Wajuzi hii imekaaje? Kwa sasa Nembo ya Taifa (Coat of Arms), ni kama vile imebadilishwa hasa rangi na kupoteza uhalisia wake.
Ukifuatilia hotuba za rais Samia, nembo hii inakuwa ina rangi kama ya damu ya mzee, au ya mbao hivi, tofauti na uhalisia wake.
Hivyo, waandaji wa hafla za rais jitahidini muwe mnaweka Nembo yenye rangi halisi ya Taifa (Coat of Arms), mbele ya rais kama mtaona inafaa, ili kuendeleza historia ya nchi.
Hapo chini nitabainisha nembo halisi na hii nembo ambayo imechakachuliwa ila inatumika kwenye hotuba za rais kwa sasa.
Kwa wasiofahamu, nembo ya taifa (Coat of Arms), ni nembo rasmi ya serikali. Hii hutumika kama muhuri rasmi wa serikali ya Tanzania.
Nembo hii imebeba ujumbe mbalimbali ndani yake, hivyo kuibadilisha hata rangi tu, basi hupoteza uhalisia wake. Kwa mfano, nembo halisi ya taifa ina mimea miwili ya pamba na karafuu, swali, je hayo mazao yataonekana vipi ikiwa rangi ni damu ya mzee badala ya kijani?
Kwa ufupi, nembo ya taifa halisi imebeba vitu 12 vyenye maana zake, ambavyo vinatakiwa viwe katika rangi halisi kama ifuatavyo, kwa kifupi lakini:-
1. Watu wawili-mwanaume na mwanamke.
-Humaanisha, nchi itajengwa kwa ushirikiano wa wanaume na wanawake.
2. Ngao na Mkuki (Shield and Spear)
-Huwakilisha silaha zilizotumiwa na Watanzania wakati wa kupinga ukoloni.
3. Ufito wa rangi ya dhahabu (Golden band) sehemu ya juu ya ngao.
-Huwakilisha utajiri wa madini yanayopatikana nchini.
4. Moto unaowaka katika mwenge wa uhuru.
-Huwakilisha uhuru na nuru.
5. Bendera ya taifa.
-Huwakilisha Tanzania ni nchi huru.
6. Ufuto mwekundu katika ngao (Red band on the shield).
-Huwakilisha udongo wa rutuba unaopatikana nchini.
7. Shoka na Jembe (Axe and Hoe).
-Huwakilisha vifaa vilivyokuwa vinatumiwa kuiendeleza nchi.
8. Mawimbi ya bahari (Sea waves).
-Huwakilisha vyanzo vya maji vinavyopatikana Tanzania.
9. Kilele cha mlima Kilimanjaro.
-Huwakilisha mlima mrefu Afrika unaopatikana Tanzania.
10. Mazao-Pamba na Karafuu.
-Huwakilisha mazao ya biashara yanayolimwa Tanzania.
11. Maneno "Uhuru na Umoja".
-Huu ni moto/motto (kionjo) wa nchi yetu.
12. Pembe mbili za ndovu.
-Huwakilisha urithi wa nchi yetu katika nyanja ya wanyama.