Yah:DC Rugimbana na bomoabomoa ya wavamizi na wakimbizi MADALE na kwingineko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yah:DC Rugimbana na bomoabomoa ya wavamizi na wakimbizi MADALE na kwingineko

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kupelwa, Aug 30, 2012.

 1. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Kwa takribani kama siku tano hivi, maeneo mbali mbali wilayani kinondoni hasa mapori ya madale karibu na magereza ya boko, kulifanyika bomoabomoa ya wavamizi iliyosimamiwa na mkuu wa wilaya na RPC wa kimkoa wa kinondoni.bomoa bomoa hii ilikwenda mbali na kuhamia maeneo mengine kadhaa wilayani kinondoni na hasa kata ya wazo.Alipouulizwa mkuu wa wilaya na RPC kinondoni wanatekeleza ubomoaji huu kwa amri gani,walijibu,"ni kwa amri ya mahakama".amri hiyo ya mahakama ilikuwa inataka ubomoaji wa kaya sita kwenye soko moja maeneo ya madale, ambayo pia hukumu haikuzingatia walalamikiwa kuwa hawakutakiwa kuwa wananchi bali manispaa ya kinondoni ambayo ndo anatakiwa kumiliki soko.Pia maelezo yao yalienda mbali zaidi kuwa kuna wakimbizi ambao ni mungiki wamevamia mashamba ya watu na kuwa tishio kwa maisha ya wamiliki wa mashamba hayo.
  jana kwenye ,kipindi cha pambanua, wanasheria wa LHRC walijaribu kuchambua kisheria na kisiasa kuhusu haki na mazingira yalitumika katika bomoabomoa hiyo, kumeonyesha mapungufu mengi kama ifuatavyo;
  1.haikuzingatia haki ya upande wa wavamizi/wakimbizi nao hata kama walikuwa wakimbizi , kwa sababu kati yao wana haki ya kuwa maeneo hao walipewa kwa taratibu za kiuongozi , enzi hizo mkuu wa mkoa makamba aliwapa maeneo hayo sababu wenye mashamba hayo waliitwa wayaendeleze lakini hawakuonekana, hivyo makamba akawapa kwa nyaraka sahihi.
  2.wlalamikaji wa mashamba yaliyovamiwa, walienda mahakamani kuomba haki ya wavamizi hao kuondolewa kisheria, na kesi yao ilikuwa inatajwa jana, lakini kabla ya mahakama kutoa nani mmiliki halali wa maeneo hayo, tayari mkuu wa wilaya na RPC alikuwa ametekelza ubomoaji huo bila mahakama idhini hiyo.
  3.amri ambayo ilikuwa ya kubomoa kaya sita ambazo zinalalamikiwa kuwa ni soko na mmoja wa walalamikiji, ilikuwa ya kaya sita tu.na pia amri hiyo tayari ilikuwa imepingwa mahakamani sababu walalamikiwa si manispaa ya kinondoni ambaye ndo mmiliki wa soko.lakini tayari huku kukiwa na kesi ya kupinga hukumu hiyo bado ipo mahakamani, mkuu wa wilaya na RPC walikuwa wanaendesha bomoabomoa hiyo.
  4.Je, kama ilikuwa amri ya kaya sita , na ilikuwa imepingwa mahakamani iweje kubomoa makazi ambayo hayakuwa kwenye hukumu na amri hiyo , huku RPC anafurahia kufanya hivyo kwa kuchoma mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo.
  5.je kama kweli walikuwa wakimbizi na wahalifu , uhamiaji imekuwa wapi miaka yote taratibu za kisheria zifuate ?na je inakubalika kuharibu mali za mkimbizi bila kuwa na ushahidi wa wazi na ulithibitishwa?
  katika mada hii nisingependa kuwwatetea watakaothibitika kuwa kwli ni wavamizi, je kama hatawatakuwa wavamizi , huo uharibifu wa mali na makazi ya familia 1000, nani atawafidia?je kwanini mkuu wa wilaya na rpc kama kunawavunja sheria za jinai kama kutishia, kubaka, kujeruhi, kwanini asingewashughulikia ipasavyo hicho kikundi kuliko kubomoa makazi ya watu wote hata wasonkuwa na makosa?piakulikuwa na kesi mahakamani , je DC RUGIMBANA na RPC wako juu ya sheria za nchi na mahakama?na pia , je srikali hii ya ccm inafurahia kuona wananchi wake wakiwa hawana makazi wanalala nje bila chakula, na namna nyingine ya kujikimu kimaisha.
  ikumbukwe, diwani wa wazo, mwenyekiti wa serikali ya mtaa, wajumbe wamekiri hawakushirikishwa katika zoezi hili ambalo linapingana na haki za binadamu.
  TAFAKARI:WAPI SERIKALI YETU YA CCM INATUPELEKA?NDO UTEKELEZWAJI WA AGIZO LA PINDA LA MADC KUKOMOA WANANCHI ILIKUSUDI CCM IENDELEE KUTAWALA?
  CHANZO:LHRC
   
 2. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,403
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  We ni mwandishi wa habari?mnatafuta negativity tu hamuangalii positivity na watu waliokuwa wanatapeliwa na hao unaowatetea kwa kuuziwa maeneo feki ya kichina,,,imefika wakati weka uchama pembeni kama serikali imefanya kitu kizuri yastahili kupewa pongezi kwa hatua hiyo,labda na wewe ungepigwa changa la macho na hao wavamizi ndio ungenyoosha usemi huo.
   
 3. G

  Gwakisa Mwandule JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 520
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Usijikite kwenye issue za uchama hivi wewe hujiulizi hawa jamaa wanataka kutupeleka wapi?Kama mtu ni mkimbizi na ni muhalifu ni jambo zzuri lakini kuhusu mambo ya ardhi siungi mkono maana pale boko chasimba mgogoro ni kati ya kiwanda cha wazo na wananchi,na kimsingi wazo ndio wenye makosa makubwa kwa kushirikiana na serikali kupora yale maeneo ambayo hawayaendelezi na wala hawayahitaji kama wananchi wanavyoyahitaji
   
 4. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Serikali ipime maeneo ya kutosha na iuze viwanja kama ilivyokuwa mradi wa viwanja 20,000 ili kuondoa usumbufu kwa wananchi na hasa masuala ya kutapeliwa.
   
 5. M

  Mwanaharakatihuru JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2012
  Messages: 479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ungebomolewa nyumba ndio ungejua nyambafijo
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  Kinondoni Kuna Uozo Mwingi Kila Kona!! Huyo rugimbana ameona Huko madale tu? tena jimbo la cdm?
   
 7. Bouncer

  Bouncer JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Bora tupumue, hawa wavamizi walikuwa wanatunyima usingizi kwa kweli. Wote watakaobainika sio watanzania warudishwe makwao. Majitu yameua na kubaka huko kongo, Burundi na Rwanda kisha yanakuja kujificha kwenye mashamba yetu. Good work Kinondoni.
   
 8. Bouncer

  Bouncer JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 30, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Wao wanapobomoa au kutaifisha na kukaa kwa nguvu kwenye nyumba za wamiliki halali wa maeneo ni sawa!!!!??

   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  We ni mwandishi wa habari?

  Yeye ni JF member mwenye haki ya kutushirikisha wana JF wengine.

  mnatafuta negativity tu hamuangalii positivity na watu waliokuwa wanatapeliwa na hao unaowatetea kwa kuuziwa maeneo feki ya kichina,,

  Mimi ni mkazi wa eneo hilo la soko na mtoa thread ameeleza kwa ufasaha suala hilo na LHRC. Usichokijua polisi wako wameingia kwenye nyumba zetu (nje ya eneo la mgogoro) kwa nguvu, yaani wamevunja milango na madirisha na kuiba vitu pamoja na fedha taslimu. Nenda polisi Wazo kaulize wanavyohaha kulizima tukio la kijambazi walilolifanya baada ya kufunguliwa RB. Hapa ni suala la kutenda haki kwa anayestahili bila kuwaathiri asiyestahili

  ,imefika wakati weka uchama pembeni kama serikali imefanya kitu kizuri yastahili kupewa pongezi kwa hatua hiyo,labda na wewe ungepigwa changa la macho na hao wavamizi ndio ungenyoosha usemi huo.


  Hapa siyo suala la uchama, ni suala la kupotosha taratibu tulizonazo kwa maslahi fulani. NAKUULIZA INGEKUWA WEWE UMEFANYIWA KILICHOFANYWA NA NAMNA KILIVYOFANYA UNGEJISIKIAJE?

  Nielewavyo mimi naona serikali ya CCM inadhihirisha kilicho ndani ya mioyo yao (ufisadi); wanaacha kuwasimamia watendaji wa serikali ili wao waendelee kuhujumu nchi kwa kutupatia kila aina ya shida.
   
 10. zubedayo_mchuzi

  zubedayo_mchuzi JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 4,922
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kuwa mtazamaji nayo ni tiba
   
 11. Chimbuvu

  Chimbuvu JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 4,403
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 145
  kunakitu kinaitwa long term plan mkuu samahani kama nitakuita mtu asiyefikiria mbele nisamehe kwa hilo lakini ndivyo inavyoonyesha,viwanda huwa vinakua kutokana na demand na population ya watu kwa wazo kushindwa kuendeleza sa hv siyo kuwa watashindwa miaka kumi ijayo,maana hamkawii mkiachiwa muende tu mtaanza kulalamika makelele ya kiwanda.
   
 12. p

  puto Member

  #12
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 84
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 25
  mtoa mada yuko biase coz wakati wamiliki halali wana pigwa na kubakwa wamizi pindi walipo wanaenda kwenye maeneo alikuwa kutoa hoja zake?
   
Loading...