakikisha ule mchakato wa Katiba Mpya aliouanzisha anausimamia na kuuukamilisha, lakini matokeo yake alikubali kufuata ushauri wa hao wafuata upepo nae akahamia upande wao.

Nina wasiwasi na Samia nae ataingia kundi hilo hilo, ni suala la muda tu majibu yatapatikana, kama wale Covid 19 bado mpaka leo wako bungeni licha ya mahakama kutupa ile kesi yao, nani anaewalinda? naona dalili hata Samia nae anafuata mawazo ya wenzake wafuata upepo.
 
Back
Top Bottom