Dalili hatari wakati wa Ujauzito na Maandalizi ya kujifungua

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
1643779025559.png

Hizi ni dalili za hatari wakati wa ujauzito.

Uchungu wa uzazi unaochukua muda mrefu sana

Uchungu wa uzazi wa zaidi wa saa 12 kwa mama aliyerudia kuzaa (mzoefu), au uchungu zaidi ya saa 24 kwa mama anayejifungua kwa mara ya kwanza ni hatari. Uchungu namna hii mara nyingi husababisha majeraha kwa mama na unaweza kuleta madhara kwa mtoto. Vilevile pale ambapo maji ya uzazi yataanza kutoka lakini uchungu wa uzazi ukawa umekawia kwa hadi saa 12 hii inaweza kusababisha maambukizi.

Shinikizo la juu la damu
Shinikizo la damu la 160/110 au zaidi ni dharura na hatari. Tafuta msaada wa daktari haraka.

Homa
Unapopata homa au kusikia mapigo ya moyo wa mtoto yanakwenda haraka, huenda kuna maambukizi kwenye tumbo la uzazi ambayo yanaweza kumuathiri mama na mtoto. Tafuta msaada wa daktari.

Mtoto aliyelalia upande katikati ya njia ya uzazi (bila kukaa wima)
Huu ni mkao ambao hauwezi kuruhusu mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida. Operesheni hospitalini inahitajika mara moja ili kunusuru maisha ya mtoto. Mama apelekwe hospitalini haraka.

Kiunga mwana (placenta) kinapotoka nje kabla ya mtoto kuzaliwa
Tukio hili hutokea kwa nadra na linaweza kusababisha kichwa cha mtoto kugandamiza kiunga mwana na kutoruhusu damu kumfikia mtoto. Mtoto atanusurika tu kama mama atawahishwa hospitalini kwa ajili ya operesheni. Mama anapaswa kubaki akiwa amejiegemeza kwenye mikono na magoti yake sehemu ya kiunoni ikiwa imeinuliwa juu kupunguza mgandamizo kwenye kiunga mwana.

Vifaa na mahitaji kwa ajili kujifungua
Kwa ajili ya kujifungua salama, andaa vifaa vifuatavyo:
Zingatia, nunua vifaa kwa ajili ya mama na mtoto tu
Taratibu zote za kujifungua zinatolewa katika vituo vya afya na wakunga waliobobea katika maswala ya uzazi
  • Sabuni na maji kwa ajili ya kunawa mikono mara kwa mara, kumsafisha mama, na kusafisha vifaa tiba. Vilevile andaa beseni au bakuli kwa ajili ya kunawia
  • Nunua boksi dogo la glovu (surgical gloves) kulinda afya ya mama, mtoto na mkunga.
  • Kamba zilizotakaswa na dawa au kuchemshwa, au riboni au kibanio maalum kwa ajili ya kufunga au kubana kitovu. Zinapatikana duka la dawa.
  • Andaa kanga, blanketi la watoto wachanga, nepi, n.k. kwa ajili ya kumfuta na kumfunika mtoto ili apate joto la kutosha punde tu atakapozaliwa.
  • Maji kwa ajili ya kunywa na usafi.
Muhimu
Unapokwenda kliniki jitahidi kuuliza mahitaji muhimu na vifaa vya kuandaa kwa ajili ya kujifungua. Watakueleza vyema ili ujipange kuepusha purukushani siku ya siku.
 
Back
Top Bottom