Yahaya Hussein amtabiria rais mwenye jina K....

Pengo

JF-Expert Member
Oct 15, 2009
579
10
Jana jumatatu 01/02/2010,Nilikuwa naangalia TV ya channel 10 kipindi cha nyota zenu na sheikh Yahaya, nilishtushwa na utabiri wake ambao kimsingi alisema "Mwaka huu kutatokea kifo cha kiongozi maarufu ambaye jina lake linaanzia na S ikifuatiwa na H, vilevile mwenye jina linaloanzia na K.

Baada ya kuongea jilo ndipo alipokoroga kabisa kwa kusema "Natabiri, uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka huu hautofanyika na utahairishwa kutokana na tatizo litakalojitokeza "Tena akaongeza "Hata kama tatizo hilo litatokea Zanzibar basi litasababisha uchaguzi mkuu wote kuhairishwa, na anayebisha asubiri aone"

Akanitisha zaidi pale aliposema "watu wanaogopa kifo wakati kifo ni lazima,watanzania msihofu kufa kwani hata Yesu alikufa ili kuwakomboa walimwengu"

Ndugu zangu,kama ya Yahaya yana ukweli inamaana tutegemee matatizo kutokea hasa kifo cha kiongozi anayeanzia kwa jina la K, sasa hapa TZ ni nani hao wenye majina yanayoanza na K kama si Kikwete, Karume.....?

Naomba tujadili!
 
K wapo wengi tu, labda kwa marais ni hao. S na H je? Sharif? anyway hayo ni yake, mimi naamini katika Mungu na maandiko yanasema hakuna anayejua saa wala muda...
 
ujinga mtupu,kama kweli mtabili si ataje kabisa jina sasa hapa anacheza na probability tu,hakuna lolote
 
Duh hii hatari kubwa sana Sheikh Yahaya alitabiri atakaempinga kikwete ndani ya CCM atakufa,.Uchaguzi mkuu unaweza kuahairisha iwapo mgombea urais au makamu wake atafariki.Ingawa mimi si muumini wa mambo ya utabiri lakini anaetabiriwa kifo hapa ni Kikwete sio Dr karume kwasababu ameshasema hatagombea urais wa zanzibar.

Sheikh Yahaya anatakiwa kukamwatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuatarisha usalama wa taifa.Natumaini safari hii huyu sheikh feki atawajibika kwa kauli zake zenye utata
 
Hiyo ndiyo astrology amini usiamini lakini ndiyo hivyo. time is the best judge of things to come.
Binafsi siamini mambo hayo lakini kuna mambo yaliyotokea huko nyuma ambayo huyu mzee alitabiri na yakatokea hivyo im keeping mum
 
hapa ni mkulu manake kweli karume hatagombea then si hatakuwa na mpinzani coz ukimpinga utadead ghafla. it means hii kitu itasababisha uchaguzi kuahirishwa. haaa!! dis dude is kidding now, im telling u. how come?
 
Jana jumatatu 01/02/2010,Nilikuwa naangalia TV ya channel 10 kipindi cha nyota zenu na sheikh Yahaya, nilishtushwa na utabiri wake ambao kimsingi alisema "Mwaka huu kutatokea kifo cha kiongozi maarufu ambaye jina lake linaanzia na S ikifuatiwa na H, vilevile mwenye jina linaloanzia na K..QUOTE]

Huyu nae mwizi tu!

Kwa nini asiwataje kwa majina kama ana uhakika na analolisema?

Huyu ni 'shehe' kweli au mganga wa kienyeji aka mchawi!?
 
aah mie nikashangaa pale aliposema uchaguzi mwaka huu utaahirishwa ..na akaendelea kukazia teteteteeh kweli utabiri;)
ngoja tuone
 
Ha ha. Halafu Jerry Muro anakamatwa. Badala akamatwe huyu mtu for "high treason"!!
Kwa hiyo mwaka huu anakufa Shein na Kikwete au Karume.
Tena amesema on (almost) national TV halafu anaachiwa hivi hivi. Kama si kweli kuwa hawa wanasiasa huwa wanaenda kwake, basi wajitokeze na kumpa onyo!!

Halafu, huyu jamaa ni kiongozi wa kidini, na ninavyofahamu dini ya kiislamu kama ilivyo ya kikristo hairuhusu usomaji nyota/ utabiri!! Sasa BAKWATA au baraza la mashekhe wamelala? Mbona huyu anaruhusiwa kuongoza ibada?
 
hawa ndio wenye S
Salim
Slaa
Selelii
Sitta
Simba

hawa ndio wa H
Hosea
Husein (Mwinyi)
Harrison (Mwakyembe)

hawa ndio wenye K
Kingunge
Kikwete
Kabwe
Karamagi
Karume

kaaaaaaaazi kwelikweli
 
Back
Top Bottom