Yagundulika kuwa Tanzania tumepiga ramli kujua kuwa hatuna tena wagonjwa wa Covid-19 nchini na kuutangazia ulimwengu hivyo

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Njia pekee ya kutoa matangazo rasmi kwamba mikoa ya Tanzania haina tena watu walioathirika na virusi vya Covid-19 ni kama tumeenda kuwauliza waganga wa kienyeji na wao ndio wakatupa huo uhakika.

Haingii akilini katika karne hii ya 21 kwamba tunajua kwamba mtu anaweza kuwa na virusi vya Covid-19 na asionyeshe dalili zozote za kuumwa, halafu tunasema hakuna wagonjwa wa Covid-19 Tanzania. Imani iliyoonyeshwa katika kuomba Covid-19 iishe isiwe msukumo wa kutangaza rasmi kwamba sasa hatuna tena Covid-19.

Je, tumefanya utafiti gani na kujihakikishia kwamba hatuna wagonjwa? Tumepima watu wangapi na katika maeneo yepi na kuona kwamba karibu 100% ya tuliowapima hawana virusi vya Covid-19 na hivyo ni halali kwetu kutangaza kwamba mikoa na Tanzania kwa ujumla haina wagonjwa wa Covid-19?

NIlishasema humu JF, hebu Ummy Mwalimu ajaribu hapa Dar angalau aende sehemu kama soko la Kariakoo, Manzese, Temeke, Tandale halafu apime watu "randomly" angalau 50 kila siku. Akikuta katika hawa 50 aliowapima 40 hawana Corona virus basi nitamuunga mkono kutangaza kwamba Tanzania hatuna Covid-19.

Suala la Wakenya kupima madereva wa Tanzania na kukuta kwamba labda 40% ya wanaowapima wana Covid-19 tusilichukulie kisiasa na kuanza kuwatukana Wakenya. Tunapaswa tuone ni dalili kwamba kuna kitu hakiko sawa Tanzania. Tunapaswa kuwashukuru Wakenya kwa kutuonyesha hilo na kufuatilia suala la upimaji badala ya kuwalalamikia.

Ni wazi kwamba haya matangazo ya Ummy yanalenga kumfurahisha Magufuli, lakini hayana mshiko wowote wa kisayansi. Na ndio maana tunakata shauri kwamba ili kutoa tangazo kwamba hatuna tena Covid-19 basi lazima itakuwa imepigwa ramli.
 
Tulia kijana corona ni gonjwa kama magonjwa mengine mbona hausemi tupime na malaria au lenyewe sio gonjwa na haliui.

Huko kutokutangaza hauoni kama kumesaidia yani huko kutangaza ni kutia hofu bure watu na hofu ni mbaya kuliko hata hilo gonjwa.

Kikubwa kuwa na tahadhari hiyo idadi ya wagonjwa haita kusaidia chochote wewe ni kukuingezea hofu tu
 
Ati wasema, kwa kujiamini, uzushi, mbwembwe na bila aibu, kwamba matangazo ya Ummy yanalenga kumfurahisha Magufuli. Kwa jinsi mnavyomchukia Rais, CCM na Serikali yake, hakika mngechukua waandishi wa habari, wa ndani na nje, mkavamia hospitali au kituo cha wenye maambukizi,ili kuutangazia ulimwengu jinsi wagonjwa walivyofurika.
 
Lakini madaktari kupitia chama Chao Cha MAT waliunga mkono hakuna wagonjwa Hospitali na Wala mochwari hazikuongezeka maiti wengi kuashiria vifo vingi.

Ninavyoona Corona ipo lakini haiuwi sana Kama ilivyodhaniwa, so watu wazee na wenye pre existing conditions wachukue tahadhari Ila hatuwezi kuchukua hatua extreme
 
"Mikoa ya TZ isiyo na Mgonjwa hata mmoja wa corona ni Dodoma, Mtwara, Pwani, Kigoma, Songwe, Rukwa, Mara, Lindi, Geita, Pwani, Katavi, Ruvuma na Simiyu, sio tu maambukizi mapya yamepungua bali hata Wagonjwa Hosp. wameendelea kupungua kila siku" -
@ummymwalimu
#MillardAyoUPDATES
 
"Tunaelekea kuimaliza corona Tanzania, Mimi na Mganga Mkuu tutapitia upya mpango wa Taifa kuhusu covid19 tutabadilisha kauli mbiu badala ya dhibiti corona iwe tokomeza corona sababu tayari tumeidhibiti, hata hivyo tuendelee kuchukua tahadhari" -
@UmmyMwalimu
#MillardAyoUPDATES
 
Nimeisikia asubuhi hii kwamba kampeni iliyopo kwa sasa ni tokomeza korona baada ya ile hatua ya kuthibiti korona kufanikiwa kwa kiasi kikubwa..
 
Haingii akilini katika karne hii ya 21 kwamba tunajua kwamba mtu anaweza kuwa na virusi vya Covid-19 na asionyeshe dalili zozote za kuumwa, halafu tunasema hakuna wagonjwa wa Covid-19 Tanzania. Imani iliyoonyeshwa katika kuomba Covid-19 iishe isiwe msukumo wa kutangaza rasmi kwamba sasa hatuna tena Covid-19.

Mkuu kama ulivyo andika hapo juu kuna tofauti kati ya mtu kuwa na maambukizi ya Corona Virus na kuwa na ugonjwa wa COVID 19 (huyu anaonyesha dalili za ugonjwa). Na ndio maana takwimu sahihi zinatakiwa zitenganishe hayo mawili. Inawezekana wagonjwa wakawa wachache lakini walio ambukizwa wakawa wengi.

Hii tofauti ndio ili muathiri Mwele kuhusu Zika samples zilionyesha uwepo wa vidudu lakini sio ugonjwa. Yeye akatangaza ugonjwa walioshika mpini wakamla kichwa.

Tukirudi kwenye COVID-19 wagonjwa hupatikana hospitali na majumbani, hivyo kiuhalisia na kisayansi inatakiwa ifanyike savei (survey) kwenye vituo vya afya na majumbani ili mtu aseme kwa uhakika kuwa hatuna wagonjwa kwa siku fulani au juma fulani, lakini bila takwimu za maambukizi unakuwa unajipa matumaini ambayo kiuhalisia hayapo. Bila vipimo huwezi kujua hali ya ugonjwa.
 
Back
Top Bottom