Yafahamu Makundi ya muziki kipindi hicho

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Hapa tusahau kidogo kuhusu Mabaga Fresh, Solid Ground Family, Hard Blasters wale wa kipindi hicho watakua wanayafahamu.

Njoo kwenye kizazi chetu ndio mziki wetu wa kisasa unaanza kuvuma kulikua ja makundi kadhaa yaliyochangamsha sana mziki wetu ndipo tukaanza kusikia Maneno kama vile BIFU.

1. East Coast Vs TMK wanaume
Hapa palikua pamoto sana haya makundi yalikua na Bifu ila nahisi lilikua la kisanii tu walifika mpaka wakaanza kutungiana nyimbo, East coast walikua na nyimbo kama ama zangu ama zao, itikadi, komaa nao, TMK walikua na nyimbo kama nyumbani nyumbani hata kama kichakani japo Tmk walibase sana kwenye kutoa burudani kiranja mkuu wa East alikua Crazy GK wadau wanasema hili kundi walikua mambo safi

Kule TMK kiranja mkuu alikua Juma Nature Mkongwe hakika ilikua burudani sana

2. Nako 2 Nako Soldiers Vs Mapacha
Hapa napo palikua patamu full hip hop mziki mtamu ndio N2n soldiers wanaibuka wakali kama Bou Nako, Gnako, lord eyes wanatamba na ngoma kama ndio zetu kuwakilisha haaa hatujaja kuwashika...hapo Mapacha kuna watu wamejaa kinyama wana nyimbo kama pasu kwa pasu..nk ila mwisho wa siku walikuja kupataka Nipe Gwara nipe tano tusiwaharibie Mapacha.

3. Kikosi cha mizinga vs N2N soldiers
Kule kuna Kala Pina nabii kokooo zilikua haziivi kabisa na N2n hawa walifika mpaka kutishiana maisha nakumbuka nipo skuli moja ya maboys tupu raia wengi walikua majamaa wa north kama unavyofahamu disco la maboys tunakamua Hip hop tu

Zilikua zikipigwa nyimbo za N2n soldiers ilikua shangwe balaa sasa DJ ajichanganye apige nyimbo za kikosi disco linaweza kuishia hapo na matusi makali, imebaki historia tu.

Hebu tukumbushe nawe unakumbuka utamu wa kundi lipi na lipi
 
We mtoto kumbe inazungumzia makundibya juzi. ongelea NUTA Jazz
Kaka nasema kwa miziki ya kileo ndio maana waona sijaweka kina Msondo ngoma hapo, Nutta jazz, Ottu jaz, Twanga pepeta, Double M sound, Stono musica, wajelajela, Njenje.
 
1.MABAGA FRESH
2.HOTPOT FAMILY
3.WATURUTUMBI
4.HOT GIRLS
5.UNIQUE SISTERS
6.WATENGWA
7.WACHUJA NAFAKA
8.WATU PORI
9.DAZ NUNDAZ
10.GANGWE MOB
11.UNIVERSITY CORNER (UVC)
12.KWANZA UNIT
13.HARD BLASTERS CREW (HBC)
14.USWAHILI MATOLA
15.SOLID GROUND FAMILY
16.WAGOSI WAKAYA


Hayo ni baadhi tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom