Yafuatayo yatatukwamisha kufikia Tanzania ya Viwanda

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
1.Watanzania wengi tunajua kuongea sana pasipo kuyatenda tunayoyaongea - hii ni kwa wote ;viongozi na wananchi

2.Viongozi wetu walio wengi kipaumbele chao ni kutaka heshima na kuogopwa kuliko kutimiza majukumu yao

3.Watanzania wengi tunaushabiki hata kwa mambo tusiyoyafahamu undani wake

4.Baadhi ya viongozi waandamizi hawajui namna bora ya kuwasimamia walio chini yao ili kupata end result iliyo bora badala yake wanaongoza kwa vitisho na mikwara

5.Watanzania wengi bila kujali hadhi na nyazifa zetu tuna ulimbukeni na tunajifanya kujua kila kitu - hii hutuondolea hali ya kujifunza sisi kwa sisi

6.Watanzania wengi hatuna tabia ya ku-appriciate juhudi za wenzetu - hii ipo pia kwa baadhi ya viongozi wao kwa wao

7.Watanzania walio wengi na baadhi ya viongozi wetu tunapenda utawala wa matukio na senima za viongozi kwenye vyombo vya habari

Haya na mengine mengi hayatatufikisha kwenye Tanzania tunayohubiriwa kila kukicha. Tusipoyaacha haya, tusishangae kurudi nyuma badala ya kwenda mbele.
 
1.Watanzania wengi tunajua kuongea sana pasipo kuyatenda tunayoyaongea - hii ni kwa wote ;viongozi na wananchi

2.Viongozi wetu walio wengi kipaumbele chao ni kutaka heshima na kuogopwa kuliko kutimiza majukumu yao

3.Watanzania wengi tunaushabiki hata kwa mambo tusiyoyafahamu undani wake

4.Baadhi ya viongozi waandamizi hawajui namna bora ya kuwasimamia walio chini yao ili kupata end result iliyo bora badala yake wanaongoza kwa vitisho na mikwara

5.Watanzania wengi bila kujali hadhi na nyazifa zetu tuna ulimbukeni na tunajifanya kujua kila kitu - hii hutuondolea hali ya kujifunza sisi kwa sisi

6.Watanzania wengi hatuna tabia ya ku-appriciate juhudi za wenzetu - hii ipo pia kwa baadhi ya viongozi wao kwa wao
Ukijua tatizo bila kulifanyia kazi ni upuuzi. Toa suluhu nini kifanyike.
Kwa maoni yangu ni kuipiga chini CCM
 
Huenda likawa suruhisho kwa upande wako, lakini suruhisho la kudumu ni kubadili fikra na mtazamo kwa kila mmoja wetu

Babu zetu waliishi zama za mawe za kale, uwezo wa kufikiri na kutenda mambo ulipoongezeka nao wakaendeleza zana zao, wakaweza kuzalisha hadi ZIADA.

kidogo kidogo kadiri walivyozidi kushughulisha ubongo ;wakajikuta wanavumbua moto na hatimaye chuma na leo hii tuna endeleza walipoishia....

Maendeleo yote hayo waliyopitia, walikuwa wanabadilisha CCM!?
 
hacha urongo,mashine ya kusaga kiwanda,ya kufyatua tofali viwanda,kibao cha kukunia nazi kiwanda,mashine za popcorn,juice za miwa brafnda ya juice vyote ni viwanda
 
Huenda likawa suruhisho kwa upande wako, lakini suruhisho la kudumu ni kubadili fikra na mtazamo kwa kila mmoja wetu

Babu zetu waliishi zama za mawe za kale, uwezo wa kufikiri na kutenda mambo ulipoongezeka nao wakaendeleza zana zao, wakaweza kuzalisha hadi ZIADA.

kidogo kidogo kadiri walivyozidi kushughulisha ubongo ;wakajikuta wanavumbua moto na hatimaye chuma na leo hii tuna endeleza walipoishia....

Maendeleo yote hayo waliyopitia, walikuwa wanabadilisha CCM!?
Kwanza naomba nikujuze jambo kuu!

Huwezi kuendelea kama kila unachofikiri kufanya nyuma yake kuna mamlaka imejipanga kukukwamisha. Enzi za miaka ya themanini kuna watu walikuwa na uwezo wa kutengeneza mizani lakini walikuwa wakikamatwa na kufungwa eti hawana vibali.
Kuna watu waliwahi kujitahidi kuunda siraha nao waliishia ndani eti zinatumika vibaya. Watu hawa wangeendelezwa ili wawe chanzo cha viwanda. Sasa hivi akili za vijana wetu ni mfu. Hakuna hata anayewaza kutengeneza kikapu, kila kitu tunaletewa toka China.
Sera mbovu za serikali ya CCM ndo zimetufikisha hapa. Babu zetu hawakuishi na mawazo ya ki-CCM.. \

Jaribu kuanzisha kakiwanda hata ka kutengeneza wine / juice huone TFDA, TBS, TRA, SIDO na vimamlaka kibao watakavyokuandama. Niwaachie na wengine wachangie .... ila mawazo yako mazuri japo hukutoa ni nini kifanyike.
 
Kuhusu nini kifanyike, ni kuyabadilisha hayo yote niliyoyataja kuwa chanya.

Sikatai kwamba viongozi wanaotuongoza (walioko madarakani) wanatukwamisha, nachotaka kusema ni kwamba hao walioko madarakani mind set zao zisipobadilika hata vyama vingine vikishika madaraka huenda mambo yakawa yale yale!

Kikubwa ni sisi kubadili mitazamo yetu kwani hata hao viongozi hutoka miongoni mwetu

Na uliyoyasema kuhusu TBS, TFDA, TRA, SIDO N.K ni ya kweli kabisa na hayo hutokana na nilichokisema kwenye namba nne (4)
 
A man is a property of the society.Tutaenedelea kuwa ni viongozi wabovu mpaka tustaarabike sisi kwanza vinginevyo atokee wa kimuujiza.
 
Back
Top Bottom